Ufugaji wa nyuki
una maana kuwa makundi ya nyuki yanamilikiwa na mmiliki ambaye atalinda usalama
wa kila kundi, kutunza kundi, na kuvuna asali na mazao mengine ya nyuki kwa
wakati ufaao, na kwa
mtindo ambao
utabakiza asali ya kutosha kwa matumizi ya nyuki katika kila kundi. Ubora na
uwingi wa mazao ya nyuki huweza kuongezeka na kuweza kutoa aina nyingi zaidi za
mazao hayo. Makundi ya nyuki yanaweza kuhamishwa, jambo ambalo huitwa “uhamaji”
kwa njia hii mfugaji nyuki anaratibisha makundi yake kuruka kufuata mazao
fulani fulani, huku kwa kufanya hivyo anaongeza muda zaidi wa majira ya nyuki
na kuongeza mavuno ya mazao ya nyuki.
2.1 Mavuno katika
makundi ya nyuki
Ø Nyuki hukusanya
majimaji matamu yaitwayo nekta kutoka kwenye maua na kutengeneza asali tokana
na nekta hiyo. Nekta huhifadhiwa juu ya masega yaliyo ndani ya mzinga pia
kwenye kuta za mzinga, hii nekta ikitumika kwa lishe ya nyuki na pia ghafi ya
kutengeneza nta na kutunza joto.
Ø Nta
inatengenezwa na nyuki katika tezi zao zitoazo nta. Chanzo cha nguvu na chanzo
ghafi cha kutengeneza nta ni asali.
Ø Nyuki anapofyonza
nekta kutoka katika maua, chavua hunasa katika nywele zilizo kifuani mwake.
Nyuki hupukuta chavua hii na kuifinyanga kuwa vidonge vidogo, akitumia miguu
yake ya nyuma.
Ø Pindi nyuki
atuapo kwenye maua mbalimbali ya mimea inayoshabihiana kielimu viumbe, maua
huchavushwa kwa chavua za kike au kiume.
Ø Uchavushaji
mtambuka huleta matunda makubwa na mbegu kubwa.
Ø Mabonge ya
chavua husukumizwa ndani ya vyumba vya masega, ambamo hutengenezwa na kufikia
hali ya kuwa mkate wa chakula cha nyuki. Jambo hili hufanyika ndani ya kila
masega.
Ø Nyuki vijana
hutumia ute ute kutoka katika tezi maalum katika vichwa vyao, ambao huutumia
kubadili mkate wa nyuki kuwa maziwa ya nyuki na jeli ya kifalme ambavyo, pamoja
na mayai na viluwiluwi vya nyuki, huitwa nyuki kinda: tazama mchoro Na. 3.
Ø Nyuki kinda huwa
ndani ya masega kwa ndani na juu ya mkate wa nyuki, katikati ya kundi la nyuki.
Nyuki huchukua nafasi ya mahali palipokuwa mkate wa nyuki ulipoondolewa kwa
kuunda maziwa ya nyuki.
Ø Nyuki
wanaoanguliwa kutoka katika masega huwa ni vibarua, malkia na madume nyuki.
Ø Nyuki vibarua
husafisha vyumba vya nyuki kinda kwa kutumia gundi nyeusi, hutengeneza asali kutokana
na nekta, hutengeneza mkate wa nyuki kutokana na chavua, halafu kubadili mkate
wa nyuki kuwa maziwa ya nyuki na jeli ya kifalme.
Ø Nyuki wa mzinga
hutoa jasho la nta ambalo hutumika kutengeneza vyumba katika masega.
Ø Baadaye nyuki
ndani ya mzinga huwa nyuki walinzi ambao hulinda mzinga kwa kutumia mwiba wenye
sumu ulio matakoni mwa nyuki aina hii, na hivyo kumdhuru adui.
Ø Nyuki vibarua na
nyuki malkia ndio hutengeneza sumu katika tezi, na kuihifadhi katika kifuko
kilicho karibu na mwiba unaodunga.
Ø Baadaye nyuki
vibarua hubadilika kuwa watafutaji wa lishe na hukusanya nekta na chavua.
Ø Nyuki hawa pia hukusanya
nta, gundi na utomvu kutoka katika miti na mimea, ambavyo huvichanganya wao
ndani ya gundi nyeusi baada ya kuongeza nta na mate.
Ø Gundi nyeusi
hufanya kazi muhimu katika kuhifadhi joto muafaka katika mzinga kwa sababu
gundi hiyo hutumika kuziba matundu katika kuta za mzinga.
Ø Joto hutokana na
nyuki kupumua, na ile hewa ya joto inajaa na kutoka nje (ikiwa na harufu ya
nyuki) na ina manufaa ya kitabibu.
Ø Wakati mwingine
maji huletwa kwa kupoza joto. Maji hutunzwa katika utumbo wa asali tumboni mwa
nyuki. Maziwa ya nyuki na nyuki kinda ndivyo pekee vilivyo na unyevunyevu
mwingi. Mazao mengine ya nyuki huwa makavu au yana sukari kali mno (concentrated
sugar).
Ø Nyuki, makundi
ya nyuki, makundi mapya na malkia ni mazao ya mzinga.
Ø Mavi ya nyuki ni
zao la manufaa ambalo bado halijatumika kutengenezea bidhaa. Mavi haya ni ya
usumbufu pia, kwa mfano yakidondoka kwenye nguo au kwenye vioo vya madirisha yanaweka
uchafu mweusi.
2.2 Uvunaji na
usindikaji
Lengo la ufugaji
nyuki ni kuvuna mazao kutoka kwenye mzinga, na kuchavusha maua. Mzinga bora
hutoa asali, na bila shaka hili ndilo zao linalofahamika sana. Lakini asali
siyo zao lenye maana zaidi.
Uchavushaji maua
na uoto asili ndiyo mazao ya maana zaidi kuliko asali, ukilinganisha uzalishaji
kila mzinga, au kwa kila hekta. Mazao kama vile asali na mkate wa nyuki huvunwa
kutoka ndani ya mzinga, lakini mabonge ya chavua na sumu ya nyuki hukusanywa
kutoka nje ya mzinga kwa kutumia vikapu maalum miguuni. Kwa kutoa jeli ya kifalme
(royal jelly) lazima mzinga uundwe rasmi kwa kazi hiyo. Mfugaji nyuki hukusanya
mwenyewe gundi nyeusi iliyonata ndani ya kuta za mzinga.
Uvunaji
Ni muhimu kuvuna
mazao ya nyuki kwa muda upasao katika msimu wa nyuki. Chavua huhamishwa, na
uchavushaji hutokea mwanzoni mwa msimu wa nyuki, maziwa ya nyuki hupatikana
muda kidogo
baadaye, lakini
ni wakati wa kundi linapo endelea kukua. Wakati kundi linakua huunda masega
mapya. Baadaye kundi huweza kujigawa katika makundi madogo mawili au zaidi, kwa
kujitenga
kabisa. Asali
hutunzwa zaidi baada ya kundi kujitenga, lakini haijakomaa bado mpaka mwisho wa
msimu wa nyuki au hata baadaye zaidi. Nyuki hutumia gundi nyeusi ukiisha msimu
huu lakini kabla
nyuki kuanza
msimu wao wa baridi. Uvunaji wa wastani badala ya kuvuna na kufilisi mazao ya
mzinga ni uvunaji unaofaa kuendeleza uzalishaji wa kundi. Agrodok Na. 32 –
Ufugaji nyuki inaeleza zaidi kuhusu misimu ya nyuki na utunzaji nyuki kila
msimu.
Usindikaji
Katika kuvuna
mazao ya nyuki, mfugaji nyuki huvuna mazao ya msingi, mapya yatokanayo na
nyuki. Kutokana na upya (ubichi), mazao hayo yana thamani nyingi zaidi kwa
matumizi ya kitabibu
(madawa). Kwa
ajili ya lishe, usindikaji na kuuza, mfugaji nyuki husindika mazao ya nyuki
hatua ambayo kwa kawaida (lakini siyo kila mara) huongeza thamani ya zao kwa
wanunuzi. Asali huondolewa katika masega, nayo nta huchujwa. Hatua hii huitwa
kutenganisha. Asali kisha hujazwa katika chupa, nayo nta safi hutolewa kwa kuchemsha
masega matupu. Nta hii ina thamani zaidi na inadumu zaidi kuliko nta ghafi,
lakini asali ndani ya chupa ina thamani ndogo sana kulinganisha na masega mapya
baada tu ya kuvunwa.
2.3 Mnyororo wa
thamani na uuzaji
Mnyororo wa
uzalishaji ni mzunguko unaoanza na ufugaji wa nyuki, yaani kundi la nyuki na
mfugaji wake. Hapa ndipo ubora wa mazao unapoanzishwa. Tazama mchoro Na. 4. Iwapo
nyuki hawatunzwi vizuri, ni vigumu kufanya lolote kuboresha hayo mazao ya
nyuki. Baada ya kuvuna, mazao huchujwa au hukaushwa, lakini mfugaji anaweza
kuuza bila kusindika. Asali ambayo imepondwapondwa au iliyotiririshwa, au iliyopitishwa
katika mtambo wa kuzungusha kasi (centrifuge) inauzwa upesi zaidi na kwa hiyo
kuleta pato bora. Kwa sababu hii na sababu nyinginezo, kwa mfano tishio la kuganda/kuchenguka
(crystallize), asali huuzwa katika nchi nyingi ikiwa ya hali hizo tatu na vema
zaidi ikiuzwa na mfugaji nyuki mwenyewe. Thamani inayoongezeka katika asali
iliyochujwa na katika nta iliyosafishwa kwa njia hizi humnufaisha mfugaji
nyuki. Iwapo mfugaji nyuki hapati pato la kutosha kutokana na mazao hayo, basi uzalishaji
utapungua.
Uuzaji
Mfugaji nyuki
huuza asali moja kwa moja kwa mlaji (tazama mchoro Na. 5) biashara reja reja au
kwa uwingi kwa mfanya biashara (biashara ya jumla) au kwa kampuni inayonunua
asali (kampuni ya
upakiaji asali).
Kampuni ya upakiaji asali katika chupa husindika asali kwa kuchemsha, kuchuja,
na kupakia ndani ya chupa; kwa njia hii thamani huongezwa tena ingawa asali
sasa si mpya tena, hivyo imepoteza sifa za asali mpya (mbichi). Aina hii ya
usindikaji ni nzuri ikiwa uzalishaji ni mwingi kuliko mahitaji ya wanunuzi, kwa
sababu muda wa kuendelea kuuza asali huongezeka, vile vile unadhifu wa asali
huongezwa na kuwezesha kuuza nchi za nje. Kama hii hatua ndiyo inafanyika,
huweza kuwa na manufaa kwa mfugaji nyuki au Chama cha Wafugaji nyuki kuipelekea
kampuni kama hiyo. Sura ya 14 inazungumzia suala hili kwa kina.
2.4 Miradi ya ufugaji
nyuki
Katika miaka ya
hivi karibuni kumekuwapo ongezeko la mwamko wa kuandaa miradi ya ufugaji nyuki
katika maeneo yenye uwezekano wa kuzalisha asali na mazao mengine ya nyuki. Walengwa
kwa kawaida huwa ni wafugaji nyuki au vyama vya wafugaji nyuki, lakini huweza pia
kuwa ni kampuni ya usindikaji asali inayoshirikiana na vyama vya wafugaji
nyuki. Katika kuandaa mradi, ni muhimu kuwa uundwe vizuri, yaani, walengwa
wasaidiwe kweli kweli na lengo lililokusudiwa lifikiwe hasa. Katika maeneo
mengi, uzalishaji asali ni kidogo mno na kiwango hafifu kiasi kwamba matarajio
ya uuzaji hayawezi kutimizwa. Kwa hiyo basi katika hatua ya kuandaa mradi budi
kupata
ushauri wa
wataalam wenye uzoefu katika ufugaji nyuki katika nchi za joto. Ufugaji nyuki
ni mojawapo ya biashara ngumu na zenye utata, lakini mara nyingi watu wasio
wafugaji nyuki hufikiri kwamba ni kazi rahisi sana. Kuwa na mizinga ya kisasa
hii pekee haileti ongezeko la uzalishaji; kwa kweli hakuna tofauti baina ya
ufugaji nyuki kwa mtindo wa asili na wa kisasa, bali kati ya vifaa (zana) za
kiasili na za kisasa. (Mchoro Na. 6 na Na. 7). Maarifa ambayo wafugaji nyuki wamerithisha
vizazi kwa vizazi katika eneo fulani, ndiyo yatumike kama chanzo cha habari
katika kuandaa mtindo wa ufugaji nyuki wa eneo hilo. Ushirikiano baina ya
wafugaji mbalimbali wa nyuki na wataalam wa ufugaji nyuki katika nchi za joto
ni wa muhimu vile vile. Agrodok Na. 32 – Ufugaji nyuki katika nchi za Joto –
kinafafanua hali hii katika sura inayojadili huduma kwa nyuki katika majira
mbalimbali ya msimu na kuhusu aina mbalimbali za mizinga.
Uchavushaji
Ikiwa nyuki
atafyonza nekta kutoka katika ua, nayo chavua kutoka kwenye vikonyo vya sehemu
ya kiume ya ua hunata kwenye vinywele vya nyuki huyo. Nyuki atuapo kwenye ua
jingine chavua kidogo hupukutika na kudondoka kwenye sehemu ya kike ya ua. Hii
ndiyo huitwa uchavushaji mtambuka. Jinsi ua linavyofanana kimchoro: kushoto ni
mchoro ukionesha ua toka juu, kulia ni mchoro ukionesha ua lililopasuliwa juu
hadi shina la ua.
3.1 Kanuni na Jinsi
inavyotendeka
Punje ya chavua,
ambayo huwa na nukleasi mbili, ikipeperushwa hutua na kuota juu ya
sehemu ya kike ya ua na kuendelea kukua ndani ya mrija wa chavua mpaka katika
shina la uke wa ua. Shina la uke hutunza vijiluwiluwi vya yai visivyochavushwa
bado, na kondo, ambavyo vikishachavushwa vitakomaa kuwa mbegu au tunda.
Moja ya nukleasi
zile mbili katika mrija wa chavua, hupenyeza kila kiluwiluwi cha yai na
kukichavusha. Nukleasi ya pili hupenyeza katika kondo la viluwiluwi vya mayai
na kuvichavusha kwa ufanisi zaidi kuleta matunda bora zaidi na mbegu bora
zaidi. Matunda haya na mbegu, navyo hukua na kuwa mimea bora. Hali hii
haifanyiki kama uchavushaji unatendeka kwa kutumia chavua na mbegu ya kike ya
ua lile lile. Mara nyingi uchavushaji wa ua kwa mbegu ya kike ya ua hilo
hilo
hauwezekani. Nyuki huruka kutoka ua moja hadi jingine na kwa vile nyuki mmoja
mmoja hufuata maua ya aina moja tu, uchavushaji mtambuka unahakikishwa
kutendeka baina ya maua ya mashina mbalimbali lakini ya jamii moja. Nyuki ni
muhimu kwa uchavushaji wa miti yenye maua yenye jinsia moja moja au jinsia
zote. Mimea yenye jinsia mojamoja, kwa mfano mipapai, na mti uitwao kiwi huwa
na maua ya kiume katika mti mmoja na maua ya kike katika mti mwingine. Miti
mingi ina maua yenye jinsia zote. Mimea inayochavushwa kwa chavua zinazopeperushwa
na upepo, kwa mfano, nyasi, hiyo tu huwa na chavua nyingi na inaweza kutekeleza
uchavushaji bila kutegemea nyuki.
Nyuki na Maua
Muda kamili kwa
uchavushaji hutofautiana kati ya aina ya mmea na mwingine, lakini huwa ni pale
ua litoapo harufu zaidi kabisa. Kwa hiyo basi nyuki hutembelea ua hilo kwa
wingi wakati fulani fulani wa siku. Nekta hukusanyika kabla ua halijafunguka.
Baada ya ua kufunguka, nekta huanza kukauka kwa hewa pale uwiano wa unyevunyevu
unapopungua jinsi siku inavyomalizika, hasa katika nchi za joto.
Kwa kila mmea,
wapo aina ya nyuki maalum wanaochavusha mimea hiyo vema zaidi. Nyuki asili wa
eneo fulani, kwa mfano aina ya Apis cerana ya nchini Asia, ambao
hutoa asali kidogo kuliko nyuki bora waitwao Apis mellifera, ni bora
zaidi kwa uchavushaji na wanaweza kufugwa maalum kwa kazi hii. Nyuki wasiouma
wanaweza pia kufugwa kwa kazi ya uchavushaji. Wachavushaji wengine kama popo na
ndege, huweza kuwa washindani kwa kula chavua na nekta. Aina za mimea ambazo hutembelewa
au kuchavushwa kwa msaada wa nyuki ni pamoja na michungwa, nectarine,
peaches, lychees, kiwi, mipapai, miembe, parachichi, mapera, mibuni,
michai, pamba, minazi, mitikiti maji, mibuyu, maharage na migomba itoayo mbegu.
Mimea baadhi ambayo hutembelewa na nyuki hainufaiki na uchavushaji, kwa mfano
mahindi na migomba. Ufanisi wa uchavushaji mtambuka kwa msaada wa nyuki unaweza
kuchunguzwa kwa kuzuia sehemu ndogo ya shamba isifikiwe na nyuki kwa kutumia
wavu wenye matundu madogo.
3.2 Uzalishaji
Matokeo ya
uchavushaji mtambuka katika uoto asili ni kwamba mimea huwa na uzao bora zaidi.
Ndege na wanyama wanaokula mbegu na matunda, kwa mfano popo, kuchakuro na
tumbili pia
hufaidika kwa
matunda makubwa na mbegu. Uchavushaji wa mazao kwa kawaida huhitaji nyuki wengi
zaidi kuliko wanavyopatikana kawaida kwa hiyo mfugaji nyuki huangika mizinga
kadhaa ya nyuki karibu au ndani ya shamba kuhakikisha wapo viumbe wa kueneza chavua
ya kutosha katika eneo hilo.
Idadi ya makundi ya nyuki
Idadi kamili, na
ukubwa wa makundi ya nyuki ni muhimu sana. Iwapo yapo makundi mengi zaidi ya
nyuki kuliko yanavyofaa ustawi wa makundi yenyewe na uzalishaji wa asali, basi
mizinga ya nyuki itakuwa na upungufu wa chavua na nekta. Mfugaji nyuki hapo atalazimika
kulisha chakula makundi yake ya nyuki au abadili makundi mara kwa mara. Hii ni
muhimu hasa kwa mazao katika mabanda ya kioo ya mazao (green houses), ambamo
nyuki hawawezi kutoka nje kukusanya chavua na nekta zaidi. Iwapo makundi ni madogo
sana, hayataweza kuchavusha mimea ya kutosha. Kwa ajili ya uchavushaji katika
mabanda ya bustani kama hizi, ni muhimu zaidi makundi ya nyuki yasiwe mengi mno
pia yasiwe makundi makubwa mno. Iwapo maua hayapo ya kutosha, nyuki
watayaharibu. Nyuki wasiouma na wale waitwao nyuki bambi au nyuki manyoya,
hutafuna sehemu za kiume za maua.
3.3 Faida za
uchavushaji
Kwa kuongeza
makundi ya nyuki kuzidisha uchavushaji, wakulima na wafugaji nyuki wanaweza
kupata manufaa zaidi kuliko kupata asali tu. Kwa kuonesha ukweli kwamba
uchavushaji ni kipato, tutatoa mfano wa faida inayopatikana kwa mkulima na kwa
mfugaji nyuki anayekodisha makundi yake ya nyuki kwa mkulima mwingine. Mfugaji
nyuki anaweza kuwakodisha wakulima wengine mizinga ya nyuki kwa kipindi cha
msimu mmoja wa zao. Mfugaji nyuki anaangika mizinga miwili ya nyuki katika
hekta moja ya zao la alizeti, kwa mfano. Bila kuwapo nyuki wa kukodiwa, mkulima
anapata kilo 500 za alizeti, kwa hekta, wakiwapo nyuki wa kukodiwa, anapata kilo
850, hivyo kilo 350 zimeongezeka. Mfugaji nyuki anapata pia kilo 50 za asali
kwa kila kundi la nyuki ambazo ni jumla kilo 100 kwa hekta. Alizeti ikiuzwa
shilingi 1,700 kwa kilo, na asali kwa shilingi 1,000
kwa kilo, baada
ya kutoa gharama, mkulima atapata mara 3 ½ zaidi kutokana na uchavushaji kuliko
kutokana na asali tu. Mkulima atamlipa mfugaji nyuki shilingi 25,000 kwa kila
mzinga wa nyuki, ambayo jumla ni shilingi 50,000/= kwa hekta. Kwa hiyo mfugaji
nyuki hupata shilingi 150,000/=. Hii ni mara 1 ½ zaidi kulinganisha na mapato
kutokana na asali pekee. Mkulima atapata shilingi (350 – 50) = shilingi 300
zaidi kwa kila hekta, kwa msaada wa nyuki. Hii ni asilimia 60 zaidi kuliko
mavuno bila kukodi nyuki. Jedwali Na. 2 inaonesha hili ongezeko muhimu la mbegu
na matunda
kimchoro kwa
hekta kwa kila mzinga wa nyuki, pamoja na ada ya uchavushaji.
Iwapo mfugaji
nyuki ni mkulima vile vile wa zao hilo, pato lake litakuwa kubwa zaidi.
Wafugaji nyuki ambao pia ni wakulima wanaweza kupata pesa zaidi kwa kupanda
mazao yanayonufaika na uchavushaji
mtambuka.
3.4 Mkataba wa
uchavushaji
Uchavushaji kwa
kufikiria kipato, ndio zao kuu la ufugaji nyuki. Hii ni kweli kwa kila mzinga,
pia na kwa kila hekta iwapo mazao yanayopandwa kutoa matunda au mbegu ni aina
ambayo hunufaika na
uchavushaji
mtambuka. Ambaye hunufaika zaidi ni mkulima, kwa mantiki, ana deni la kumfidia
mfugaji nyuki. Mkulima anapaswa kumlipa mfugaji nyuki ada ya kuchavushiwa
mazao, kwa kutunza
vizuri hao
nyuki. Mara nyingi ada hii ni asilimia ndogo kutoka katika mapato
yaliyoongezeka kutokana na mazao, lakini kwa mfugaji nyuki ada hii inaweza kuwa
kubwa zaidi kuliko mapato yanayotokana na uuzaji asali. Kwa kuhamisha hamisha
makundi ya nyuki, mfugaji nyuki anaweza kufanya uchavushaji kuwa biashara yenye
faida sana. Mfugaji nyuki anaweza kuafikiana mkataba na mkulima. Mkataba kama
huu utahusu mambo manne:
Ø ada ya
uchavushaji (kwa sababu mfugaji nyuki anamletea faida zaidi mkulima)
Ø huduma kwa makundi
ya nyuki
Ø usafirishaji wa
mizinga ya nyuki kwenda na kurudi kutoka kwenye mazao shambani
Ø bima ya
kupunguza athari, kama vile matukio ya wizi, uharibifu Ada ya uchavushaji budi
imudu gharama za mfugaji nyuki za kuhudumia mizinga ya nyuki. Gharama hizi
zinaweza kuwa kubwa hasa katika mabanda ya kioo ya bustani na sehemu kama hizi zilizofungiwa
kwa sababu makundi ya nyuki lazima yatunzwe na kulishwa kwa ratiba maalum.
Usafirishaji wa mizinga ya nyuki kwenda na kurudi kutoka shambani nao ulipiwe,
na tahadhari ya uharibifu pia ilipiwe.
Umuhimu wa kusambaza habari
Mara nyingi
mkulima siye anayeagiza kuwa nyuki waletwe, kimsingi hasa kwa sababu hana
habari. Iwapo mfugaji nyuki ndiye anayeagiza kwamba nyuki waletwe, basi yeye
atadaiwa na mkulima au mwenye ardhi, ada ya kuletewa nyuki. Kwa vile mwenye
ardhi au mwenye shamba hunufaika zaidi
kutokana na
uchavushaji uliofanikiwa (tazama mchoro 10) hata kama mfugaji nyuki atavuna
asali nyingi, siyo vema yeye alipe ada. Hivyo ni muhimu Vyama vya Wafugaji
nyuki na Wataalamu Washauri wa kilimo wasambaze habari za matakwa ya pande zote
mbili. Wakulima kadhaa hununua mizinga ya nyuki kwa uchavushaji ili kupunguza
matumizi. Kwa vile hawana ujuzi wa ufugaji nyuki,
wakulima
hawawezi kutunza vizuri makundi yao ya nyuki na kwa hiyo uchavushaji haufikii
kiwango cha kutosha. Hii pia humaanisha kwamba mfugaji nyuki anayeuza mizinga
ya nyuki hupata pesa kidogo kutoka mzinga bora. Uamuzi wa kununua mizinga ya
nyuki ni wa hasara kwa wahusika wote wawili.
4 Asali
Nyuki hukusanya
nekta kutoka katika maua. Nekta ni maji yenye ladha ya sukari ambayo muundo
wake hutofautiana kati ya jamii mbalimbali za mimea. Nyuki wanao kusanya nekta
huchukua nekta
ndani ya matumbo
na kuipeleka ndani ya mzinga na kuwagawia nyuki wasiotoka nje ya mzinga. Hawa
nyuki wasiotoka nje ndio huirekebisha nekta kwa kupunguza unyevu ili iwe nzito
na kisha
huijaza katika
vyumba vya masega, ambamo huanza kubadilika kuwa asali, na ndipo vyumba vya masega
huzibwa kwa nta.
Sifa na muundo
Asali
inayotokana na maua ya jamii moja huitwa asali ya maua sare, kwa mfano. Asali
ya maua ya mti wa msufi au asali ya maua ya migomba, au asali ya maua ya mibuni
(kahawa), n.k. Iwapo asali inatokana na nekta kutoka maua ya jamii mbalimbali,
hapo huitwa asali ya maua mchanganyiko.
Nekta huundwa
kwa kiasi kidogo cha chavua, ambayo ina mwonjo kwenye asali. Chavua hukutwa
kwenye sehemu ya kiume ya maua ya mimea wowote, ambapo ndipo nyuki huipata. Ipo
chavua kidogo tu katika asali siku hizi, kama ukiangalia chembe ya chavua kwa darubini
kali, unaweza kufahamu asili ya chavua hiyo kwa aina ya mimea itokanapo, kizazi
nasaba (genus) na kizazi chanzo (species) Nyuki pia hukusanya asali umande.
Haya ni matone madogo ya maji ambayo huning’inia kwenye maua nyakati za
asubuhi, pia kutoka kwenye nekta kutoka sehemu zozote zisizokuwa za maua, kwa
mfano kinga ua (calyx), shina ua (flower stalk) au jani halisi.
Asali iliyotokana na asali umande au iliyotokana na asali jani huwa na vitu kadhaa
vinavyopatikana kwenye maua (petal) shina la mmea au majani, pia huwa na
kiwango kikubwa cha chachu na vumbi vumbi. Asali ya aina hii huganda kwa
haraka. Pia mara nyingi ina rangi ya giza kidogo, ladha yake ni chungu na asali
hii ina haribika upesi zaidi.
4 Asali
Nyuki hukusanya
nekta kutoka katika maua. Nekta ni maji yenye ladha ya sukari ambayo muundo
wake hutofautiana kati ya jamii mbalimbali za mimea. Nyuki wanao kusanya nekta
huchukua nekta
ndani ya matumbo
na kuipeleka ndani ya mzinga na kuwagawia nyuki wasiotoka nje ya mzinga. Hawa
nyuki wasiotoka nje ndio huirekebisha nekta kwa kupunguza unyevu ili iwe nzito
na kasha huijaza katika vyumba vya masega, ambamo huanza kubadilika kuwa asali,
na ndipo vyumba vya masega huzibwa kwa nta.
Sifa na muundo
Asali
inayotokana na maua ya jamii moja huitwa asali ya maua sare, kwa mfano. Asali
ya maua ya mti wa msufi au asali ya maua ya migomba, au asali ya maua ya mibuni
(kahawa), n.k. Iwapo asali inatokana na
nekta kutoka maua ya jamii mbalimbali, hapo huitwa asali ya maua mchanganyiko.
Nekta huundwa
kwa kiasi kidogo cha chavua, ambayo ina mwonjo kwenye asali. Chavua hukutwa
kwenye sehemu ya kiume ya maua ya mimea wowote, ambapo ndipo nyuki huipata. Ipo
chavua kidogo tu katika asali siku hizi, kama ukiangalia chembe ya chavua kwa darubini
kali, unaweza kufahamu asili ya chavua hiyo kwa aina ya mimea itokanapo, kizazi
nasaba (genus) na kizazi chanzo (species) Nyuki pia hukusanya asali umande.
Haya ni matone madogo ya maji ambayo huning’inia kwenye maua nyakati za
asubuhi, pia kutoka kwenye nekta kutoka sehemu zozote zisizokuwa za maua, kwa
mfano kinga ua (calyx), shina ua (flower stalk) au jani halisi.
Asali iliyotokana na asali umande au iliyotokana na asali jani huwa na vitu kadhaa
vinavyopatikana kwenye maua (petal) shina la mmea au majani, pia huwa na
kiwango kikubwa cha chachu na vumbi vumbi. Asali ya aina hii huganda kwa
haraka. Pia mara nyingi ina rangi ya giza kidogo, ladha yake ni chungu na asali
hii ina haribika upesi zaidi. Asali iliyokomaa ni sukari kali sana ambayo kwa
kawaida huwa na maji chini ya asilimia 20, na sukari asilimia 80. Sukari hii
hatimaye huganda na asali yenyewe huwa ngumu. Sukari inayounda asali ni aina
iitwayo kiini sukari kama vile sukari unga nyeupe (glucose) na sukari
matunda (fructose). Iwapo katika mchanganyo wa sukari unga nyeupe ni
mwingi kuliko sukari matunda, basi asali itaganda upesi zaidi. Tazama sura ya
13 – Viwango na Masharti. Baadhi ya asali huganda ikiwa bado ndani ya masega
hata kabla ya kuvunwa. Hata hivyo, kutokana na joto jingi lililomo, asali ina
ganda ndani ya mzinga baada ya muda mrefu zaidi, kuliko inavyoganda baada ya
kuvunwa. Wakati wa uvunaji, vumbi vumbi huingia kwenye asali na kuongeza kokwa
za kusaidia kuganda.
Asali kabla ya kusindikwa
Asali iliyo
ndani ya masega ina kiasi kidogo cha chavua, nta, gundi nyeusi na huenda pia
sumu ya nyuki. Kiasi cha vitu hivyo vilivyomo katika asali hutegemea kiasi cha
muda ambao asali imekuwa ndani ya masega. Iwapo asali inatoka katika masega
yaliyotumika kwa kutunza nyuki kinda, basi itakuwa na gundi nyeusi kutoka
kwenye utando nofu (membrane) wa vifukofuko (cocoons). Hata hivyo ni
kiasi kidogo tu cha chavua huwa katika asali. Vitu vingine ambavyo hunata
kwenye nyuki wakati wanaruka hewani, vinapopukutishwa pamoja na chavua, navyo
huingia kwenye asali kwa kiwango kidogo. Asali huwa na vimeng’enya, yaani vitu
fulani fulani vya kimaisha vyenye kemikali kutoka katika mate ya nyuki na maji
maji ya matumboni mwa nyuki, pamoja na protini au protini tata (oligopeptides).
Asali halisi ina madini kidogo sana, viiniyoga (spores) na vitamini.
Asali iliyosafishwa
Asali ambayo
imesafishwa kwa mashine pewa (ya kuzungusha asali kwa kasi ndani ya chombo)
inafanana sana na asali itokayo kwenye masega. Hata hivyo asali iliyovunjwa
vunjwa au iliyokamuliwa inaweza kuwa na kiasi kingi cha chavua. Iwapo kuna
kiasi kikubwa cha mkate wa nyuki katika masega, asali hii hasa ni mchanganyiko
wa asali na chavua. Hii asali iliyoboreshwa, pamoja na kuwa na viinilishe katika
chavua, inayo pia kiasi kikubwa cha vitamini, madini, na
kemikali hai za
kimaumbile. Iwapo nyuki kinda watakamuliwa pamoja na asali, basi asali itakuwa
na protini
nyingi zaidi, vitamini, madini, na maji maji. Aina tatu au nne za maada
zikichanganyika, yaani, asali, mkate wa nyuki, maziwa ya nyuki, na nyuki kinda.
Hii ndiyo sababu asali iliyovunwa na
kukamuliwa
kutoka mizinga ya kiasili huwa ni ya kiwango duni na haidumu kwa muda mrefu,
lakini ni bora katika viinilishe. Inawezekana hata hivyo kuvuna asali ya kisasa
na mazao mengineyo kila aina peke yake kutoka kwenye mizinga rahisi ya
kienyeji. Tazama aya zifuatazo hapa chini juu ya uzalishaji na usindikaji
Manufaa ya asali kwa afya
Asali inaweza
kuokoa maisha kwa watu na wanyama walio katika hatari kiafya. Sukari chanzo, na
hasa sukari matunda iliyomo, huwa msingi mkuu. Asali inanyonywa haraka sana
ndani ya nyama hai. Huwa na kiasi kidogo cha maada za mazao ya nyuki kama vile chavua,
maziwa nyuki, gundi nyeusi, sumu ya nyuki. Hizi maada kwa pamoja husababisha
tiba kooni, utumbo na tumboni kwenye ngozi na nyama hai. Kimeng’enya glucose
oxidase huanza kutoa hewa ya “hydrogen peroxide” (H2O2) baada ya asali
kuchanganywa na maji, mate au maji maji katika jeraha. Hii “hydrogen
peroxide” ina uwezo wa kuua vijidudu. Hewa hii inatolewa polepole kwa hiyo
ina manufaa zaidi na haisababishi maumivu kama dawa madukani yenye jina hilo, inayotibu
majeraha. Asali inapopashwa joto, kimeng’enya kinapoteza uasili wake, (tazama
pia aya 13.5) kwa hiyo asali ghafi, na mpya ndiyo inayofaa zaidi kwa tiba. Asali
kutoka nyuki wasiouma (Apis melliponini) wanaopatikana katika nchi za
joto, ni tiba bora zaidi kuliko ile itokanayo na nyuki halisi. Asali hii pia
ina unyevunyevu (asilimia zaidi ya 24), na ni nyepesi, lakini haichachi upesi,
vile vile ina kiwango cha juu cha tiba zinazozuia vijidudu vya maradhi, ina
protini butu (short protein) na vimeng’enya, ambavyo huzuia kuchacha
asali.
Matumizi
ya asali katika tiba
Asali hutumika
toka zamani kijadi kupunguza matatizo ya pumu, uchovu wa ulevi, na kuzimia
kutokana na ugonjwa wa kisukari. Pia inasaidia kuleta usingizi, na kuongeza
nguvu mwilini. Sukari matunda hufyonzwa upesi ndani ya nyama hai, bila
kuzuiliwa na kemikali iitwayo “insulin” inayoundwa katika tezi ndani ya
kongosho. Kwa hakika, hii haina maana kuwa asali iongezwe bila tahadhari katika
chakula cha mgonjwa wa kisukari. Asali huongezwa maji kwa matumizi ya kutibu
kikohozi au kuboresha uwezo wa dawa hii. Haya ndiyo manufaa muhimu ya asali
katika chakula na katika viwanda vya madawa. Protini butu na gundi nyeusi ni
vitu muhimu katika muanufaa ya asali kitabibu. Asali hutumika pia kwa majeraha
ya kuungua na majeraha mengine kwa sababu ya uwezo wa asali wa kunyonya na
kusafisha na kuponya majeraha. Hewa ya “hydrogen peroxide” inayotolewa
wakati asali inaongezwa maji, huua vijidudu katika majeraha na huleta maumivu
ya ghafla. Kupunguza maumivu haya, asali inachanganywa kwa vipimo sawa na
mafuta, siagi, au mafuta ya nyama. Jinsi jeraha linavyoendelea kupona, punguza
kipimo cha mafuta. Kutokana na
kiwango kidogo
cha chavua kilichomo, asali inaliwa kuongeza ukinzani kwa athari ya homa ya
vumbi na mzio wa chavua (pollen allergy). Kwa kutibu maradhi haya
mawili, asali inayofaa ni ile
itokayo eneo la
maskani ya mgonjwa. Asali huwa ina chembechembe mbalimbali zinazo peperushwa
kwa sababu nyuki wanaporuka hunasa chembechembe hizi katika vinywele vyao
hatimaye chembe chembe zinapukutishwa pamoja na chavua. Tazama pia sura ya
tano. Asali ya nyuki wasiouma hutumika kwa kuponya maradhi yale yale kama asali
ya nyuki wa kawaida. Huko Amerika ya Kusini, inatumika pia ikiwa asali ghafi
kwa kutibu ugonjwa wa mboni ya jicho. Matumizi ya asali kwa ajili ya tiba
hufanana pote duniani kiasi cha kushangaza, lakini zipo tofauti kidogo kila
eneo kikanda. Wafugaji nyuki wanaweza kutekeleza kazi muhimu ya kukusanya habari
kama
hizi ambazo kwa
kiasi kikubwa bado hazijaandikwa.
Uvunaji asali na uchujaji
Asali huvunwa
vema zaidi baada ya kilele cha msimu wa nyuki. Ubora wa asali hubadilika wakati
wa kuundwa ndani ya mzinga, kwa hiyo uchaguzi wa masega yatakiwayo kuvunwa ndiyo
sababu
mojawapo itakayo
changia katika ubora wa asali hiyo. Uchujaji wote hufaa ufanyike mara tu baada
ya kuvuna, ambapo asali bado ni tepetepe. Wakati wa kuondoa masega kutoka ndani
ya mzinga, moshi usipulizwe ndani kupita kiasi. Asali iliyoundwa punde ndani ya
masega inaweza kujazwa katika vyombo na kuuzwa bila kukawia, kama asali
isiyochujwa. Ni muhimu kutenganisha masega kabla ya kuchuja, pia ni bora masega
yavunwe yaliyokomaa. Ni vema usivune masega ambayo asali yake haijakomaa au
yenye mkate wa nyuki na nyuki kinda iwapo inatakiwa asali safi yenye unyevunyevu
kidogo sana. Kutenganisha masega yenye rangi mbalimbali na kuchuja tofauti
tofauti kutamsaidia mfugaji nyuki kuwa na aina mbalimbali za rangi nyeupe kidogo
na ladha hafifu. Asali
iliyopondwa
pondwa hufanywa kwa kvunjavunja na kuchanganya masega ya asali.
Hii ni njia ya kiasili ya kusindika asali.Asali aina hii hufanana na asali
iliyo na siagi ya maziwa.
Namna
mbalimbali za kuchuja
Asali inaweza
kutenganishwa kwa njia mbalimbali kutoka kwenye masega. Kwa kutiririsha na
kuelea, kwa kukamua, au kwa kutumia mtambo unaozungusha pipa kwa kasi kwenye
mhimili. Njia ya kutiririsha hutumia tofauti kati ya uzito maada (density).
Katika kutumia njia ya kuelesha, nta huelea juu ya asali iliyopashwa joto, na katika
kutiririsha, asali hudondoka ndani ya chombo kutoka katika masega. Njia za
kutiririsha, kuelesha, na kukamua hueleweka kama njia za jadi za ufugaji nyuki,
lakini iwapo zimefanyika kwa ustadi, ni njia bora na hutoa asali nzuri. Njia za
kutiririsha na kuelesha mara nyingi husababisha unyevunyevu mwingi, hasa majira
ya mvua. Kabla ya kukamua, masega hufunikwa kwa waya wenye matundu madogo ili kuzuia
nta. Asali inayochujwa kwa njia hii siyo nyeupe sana kama ile itokanayo na
kutiririsha au kutumia mtambo unaozungusha pipa kuchuja asali. Waya zilizosukwa
kwa kuchujia ni bora ziwe za plastiki au chuma maalum kisichopata kutu kuliko
nyuzi za nguo kwa vile zitahakiki usafi na kuepuka mabaki ya nyuzi za nguo
ambazo husababisha asali kuganda. Kitabu. cha Agrodok Na. 32 kinaelezea njia
kadha za kukamua asali kwa mkono na kwa zana ndogo.Kutoa asali kwa kutumia mtambo
wa pipa linalozunguka kwa kasi
ni njia bora kwa masega yatokayo katika
mizinga ya nyuki ya aina za sanduku (top bar) au mizinga za aina ya vyumba
vidogo vidogo. Kitabu cha Agrodok Na. 32 kinaeleza vizuri zaidi juu ya mtambo
wa kutoa asali kwa kuzungusha pipa maalum kwa kasi kuchuja asali kwa ufanisi.
Masega
yaliyovunjwa yanaweza kuwekwa ndani ya kikapu au gunia na kuzungushwa kama
inavyofanywa katika mtambo wa pipa. Masega yenye vifuniko vilivyoziba yatengwe
peke yake kwa vile yanaweza kuwa na moshi ndani yake. Vifuniko vinaweza
kutumika kwa chakula, au kuhifadhiwa kwa kulisha nyuki makundini mwao. Unapotumia
mtambo wa kuzungusha pipa, zaidi ya asilimia 70 hadi 80 ya asali huchujwa iwapo
ni tepe tepe na bado haijaganda ndani ya masega.
Kuhifadhi
Vigezo muhimu
kufikiriwa wakati wa kusafirisha, kuhifadhi na kusindika asali ni hali ya unyevunyevu
wa hewa na joto la hewa
Mazingira
yaliyofumwa
Kwa kuhifadhi na
kusindika asali, ni vema zaidi kuwa na kibanda cha kufumia hewa ambamo hali
zote muhimu (usafi na hewa kavu) vinaweza kuhakikiwa. Shughuli zote za
kusindika asali zifanyike
katika mazingira
ya hewa kavu. Wakati wa kusafirisha na kuhifadhi asali ya masega, hata kama
asali imefunikwa kwa kuzuia hewa, bado asali inaweza kunyonya unyevunyevu
kutoka nje. Muda ufupishwe
iwezekanavyo
unaolazimu asali kuwa wazi katika hali ya hewa nyevunyevu. Vyombo vya kuhifadhi
asali vifungwe vikilazimu kuwa katika hewa nyevunyevu, pia masega nayo
yafunikwe. Kipimo chaladha ya sukari
ni cha manufaa sana kukuonyesha uwingi wa maji katika asali uliyonayo kwa hatua
mbalimbali
Kupunguza
unyevunyevu wa asali
Iwapo asali ina
unyevunyevu mwingi, hali hii hutokana na uvunaji mbaya, lakini pia huweza kutokana
na matunzo na usafirishaji baada ya kuvuna. Kuanika nje asali baada ya kuvuna,
ni njia duni. Kuondoa unyevunyevu baada ya kusindika husababisha viini lishe
kupotea hewani kama mvuke, hivyo kuteremsha sana kiwango cha maada zinazoweza
kuwa mvuke, hivyo kuteremsha sana kiwango cha ubora na ladha ya asali. Njia
inayofaa zaidi ya zote kwa kupunguza unyevunyevu wa asali ni kuhifadhi kwa siku
chache asali ya masega kamili ndani ya chumba chenye hewa kavu. Hewa kavu ndani
ya chumba itanyonya unyevunyevu wa asali hata kama masega yamezibwa kwa nta.
Kusindika na kupakia
Asali inaweza
kupakiwa bila kuchujwa. Asali mpya ina harufu nzuri ya maua yaliyotoa nekta
(majimaji matamu). Kiwango cha vimeng’enya na viinilishe vya kielimu viumbe ni
cha juu zaidi katika asali mpya ambayo haijachemshwa.Baadaye asali huganda na
kuwa ngumu. Ndipo rangi ya asali huwa nyeupe nyeupe. Asali inaweza kuwekewa
malai (cream), kwa kuichemsha kwanza kwa muda mfupi halafu kuikoroga.
Asali iliyosindikwa kwa njia hii huwa na ladha nzuri sana.Siku chache baada ya
kuvuna asali, weka asali ndani ya vyombo visivyoingiza hewa hata kidogo. Kwa
kujaza vyungu au mitungi kwa urahisi, tumia chombo chenye vali (valve),
(mchoro Na. 14). Hifadhi asali katika vyombo vidogo vya kioo au ndoo za
plastiki zenye mifuniko inayofunga madhubuti au vyombo vya bati ambayo vimepakwa
mafuta maalum ya taa (liquid paraffin) au rangi ya plastiki, au ambavyo
vimepakwa rangi nyingine inayohifadhi ubora wa vyakula Viwanda vikubwa
huchemsha asali ili kuiweka ikiwa maji maji na kuzuia isichache kama
unyevunyevu utakuwa wa kupita kiasi. Baada ya kuchemsha, asali huchujwa na
halafu kupakiwa katika vyombo vya kioo. Utaratibu huu huitwa pia kusafisha
asali. Kupitia utaratibu huu wa kuchemsha, hata hivyo asali hupoteza ubora
fulani. Upya wake hupotea, lakini huweza kuhifadhiwa kwa muda mrefu zaidi ikiwa
asali nzuri nyeupe nyeupe. Hali hizi ni nzuri ikiwa asali inakusudiwa kuuzwa
katika maduka ya vyakula.Asali huweza kuanza kuchachuka wakati inapohifadhiwa
iwapo hali ya unyevunyevu ni zaidi ya asilimia 19. Uchachukaji unaweza kuzuiwa
kwa kuchemsha asali kwa joto la nyuzi 55 hadi 60 celcius kwa masaa 8 halafu
kuipoza haraka baada ya muda huo. Lakini asali ikichemshwa kwa masaa mengi
zaidi, itapoteza ladha nzuri, harufu, vimeng’enya na viini lishe.
5 Chavua
Nyuki hukusanya
chavua kutoka kwenye sehemu za kiume za maua. Chavua hunata kwenye vinywele vya
mwilini mwa nyuki wakati nyuki anapofyonza majimaji matamu.Nyuki hupukutisha
chavua iliyo kwenye vinywele vyake kwa kutumia miguu yake ya mbele ambayo ina
machanuo. Nyuki huongeza mate yake kuweza kulowanisha chavua na kuifinyanga
katika umbo la tufe (mpira). Nyuki huruka akiwa na chavua ndani ya vikapu hai
vilivyo kwenye miguu yake ya nyuma na kuelekea kwenye mzinga. Nyuki wanaobaki
ndani ya mzinga hupokea chavua hiyo na kuiingiza
katika vyumba
vya masega kwa kutumia vichwa vyao, pamoja na kuongezea mate na asali kidogo.
Ndipo sasa nyuki huunda na kuivisha mkate nyuki.
Jinsi na muundo
Chembe za chavua
zina gamba gumu ambalo huitwa “exine” kwa kiingereza. Gamba hili mara nyingi
lina vinasio vinavyowezesha chavua kunata vizuri katika vinywele mwilini mwa
nyuki. Gamba hili limefunikwa kwa utando wa nta, ambao hufanya chavua isiweze kuyeyushwa
na ndiyo sababu pia chavua kuweza kukauka sana na kudumu ndani ya ardhi kwa
miaka mamilioni. Licha ya ugumu wa hili gamba, nyuki huweza kulilainisha na
hatimaye baada ya wiki kadhaa huunda maziwa ya nyuki au maziwa ya kifalme kwa
kulisha nyuki kinda kutokana na gamba hili. Kila fungu la chavua hutoka katika
mimea yenye kushabihiana. Kila lundo la chavua lina mfumo maalum wa protini,
linaloweza kutambulisha viini lishe vinavyopatikana humo kielimu viumbe kwa lishe
ya nyuki. Nyuki katika makundi hutembelea mimea ya aina mbalimbali, kwa hiyo
husababisha rangi mbalimbali zionekanazo katika mafungu ya chavua
yaliyokusanywa, ambayo huwa na muundo mzuri iwapo lakini chavua haitokani na
maua yenye kasoro, kwa mfano maua ya mahindi.Wakati nyuki vibarua warudipo
katika mizinga, mfugaji nyuki anaweza kutambua chanzo cha chavua kwa kuangalia
rangi ya chavua iliyokusanywa. Muundo na thamani ya kitabibu ya chavua hutofautiana
baina ya aina za mimea. Kwa kuangalia chavua kwa kutumia darubini kali
inawezekana kutambua aina ya mimea na makundi ya kielimu viumbe ya mimea hizo
(tazama pia aya 13.6). Utaalamu huu huitwa kwa kiingereza, “melissopalynology”.
Chavua huundwa kwa mafuta ghafi, mafuta yenye harufu, vitamini E (tocopherol),
wanga, protini ghafi (km. peptides, short protein au oligopeptides)
tindikali ya pantothenic, anthocynins, carotenoids tindikali za ferulic,
pamoja na vimeng’enya na madini kama chuma, manganese, zinc na viiniyoga.
Matumizi kwa tiba
Kemikali asili
zilizomo kimaumbile katika chavua kama vile anthocyanins, carotenoids
na flavenoids husaidia kutakasa damu kwa kuvamia seli hatari. Chavua
huongeza nguvu na afya mwilini mwetu, husaidia uwezo wa kiakili na kukuza
mtiririko wa damu kuingia kichwani. Vile vile chavua ni chanzo kidogo cha
vitamini B2, B6 na B12.
Chavua hutumika
kwa kuboresha uwezo wa uzazi, kupunguza maradhi ya uzeeni, kupambana na dalili
za kufunga uzazi uzeeni, kupanuka kwa tezi kibofu (prostate), kukosa
raha, na kuwa na
mfadhaiko. Kutokana na
kuwa na vyanzo vingi vya lishe, chavua huliwa na wanariadha kukamilisha lishe
yao kitaalam. Chavua kavukooni, na mafua. Kwa vile chavua ni ngumu kuyeyushwa
tumboni hutumika kuponya matatizo ya tumbo.
Kukamua na kuhifadhi
Upatikanaji wa
chavua huwezekana tu mwanzoni mwa msimu, katika maeneo yenye uoto wenye mimea
ya maua, na penye makundi mengi ya nyuki na yenye afya. Kukusanya chavua
kunaathiri maendeleo ya makundi ya nyuki kwa vile kundi linaweza kupungukiwa
chavua ya kutengeneza mkate wa nyuki na maziwa ya nyuki, ambavyo vinahitajika
kulisha nyuki kinda. Kiasi cha chavua budi kibakizwe, kwa mfano, kwa kupanga
ratiba ya ukusanyaji chavua ifanyike siku chache kwa wiki, au kwa kutembelea
makundi kwa mzunguko kukusanya chavua.
Uvunaji
Chavua hukusanywa kwa
msaada wa chombo cha kutega chavua.Chombo hiki ni nyavunyavu ambazo nyuki
hulazimishwa kupita wanapohitaji kuingia ndani ya mzinga. Matundu ya kupitia
hufanywa madogo (ya mviringo au pembe tatu) na kusababisha chavua ipukutishwe
kutoka katika vikapu vinavyotunza chavua vilivyo miguuni mwa nyuki, na chavua
kudondoka na kuangukia ndani ya kabati maalum kwa kazi hiyo ili nyuki wasiweze
kuifikia humo kabatini kuichota. Rangi mbalimbali za chavua hutumbukia ndani ya
kabati na kuchanganyikana. Nyuki wa porini, kwa mfano wale wa nchini Afrika, au
waliozoeshwa hali ya Afrika, wanakarahishwa sana na kunyang’anywa
chavua.Hawapendi unyang’anyi huu wa chavua waliojikusanyia. Kwa hiyo, budi
kukusanya chavua kutoka katika masega baada ya kuundwa kuwa mkate wa nyuki
Kuhifadhi
Chavua
huharibika upesi kwa hiyo inaweza kuachwa mbele au chini ya mzinga kwa siku
moja tu. Chavua budi ikaushwe mara tu baada ya kukusanywa kuzuia isiote kuvu,
na kuongeza muda wa kuuzwa.Unyevunyevu wa chavua hupungua wakati wa kukausha,
kutoka kama asilimia 25 (inapovunwa) hadi wastani wa asilimia 11. Chavua mpya inaota
kuvu baada ya siku moja, na kuvu husababisha sumu inayodhuru afya. Ili kuweka
chavua kwa muda mrefu, ichanganye katika asali, lakini usichanganye kuzidi
kiwango cha mchanganyiko cha asilimia 10.Chavua ihifadhiwe katika sehemu kavu,
yenye giza ili kudumisha viini lishe vinavyotakiwa. Chupa za rangi ya kikahawia
ni bora kwa kuhifadhia kuliko chupa za kioo cheupe.
6 Mkate wa nyuki
Nyuki huunda
mkate wa nyuki kutokana na chavua ambayo huikusanya. Katika sura ya tano,
tulielezea jinsi nyuki wa ndani ya mzinga wanavyo ingiza chavua ndani ya vyumba
vya masega kwa kutumia vichwa
vyao, wakitengeneza chavua katika umbo la punje punje ndogo, zilizochanganywa
na asali kidogo na mate ya nyuki. Mchanganyiko huu hubadilishwa kikemikali
kutokana na vimeng’enya
vilivyomo katika mate ya nyuki, na ute ute uliomo matumboni mwa nyuki. Kwa
msaada wa vijiumbe hai na hali ya unyevunyevu na joto ndani ya mzinga (nyuzi
joto 35 – 36) mchanganyiko huo
hubadilika na kuwa mkate wa nyuki mnamo wiki mbili.
Jinsi na muundo
Mkate wa nyuki
ni chanzo cha protini, mafuta, viini lishe na vitamin kwa mahitaji ya lishe ya
nyuki. Ni mali ghafi kwa utengenezaji maziwa ya nyuki na jeli ya kifalme,
ambayo nyuki yaya huunda wakisaidiwa na maji maji yanayokutwa katika vichwa vya
nyuki (Tazama pia sura ya 7). Mkate wa nyuki una viini lishe tofauti na chavua
(Tazama jedwali Na. 3 katika sura ya 5). Mkate wa nyuki una kiasi kidogo zaidi
cha protini kuliko chavua, lakini huyeyuka upesi zaidi. Kiasi cha unyevunyevu
hupungua kidogo hadi asilimia 13 au 14 baada ya kukausha. Vile vile mkate wa
nyuki una viini lishe vifuatavyo:
Ø protini zenye
viinilishe muhimu vya amino acid
Ø vitamin C, B1, B2, E, H (biotin),
K, P (rutin), tindikali ya nicotin, tindikali ya folic na
tindikali ya pantothenic
Ø rangi hai za carotenoid
na anthocyaninv
Ø vimeng’enya
vitokanavyo na sukari (saccharase), wanga (amylase) na fosfati (phosphatase)
Ø vikolezo vya
ladha (flavonoids)
Ø madini zaidi ya
aina 25, kama vile chuma, kasiamu (calcium), magnesia (magnesium) fosforasi
(phosphorus), potasiamu (potassium), shaba, zinki (zinc)
na seleniamu (selenium) na viiniyoga.Kwa vile kiwango cha tindikali ya
maziwa (lactic acid) ndani ya mkate wa nyuki ni zaidi ya mara sita ya kiwango
kilichomo katika chavua, hivyo hivyo kiwango cha uchachu ni cha juu, na kwa
hiyo mkate wa nyuki hauoti kuvu na vimelea vingine kwa urahisi kama ilivyo kwa
chavua.
Manufaa yake kwa afya
Muundo
Mchanganyiko wa
kemikali zilizomo kimaumbile katika mkate wa nyuki huufanya uweze kuzuia na
kutibu magonjwa mbalimbali. Kiwango cha juu cha vitamini B kilichomo huboresha
chembechembe hai za mwili kuchuja lishe yake vizuri pia hufanya mfumo wa fahamu
kuwa makini. Vile vile vitamin B huongeza uzalishaji wa chembe chembe nyekundu
za damu na hemoglobin huongezeka katika damu kwa watoto na kwa watu
wazima pia.Mkate wa nyuki na chavua vyote vina manufaa kwa mfumo wa kinga mwilini
na mfumo wa kuchelewesha uzee. Mkate wa nyuki pia huboresha ustahimilivu wa
wanariadha michezoni kwa kuwapa nguvu za ziada. Mkate wa nyuki pia una uwezo wa
kuzuia maradhi, huzuia bacteria na virusi mbalimbali na kusaidia kupunguza
homa. Pia husisimua misuli tishu (tissue) za ukuaji na uhuishaji, na husafisha
damu. Mkate wa nyuki unasababisha mwili kuburudika na kutulia, na kupunguza
kasi ya kuzeeka mwili. Huongeza hamu ya kula chakula, na kuwaongezea nguvu watu
wazee na kuharakisha wagonjwa kupona.
Matumizi
ya mkate wa nyuki
Katika tiba kwa
dawa zitokanazo na nyuki, mkate wa nyuki hutumika kwa ufanisi kabisa ukichanganywa
na njia nyinginezo kwa kuwatibu watu wazee na watoto. Mkate wa nyuki
unashauriwa kutumiwa kwa upungufu wa damu, ugonjwa wa ini, kisukari, na
magonjwa ya njia za
koo na tumbo kwa
mfano kuvimba utumbo mkubwa, kukosa haja kubwa, kuharisha kama inavyoshindwa
kutibiwa kwa dawa za hospitali za kuua vijidudu mwilini. Mkate wa nyuki
huteremsha kiwango cha mafuta yenye athari yaitwayo “cholesterol”, na kurekebisha
mpangilio wa mafuta mwilini na kusafisha damu chafu. Mkate wa nyuki pia huboresha
mwenendo wa kongosho, nyongo na ini, na kuteremsha kiwango cha msukumo wa damu.
Mkate wa nyuki, kama asali, pia nao hupendekezwa kwa kuzuia matatizo ya tezi
kibofu (prostate). Mkate wa nyuki pia husaidia sana kwa wagonjwa wanaoanza
kupata nafuu baada ya upasuaji.Vilevile husaidia kutatua tatizo la ugonjwa wa
kusahau matukio ya wakati uliopita. Mkate wa nyuki huwa bora sana kwa wataalamu
wanaofikiri sana katika uvumbuzi.
Uzalishaji, uvunaji na kuhifadhi
Mkate wa nyuki
hunyonywa mwilini mwetu kwa urahisi zaidi kuliko chavua, pia ni rahisi zaidi
kupatikana kwa mfugaji nyuki. Iwapo njia bora za uvunaji zinatumika, usumbufu
kwa makundi ya nyuki, huweza kupunguzwa hadi kiwango cha chini iwezekanavyo. Uzalishaji
kwa asili wa mkate wa nyuki kwa kutegemea mizinga ya nyuki umeelezwa hapo juu.
Mkate wa nyuki unaweza kuzalishwa kwa uwingi zaidi kwa kufanya baadhi ya
mizinga isiwe na nyuki malkia. Mkate wa nyuki utakuwa wa ziada katika makundi
yasiyo na malkia, kwa sababu hakuna nyuki kinda na pia kwa sababu maziwa ya
nyuki hayaundwi kutokana na mkate wa nyuki uliomo. Masega yenye mkate wa nyuki
uliokomaa unaweza kuvunwa. Hasara kidogo zaidi hufanywa katika makundi ya nyuki
kama njia hii inatumika kuliko kwa kuvuna chavua moja kwa moja. Mkate wa nyuki
unaweza pia kukwanguliwa kutoka kwenye masega. Chombo maalum ambacho kinaitwa
“mango ya mkate wa nyuki” hupatikana kwa kukwangua. Katika ukaushaji wa mkate
wa nyuki, unyevunyevu wake uteremshwe kutoka asilimia 20 hadi 14. Kutokana na
mabadiliko katika muundo, mkate wa nyuki unaweza kuhifadhiwa
kwa muda mrefu
zaidi kuliko chavua. Hata hivyo mkate wa nyuki hatimaye nao huota kuvu.
Mkate wa nyuki
ulio mpya unaweza kutunzwa katika jokofu (friji), au kugandamizwa pamoja na
asali, au kukaushwa. Mkate wa nyuki uliokaushwa huweza kuliwa kama mapande au
baada ya kuundwa katika maumbo mbalimbali, pia huweza kuwa kiungo cha vyakula vingine.
Mkate wa nyuki una ladha nzuri zaidi na ni rahisi zaidi kunyonywa katika miili
yetu kuliko unga wa chavua.
7 Jeli ya kifalme
Nyuki wachanga
huongeza ute ute kutoka katika tezi maalum zilizopo kichwani na kuongezea
kwenye mkate wa nyuki wanaoumeza, ndipo maziwa ya nyuki na jeli ya kifalme
huundwa. Nyuki huhifadhi maziwa ya nyuki ndani ya vyumba vidogo vya masega
vyenye viluwiluwi vya nyuki. Viluwiluwi vya nyuki vibarua, madume, na nyuki
malkia hula maziwa ya nyuki, lishe ambayo huwakuza. Maziwa ya nyuki yana aina
mbili za viinilishe, ute ute usio na rangi, na ute ute rangi ya maziwa. Jeli ya
kifalme ina mchanganyiko ulio sawa na aina hizi mbili za viinilishe, ambavyo
maziwa ya nyuki inayolisha madume na nyuki vibarua huwa ina aina ya uteute usio
na rangi. Nyuki
hutengeneza
maziwa ya nyuki kwa uwingi zaidi katika juma la kwanza la umri wao, baada ya
majuma matatu kupita, huacha kutoa uteute wa aina hii na wanaanza kutoka nje ya
mzinga kufuata maji matamu ya maua (nekta) na chavua. Kwa ajili ya kutengeneza
jeli ya kifalme ni muhimu wawepo nyuki wachanga wengi ndani ya makundi.
Jinsi na muundo
Maziwa ya nyuki
kwa ajili ya malkia ndiyo chakula chenye lishe zaidi, na ndiyo maana huitwa
jeli ya malkia, vile vile malkia hupewa chakula hiki zaidi kuliko nyuki
vibarua. Hii ndiyo sababu mojawapo
malkia hunenepa
zaidi na kuwa na nguvu zaidi kuliko nyuki vibarua. Malkia anaweza kuishi kwa
miaka michache kulinganisha na maisha ya nyuki vibarua ambao huishi kwa mwezi
mmoja hadi sita tu kutegemea na majira wanapoishi. Muundo wa maziwa ya nyuki
hutegemea kwa kiasi mkate wa nyuki na chavua (tazama pia jedwali Na. 3 katika
sura ya 5). Maziwa ya nyuki yana uwingi wa vitamini B1, B2, B6, folic acid,
inositol, pantothenic acid, vitamin C na vitamin E (tocopherol).
Jeli ya kifalme huwa na viinilishe vingine pia yaani peptides, lipids,
sterols, mafuta ya harufu nzuri, wenye vimeng’enya, anthocyanins,
carotenoids, flavenoids, ferulic acids, vile vile ina madini na
masalia ya viiniyoga kutoka kwenye mkate wa nyuki. Ute ute unaotoka katika tezi
ambao huhitajika kwa kuyeyusha mkate wa nyuki, huongeza lishe huru ya protini
na protini rahisi (oligopeptides) katika maziwa ya nyuki kuzidi iliyoko
ndani ya mkate wa nyuki. Hivi viinilishe vikichanganyika na mafuta ghafi (fatty
acids) huunda kiinilishe maalum kiitwacho “royalisin”
kinachotokana na uchambuzi wa mafuta ghafi. Kwa sababu hii, jeli ya kifalme ina
asili ya tindikali, na mwonjo wa uchachu hata kama ni mpya. Jeli ya kifalme
huweza kuhifadhika kwa siku chache (siku 5 tu) bila kuwekwa katika jokofu, wala
kugandishwa, lakini huweza kuhifadhiwa kwa kuchanganywa na asali.
Manufaa kwa afya
Sifa
Uchambuzi wa
kitindikali ya “royalisin” hufanya jeli ya kifalme kuweza kupambana na
bakteria wa aina mbalimbali lakini inashindwa kupambana na kuvu. “Royalisin”
ina maumbo ya tufe za “gamma
globulin” ambazo ni
tindikali za protini katika mfumo wa kinga. Huu uchambuzi vile vile una
“asparagin 16%” ambayo huhitajika kwa ukuaji wa nyama za miili hai. Karibu nusu
ya mafuta yaliyochambuliwa huundwa kwa tindikali mfumo wa 10-hydroxy – 2
– decanoic acid (10 HDA) ambao huchangia katika ukuaji wa mwili, mfumo
wa tezi na mfumo wa kinga. Jeli ya kifalme iliyo mpya inaundwa kwa asilimia 2
hadi 15 ya 10-HDA, ambayo pia huweka kiwango cha ubora (asilimia isiyopungua 5
hupendekezwa).
Matumizi
Jeli ya kifalme
hupendekezwa kwa tiba ya tumbo, ini, na matatizo ya uyeyushaji chakula tumboni,
msukumo mwingi wa damu, kupoteza hamu ya chakula, upungufu wa uzito, uchovu,
kukosa utulivu, kukosa usingizi, ujauzito wenye matatizo, adha ya kusimama
hedhi, matatizo ya uzeeni, muda wa mapumziko baada ya kuugua, na kuongezea nguvu
wanariadha. Jeli ya kifalme inahesabika kama chakula cha kufanya mtu awe
mkakamavu, mwenye afya na asiyechoka. Huweza kuliwa katika hali ya asili, au
baada ya kuchanganywa na asali. Huweza kuuzwa mara nyingine katika chupa za
kioo au vidonge vililvyosagwa na kupakiwa katika vifuko vidogo na kuchanganywa na
aina kadhaa za sukari kwa mfano “sorbitol”. Katika nchi nyingine, jeli ya
kifalme huongezwa katika vinywaji vya kujenga nguvu. Jeli ya vidonge iliyo
kaushwa na kusagwa na kupakiwa katika vifuko vidogo ndiyo hutumika kwa tiba
zitokanazo na nyuki. Kwa matumizi nje ya mwili, jeli ya kifalme huongezwa
kwenyemafuta ya
kujipaka, kwa sababu hukuza au kuhifadhi urembo wa ngozi ya mwili. Husisimua
ukuaji wa mwili na nywele.
Uzalishaji na usindikaji
Kwa uzalishaji
wa jeli ya kifalme budi wawepo nyuki wachanga wengi ndani ya mzinga; hali hii
ni ya kawaida mwanzo wa msimu wa nyuki. Mfugaji nyuki anaweza kuongeza idadi ya
nyuki wachanga kwa njia mbalimbali. Anaweza kuleta kundi zima la nyuki kinda kutoka
kwenye mzinga mwingine siku chache kabla nyuki kinda hawajaanguliwa. Vile vile
anaweza kupukuta nyuki kutoka kwenye masega ya kundi tofauti. Nyuki wachanga
wasioweza kuruka bado husalia kwenye masega, nao walioweza kuruka hurudi kwenye
mzinga walikotoka. Hali hii huwezesha kuwa na kundi la nyuki wa uzalishaji
asali na jingine moja au zaidi kwa kusaidia makundi ya kupata nyuki wachanga,
masega na mkate wa nyuki. Mkate wa nyuki wa kutosha, ambao ndio sehemu kuu ya
jeli ya kifalme, na asali, vinahitajika katika kundi la nyuki wa uzalishaji kwa
kulisha nyuki wachanga. Uzalishaji wa jeli ya kifalme hufanikiwa zaidi katika
kundi la nyuki lenye malkia, lakini ndani ya mzinga sehemu ya kuzalisha jeli ya
kifalme budi malkia aondolewe.
Njia ya kwanza: kukata masega
Bila kutumia
vifaa maalum, inawezekana pia kuwezesha nyuki kuunda vyumba vingi vipya vya
kujaza jeli ya kifalme kwa kukatakata kingoni upande wa chini wa masega yenye
mayai ya nyuki katika sehemu ya mzinga isiyo na malkia. Ndipo nyuki huunda
vyumba vipya vya mayai ya malkia kwa dharura. Vyumba vya mayai ya malkia huwa na
idadi kati ya 10 na 50 kutegemea ukubwa wa kundi la nyuki, idadi ya nyuki
wachanga, msimu, na uoto (miti, maua).
Njia ya pili: vidau bandia vya
plastiki au nta
Mfugaji nyuki
anaweza pia kutumia vichupa vidogo (vidau) vilivyotengenezwa kwa nta au
plastiki
ngumu (PVC).
Vidau vya nta vinaweza kutengenezwa kwa kijiti kilichochongwa kwa vipimo
vinavyofaa kikigandamizwa katika nta yenye joto. Hivi vidau, vya bandia
hugundishwa au kufungwa (tazama mchoro Na. 17) upande wa chini wa ubao, kadri
ya vidau 15 kwa kila kibao, na kasha mfugaji nyuki huweka yai la nyuki au nyuki
kinda wa siku moja ndani ya kila kidau. Njia hii
inaitwa “kubebesha” na hufanywa kwa kutumia kifaa chenye kufanana na kalamu.
Shughuli hii ifanyike kwa uangalifu ili kuepuka kudhuru nyuki kinda au mayai ya
nyuki. Mayai ya nyuki au nyuki kinda waliolala usawa wowote budi wahamishwe kwa
mlalo ule ule kuepuka kiluwiluwi kisikose hewa kwa kuzamishwa ndani ya maziwa ya
nyuki endapo yai litageuzwa juu chini. Matokeo ya ubebeshaji yanaoneshwa katika
mchoro Na. 18: nyuki hutengeneza vidau kwa ajili ya jeli ya kifalme.
Njia ya tatu: kijumba cha awali cha
nyuki kinda
Kwa kutumia
mtindo ule ule kama hapo juu vijumba/vidau vya plastiki (PVC) huwezesha malkia
mwenyewe kutaga mayai katika vidau. Vidau 100 tu huwekwa katika kasha la umbo
wa mraba, kwa mfano yale makasha yanayoundwa na kampuni ya NICOT yanayoitwa “Cupularva”.
Nyuki malkia hufungiwa ndani ya kasha hili. Nyuki wafanyakazi huweza kuingia na
kutoka kupitia katika nafasi maalum iliyo achwa kupitisha nyuki wafanyakazi
(ambayo lakini haimtoshi nyuki malkia kupita), wapeleke lishe kwa malkia huyo.
Katika kundi bora, itachukua siku moja hadi nne kwa malkia kujaza vidau vyote 100.
Kisha vidau kujaa, husogezwa katika mzinga na kufungwa katika fremu zilizo ndani
ya mzinga. Njia hii huhakikisha kuwa mayai ya nyuki hayaharibiki (kwa kushikwa
mara nyingi).
Kuvuna
Iwapo utafuata
njia mojawapo ya zilizoelezwa hapo juu, mnamo siku tatu utaweza kufikia ujazo
wa juu kabisa wa jeli ya kifalme ndani ya kila kidau, ambao ni robo gramu hadi
3/10 ya gramu. Jeli ya kifalme huweza sasa kukusanywa kutoka kila kidau kwa
kutumia kifyonzeo cha mrija wa kioo (pipette) au kijiko kidogo (tazama mchoro
Na. 19). Pia kipo kifaa kinachotumia pampu
ndogo ambacho kinasaidia kufyonza kwa ufanisi zaidi. Jeli mpya ya kifalme huweza
kuhifadhiwa kwa siku chache tu
katika hali ya hewa ya kawaida. Kwa hakika jeli ya kifalme inaweza kuhifadhiwa
kwa muda mrefu zaidi
ndani ya jokofu (friji) kubwa, au kama itachanganywa na asali, lakini hapo itabidi mchanganyiko
usizidi asilimia 3 hadi 5, kuzuia jeli ya kifalme kuchachushwa. Iwapo jeli ya
kifalme itakaushwa
kitaalamu kwa baridi kali, inaweza kuhifadhiwa kama unga unga, katika joto la
hewa ya kawaida. Kwa
vile uzalishaji wa jeli ya kifalme ni kazi ya kutumia nguvu kazi ya mfugaji
nyuki, na mavuno ni madogo sana, bidhaa hii ni ya bei ghali sana. Vile vile
mfugaji nyuki anazuru mizinga mara kwa mara, hivyo inatakiwa afuge makundi ya
nyuki wenye asili ya utulivu.
8 Nyuki kinda
Nyuki kinda ni
mkusanyiko wamayai, viluwiluwi na funza (pupae)wa nyuki walio ndani ya masega.
Tazama mchoro Na. 20.Viluwiluwi na funza wa
nyuki ni chakula hasa cha lishe. Uvunaji wa nyuki kinda ni jambo baya kwa usitawi
wa kundi la nyuki, kwa hiyo viluwiluwi na funza wa nyuki wa kiume ndivyo
huvunwa kwa kawaida kwa sababu kundi la nyuki halitegemei sana aina hizi za
vizawa. Nyuki kinda vile vile angalau kwa uchache, ni mazao yatokanayo na kuvuna
asali, hasa kutoka makundi ya nyuki wasiofugwa, tazama mchoro Na. 21. Muundo wa
nyuki kinda, hasa katika hatua ya
viluwiluwi ni sehemu ya maziwa ya nyuki. Katika hatua ya funza wa nyuki,
viinilishe vingi vifaavyo kwa
ukuaji hubadilika kuwa protini na mafuta.
Manufaa kwa afya
Mkate wa nyuki
huliwa na watu katika nchi kadha kama chakula cha asili, kikiwa pamoja na
masega, au kama viluwiluwi na funza wa nyuki. Barani Afrika, viluwiluwi na
funza wa nyuki huondolewa kutoka katika masega na kutumiwa kwa mapishi
mbalimbali. Nchini Indonesia, masega yaliyo na nyuki kinda wa aina ya nyuki
waitwao Apis cerana, ambao ni nyuki wa asili huko, masega huuzwa sokoni.
Vijumba vya masega na nyuzi za vijumba vyenye rangi ya kahawia itokanayo na
viluwiluwi, huongezwa viungo kuunda vyakula vya kijadi vyenye ladha nzuri
kabisa. Katika nchi za Ulaya Mashariki, wafugaji nyuki hutafuna nyuki kinda wa
kiume kwa sababu ya homoni zipatikanazo kutoka katika chakula hicho. Hutumika
kutibu matatizo ya afya uzeeni na kuharakisha kupata nguvu baada ya
kuugua. Vile vile huleta nguvu za ziada mwilini, mfano, kwa wanariadha. Madawa
yatokanayo na nyuki kinda dume hupatikana vile vile barani Asia.
Uzalishaji, uvunaji na kuhifadhi
Nyuki kinda wa
kiume huanguliwa kiasili kipindi cha mwanzo wa msimu. Iwapo tayari yapo masega
yenye nyuki kinda wa kiume na maji sukari yatokanayo na maua na pia chavua
vinaendelea kuongezeka,
nyuki kinda wa kiume wataanguliwa. Nyuki kinda aina hii ni asilimia isiyozidi
kumi tu ya kundi zima. Baada ya nyuki kinda wa kiume ndipo hutengenezwa mayai
ya kuanguliwa malkia.
Kwa vile kuvuna
nyuki kinda ni jambo lisilofaa kwa maendeleo ya kundi, na kwa utoaji wa asali
baadaye, ni vizuri zaidi kuvuna nyuki kinda wa kiume, na hata hao wavunwe
kidogo tu. Madume ya nyuki hujamiiana na malkia waliobalehe na huwa na jukumu
hili muhimu ndani ya kundi wakati wa kipindi cha maji sukari ya maua na chavua nyingi.
Madume yanazungukia makundi mbalimbali, kwa hiyo hata madume kutoka makundi
jirani yanaweza kuingia ndani ya mzinga usio wao. Nyuki kinda wa madume
wanaweza kuvunwa kwa kutumia kifaa maalum cha kufunulia vidau vya masega,
ambacho huvuna nyuki kinda wote wa masega kwa mkupuo mmoja. Wafugaji asili wa
nyuki mara nyingi huvuna nyuki kinda pamoja na asali. Asali iliyofungiwa katika
vidau hukamuliwa yote nje. Asali inayobaki ndani ya vidau vya masega ndiyo
hutumika kutengeneza pombe ya asali na mvinyo wa kienyeji. Nyuki kinda ambao
hawajasindikwa huweza kuhifadhiwa kwa siku moja tu. Wanaweza kuongezwa ndani ya
asali, lakini uwiano wa asali na nyuki kinda usizidi asilimia 5 kwa viluwiluwi
na asilimia 10 kwa funza wa nyuki. Viluwiluwi kutokana na jeli ya kifalme
huweza kusindikwa, kukaushwa kisha kusagwa kuwa unga unga.
9 Nta
Nyuki huhitaji
nta ili kujenga viota vya vidau katika masega. Kazi hii hufanywa kwa msaada na
nguvu ya lishe itokanayo na asali.
9.1 Uzalishaji
utokanao na nyuki
Nyuki hutoa
jasho linalounda nta kupitia jozi nne za vifuko vilivyo upande wa chini wa
tumbo la nyuki. Ukuaji wa vifuko hivi hutegemea uwingi wa chavua inayoliwa na
nyuki huyo baada ya kuanguliwa. Nyuki akila chavua ya kutosha wakati wa
kuanguliwa, basi watajihakikishia uwezo mkubwa wa kuwa na vifuko vya
kutengeneza nta. Nyuki wenye umri wa siku kumi hivi ndio hutoa nta nyingi zaidi
kutoka vifuko vyao. Wakati wanapotoa nta na kuitumia kujenga vidau vya masega, nyuki
hula na kuchuja lishe itokayo katika asali. Kiwango chao cha lishe husababisha
joto la juu ndani ya miili yao na joto la hewa ambalo hufanya nta iyeyuke na
kuwa tepetepe. Nta hutiririka kama vile uteute kutoka ndani ya vitundu vya
vifuko vya nta tumboni mwa nyuki ndipo huganda baada ya kupozwa na hewa. Nta
sasa huwa nyepesi, nyeupe, yenye gamba umbo la yai. Nyuki kisha hapa hukamata
magamba haya kwa kutumia miguu yao ya mbele na kuyatafuna hadi yawe umbo lifaalo
kujenga chumba cha masega. Iwapo kundi la nyuki litakaa katika eneo moja kwa muda,
basi nyuki wataanza kuunda magamba ya aina hii na kujenga vyumba vya masega.
Utakuta vipande vidogo vidogo vya
magamba ya nta chini ya kundi la nyuki lilipokaa kwa muda.Kundi la nyuki, yaani
ambalo bado lipo safarini tu, halijatua, hujenga masega katika kituo kipya.
Nyuki wanapotoa jasho, wanatumia nguvu nyingi za misuli yao. Nguvu hii na
malighafi za kuunda magamba hutokana na asali ambayo nyuki amehifadhi tumboni,
pia asali iliyo ndani ya chumba cha masega pale nyuki wanapokuwa na maskani au mzinga.
9.2 Sifa na muundo
Habari
iliyoelezwa hapa chini inahusu zaidi aina ya nyuki wa Apis mellifera.
Aina nyinginezo za Apis, hutoa nta ambayo ina muundo tofauti
kidogo. Nyuki wasiouma hutoa nta kidogo tu katika jasho wanalotoa,
lakini hukusanya porini gundi za kiasili na kuzichanganya na nta kidogo. Hali
hii hutengeneza nta iliyo imara na ngumu. Nta ya nyuki ni zao la asili ambalo
linaundwa kutokana na malighafi zisizoweza kuyeyuka. Hii ndiyo hufanya nta
isiwe na kizingiti cha kuyeyuka, bali iweze kuyeyuka pole pole. Nta inayeyuka
pole pole kuanzia nyuzi joto 62 hadi 65 celsius, na hata hivyo joto zaidi linahitajika
kuyeyusha nta. Hali hii ina manufaa kadhaa. Inawezesha nta kufinyangwa kwani
kuanzia nyuzi joto 35 celsius nta inakuwa tepetepe. Nta ya nyuki inaweza
kutolewa katika masega hata kwa joto la jua, mvuke au maji ya moto. Nta ya
nyuki siyo hai. Kwa hiyo nta inaweza kutumika kulinda vitu vingine visidhurike
kwa kemikali na hata asali yenyewe, iwapo nta inafunika vitu hivyo. Nta ya
nyuki inafaa vile vile kwa matumizi ambayo kemikali
muhimu inatakiwa kutolewa kidogo kidogo. Pia, nta haiyeyuki katika maji, sifa
hii inafanya nta kuwa bora katika kufanya vitu visiweze kulowa maji na vitambaa
visipitishe maji. Nta ya nyuki huyeyuka
katika nishati mafuta kama vile benzini, spiriti na mafuta yanayoweza kuwa
mvuke kiasili kama vile ether chloroform. Nta inaweza pia kuyeyushwa kwa
kuchemshwa katika mafuta laini au katika mafuta mazito.Rangi ya nta inatokana
na chavua ambazo zimekusanywa na nyuki wakati wa kuunda nta hiyo. Nta mpya, kwa
kawaida ni nyeupe, lakini huweza kuwa manjano hadi wekundu wenye njano. Kwa
kadri yanavyoendelea kutumika, masega hupata weusi hata kahawia nyeusi baada ya
kuwa na nyuki kinda. Nta hupoteza rangi yake na kupauka ikikaa juani. Nta iliyo
baridi inavunjika kwa urahisi. Uzito wa nta wa kimaada ni kilo 0.95 katika lita
moja hivyo nta ni nyepesi na inaweza kuelea juu ya maji. Lakini nta inapopata
baridi huongeza uzito wa kimaada, lakini
inasinyaa. Sifa hii ya nta inafaa kwa kuunda sura za zana, kwa sababu baada ya
nta kupoa kufuatia kuchemshwa, inaposinyaa inajibandua kutoka kwenye sura ya
zana inayoundwa.
9.3 Matumizi
Nta ya nyuki ina
matumizi mbalimbali.
Nta katika ufugaji nyuki na utoaji
asali
Matumizi ya
muhimu zaidi ya nta ni katika ufugaji nyuki, hususan kwa kutengenezea masega ya
bandia. Msingi wa masega bandia hutengenezwa kwa nta vipande bapa iliyobumbwa
au kugandamizwa ili kufanya vidau ambavyo nyuki huingia na kufanya masega
halisi kwa haraka zaidi na bila gharama kwao maana asali haihitajiki. Nta ya ziada,
inaweza kupatikana zaidi katika nchi ambako masega ya bandia hayatumiki. Nta
mpya ni safi zaidi kuliko iliyo ya zamani iliyoyeyushwa. Nta, iwe itokanayo na
masega mapya au ya zamani, ni lishe lakini haiyeyushwi tumboni mwa wanyama. Iwapo
utakula masega ya asali, utameza pia kiasi kidogo cha nta, pungufu ya asilimia
2 hadi 3 ya uzito wa asali uliyokula, kwa hiyo asali ya masega hutengenezwa
katika masega mapya tu. Asali kutoka masega ya zamani au iliyotengenezwa kwa msingi
wa masega bandia, ina ladha dhaifu. Katika nchi ambako ufugaji nyuki ni wa
asili, watu mara nyingi hula asali ya aina yoyote ya masega. Hii asali huwa na
ladha yenye utando.
Matumizi ya asili na ya viwandani
Waundaji wa zana
za muziki hutumia nta kwa sababu ina uwezo wa kubumba, kuteleza, na kutia rangi
katika mbao na ngozi. Inatumika pia katika kutengeneza kalamu za nta za rangi
na rangi za kupaka. Nta inatumika katika useremala, kubumba sura za zana za
chuma cha pua, mitambo ya uchapishaji, kutengeneza karatasi za ukaa, kufanya vitambaa
visivyopitisha maji na pia katika viwanda vya mitambo ya ufundi na umeme. Ni
malighafi muhimu katika bidhaa za kung’arisha mbao na sakafu,
hata katika girisi na dawa za kung’arisha chuma ikichanganywa na unga wa madini
ya kasiamu (calcium), pia hutumika katika stadi za uchoraji katika vitambaa na
nguo. Nta imetumika kwa karne nyingi katika uchoraji, uchoraji katika vitambaa pia
katika kubumba zana za chuma chekundu (bronze) kwa ajili ya vinyago kwa
kutumia ufundi wa kuyeyusha nta iliyobumbwa sura ya kinyago
kinachokusudiwa (lost wax ) au “cire perdue” katika lugha ya kifaransa.Mishumaa mirefu
na myembamba huundwa kwa kuchovya utambi katika nta kwa kurudiarudia. Barani
Ulaya, watengenezaji wa mishumaa hutumia nta safi kabisa kutengeneza mishumaa
kwa matumizi ya
makanisa hadi katikati ya karne ya 19. Hii bado inaendelea nchini Ethiopia na
penginepo, ingawa mishumaa ya mafuta ya taa ambayo inawekwa rangi ya njano
imeanza kuenea zaidi. Nta ilichukuliwa kama ishara ya ubikira kwa sababu ya uhusiano
na nyuki wafanyakazi katika mzinga wa nyuki waliotengeneza nta.Katika viwanda
vya vyakula, nta hutumika kwa kun’garisha na kwa kudhibiti mgando katika pipi
na peremende, kwa mfano za aina ya tofi (chewing gum) na “liquorice”.
Peremende za “liquorice” huchovywa katika nta nyembamba kusudi
zisishikamane. Nta inatumika kwa kuzuia hewa isipenye, hii huhifadhi jemu na
matunda, na kufunika asali ambayo imechujwa kutoka kwenye masega baada ya
kupashwa joto halafu kuiweka katika chupa.
Nta inatumika katika shughuli za michezo kwa mfano katika kulenga mishale kwa upinde, na katika usitawishaji matunda, kwa mfano kwa kubebesha matawi ya miti ya matunda.
Matumizi kwa vipodozi
Viwanda vya
vipodozi hutumia nta kama nyenzo ya kugandisha na kuunganisha mafuta mazito na
mafuta laini kwa sababu nta inahitaji nishati kali kuiyeyusha na muda mrefu
unaohitajika kabla ya kuyeyuka. Hali hii hufanya vipodozi hivi vibaki vigumu
katika ubaridi, na kuzuia visiyeyuke upesi zaidi katika joto la jua kama mafuta
mazito tu yawezavyo kuyeyuka. Vile vile vipodozi hivi hukaa
salama kwenye
mwili wa binadamu. Kwa hiyo nta huchanganywa katika mafuta ya malai (creams) na
pia katika marhamu na yale mafuta ya kujipodoa (lotions). Rangi ya midomoni na
wanja, ambavyo kwa kawaida huchanganywa nta zaidi ya asilimia 30, hizo ni
bidhaa kuu zinazohitaji nta ili kutengenezwa. Vile vile nta hutumika kuondoa nywele
kwa kumwagwa juu ya ngozi pale nta bado iko maji maji, kisha hubanduliwa
inapoganda.
9.4 Matumizi kwa tiba
Nta haina
protini zozote, mafuta yawezayo kuyeyushwa tumboni, wala wanga, na hivyo siyo
lishe hasa. Lakini nta inaweza kuwa kiambato katika vyakula. Unapokula nta, kwa
mfano imeambata kwenye masega ya
asali au peremende, haitayeyushwa tumboni bali hujazia tu chakula hicho. Kwa
hiyo husaidia chakula kupitishwa katika mzunguko wa utumbo, lakini nta yenyewe
itatolewa yote nje mwishowe, bila
kuyeyushwa. Ugumu wa nta pia muda wake wa kuyeyuka ulivyo mrefu, huifanya kuwa ya muhimu
katika kuunda vidonge viwekwavyo katika mkundu au uke. Nta mara nyingi inaweza
kugandisha pia kutelezesha. Katika vidonge viwekwavyo katika mkundu au uke, nta
hufanya kazi ya kuachilia pole pole madawa yaliyomo katika vidonge. Matumizi mengine
ya nta ni katika kupaka nje ya vidonge na pia kuunda zana za madaktari wa meno.
Kwa hali hii nta ni kwa ajili ya kushikanisha au kutunzia madawa mengine wala
yenyewe siyo dawa. Katika maduka ya dawa na katika maandishi ya kitabibu, nta
huitwa “cera flava” – nta safi rangi ya njano au “cera alba” –
nta nyeupe iliyopaushwa.Nta hutumika kutibu maradhi ya baridi yabisi ambayo
huhitaji kusambaa na kuhifadhi joto katika viungo vilivyo athiriwa. Kwa ajili ya
tiba za kuchezesha viungo, na kwa kukanda au kuchua misuli, nta hutumika kwa
kugandamiza misuli na viungo vya mifupa mwilini. Pia nta ina uwezo wa
kusawazisha au kutuliza maumivu, kwa mfano, katika maumivu kufuatia kupasuka
kwa kisigino cha mguu.Mishumaa isiyo na utambi hutengenezwa kwa nta tu, na
hutumika kwa tiba za jadi. Zinasemekana huchangamsha damu na ute ute uitwao
“lymph” ambavyo huzunguka katika mishipa katika masikio, koo, pua na matundu ya
fuvu la kichwa hivyo kupunguza msukumo katika sehemu hizo. Mishumaa hiyo
hufikiriwa kuwa huchangamsha mawasiliano baina ya sehemu mbalimbali za ubongo.
Mishumaa hutumika vile vile katika ibada na mafungo ya kidini. Kwa muda mrefu katika
historia, nta imechanganywa na asali na gundi nyeusi kuhifadhi miili ya wafu.
9.5 Kuyeyusha nta
Nta hutolewa
katika vyanzo mbalimbali. Masega ya asali kutoka makundi ya nyuki wasiofugwa
hutoa nta nyingi zaidi, takriban kilo moja kwa kila kundi kubwa. Baada ya
kutumika, masega yaliyokomaa huweza kutoa nta. Vipande vidogo vya masega huweza
kuokotwa na kuhifadhiwa mpaka unapotimiza kiasi cha kutosha kuyeyusha : hivi vinaweza
kuwa vipande kutoka kwenye mizinga, fremu na vifuniko vya masega vinavyobanduka
kabla asali haijakamuliwa kutoka kwenye masega. Nta kutoka kwenye vifuniko vya
nta huweza kutolewa kwa urahisi na huwa ni ya kiwango cha juu.Ili kupata nta
bora kabisa kutoka kwenye masega, budi utenganishe nta kutoka kwenye takataka
nyingine. Hii inaweza kufanyika kwanza kabisa kwa kuyeyusha nta kutoka kwenye
masega kwa kutumia nishati ya jua, maji ya moto au mvuke. Baada ya hapo nta
husafishwa.Tutajadili hapo chini baadhi tu ya mbinu zinazotumika katika
shughuli hii. Kwa njia ya kutumia maji ya moto, makapi baada ya kuyeyusha nta
bado yana kiasi cha asilimia 30 ya nta. Kwa sababu hii ni ufanisi kuyeyusha na
kukamua makapi haya mara ya pili.
Jua
Nta inaweza
kuyeyushwa kwa nishati ya jua kupitia sanduku la mstatili ambalo limeinuka
zaidi upande mmoja na lililofunikwa kwa kipande cha kioo (bora zaidi vipande
viwili) au karatasi ya plastiki inayopitisha mwanga. Kipande cha bati hufungwa
ndani ya sanduku.Mionzi ya jua
hupenyeza ndani ya kioo na kupasha joto kipande cha bati. Kipande hiki cha bati
hubadili mionzi ya jua kuwa joto, ambalo huongeza joto ndani ya sanduku. Nta
ambayo huwekwa kwenye chanja ndani ya sanduku huanza kuyeyuka na kutiririka na
kuingia katika sinia maalum la kupokelea nta. Mtambo huu wa kuyeyusha nta unafaa
sana kwa kuyeyusha nta itokanayo na vifuniko vya masega, na masega yaliyo tupu.Ni muhimu kwamba
mionzi ya jua iangaze moja kwa moja kwenye sanduku ili kuzuia kioo kisiakisi
mionzi hiyo. Weka sanduku kwa mkingamo ambao unawiana na jua. Kipande cha kioo
kinaweza kufungwa kimoja
au vipande viwili pamoja, au karatasi la plastiki lenye kupitisha mwanga
hutumika pia. Kipande cha kupokea joto kinaweza kuwa mawe meusi ya vigae au
bati laini (zinc) lililopakwa rangi nyeusi.
Sinia la kupokea nta hutengenezwa kwa bati jembamba ili iwe rahisi kuondoa nta
iliyoganda.
Maji ya moto
Katika kutumia
maji ya moto kuyeyusha nta, vipande vya masega na vifuniko vya nta hufungwa
ndani ya mfuko au gunia. Mfuko unazamishwa ndani ya sufuria lililojaa maji na
kugandamizwa kwa kitu kizito.
Maji yaanze kuchemshwa (tazama mchoro Na. 23). Pindi joto linapo ongezeka
kuzidi nyuzi joto 65 celcius, nta huanza kuyeyuka, hujichuja kupitia nyuzi za
mifuko /gunia na kuelea juu ya maji. Pale nta haielei tena juu ya maji unaweza
kugandamiza mfuko ili kutoa nta iliyosalia. Njia hii inaweza kurudiwa mara moja
au mbili ili kuondoa nta yote iliyosalia, ambayo yaweza kuwa theluthi moja ya nta
iliyopatikana mwanzo. Mtambo wa kuyeyusha nta kwa kutumia maji hufaa kwa masega
matupu. Vifuniko vya nta vinaweza kuyeyushwa moja kwa moja ndani ya maji ya
moto bila kufungwa ndani ya mfuko au kugandamizwa. Asali yoyote itakayonata
kwenye vifuniko hubaki juu
ya maji, na hii inaweza
kutumika kwa kuunda lishe za mifugo.Nta huganda ndani ya maji, na inaweza
kuondolewa ikiwa mabonge ya kuyeyushwa zaidi. Ni muhimu kwamba maji
yasiruhusiwe kuchemka sana. Mfuko/gunia halitaweza kukaa chini kabisa kwenye sufuria
lililo kwenye mafiga kwa kuwa kiwango cha joto ni cha juu mno mahali hapo. Kwa
hiyo mfuko/gunia viwekwe juu ya chaga la mbao ndogo ndani ya sufuria.
Mvuke
Mchoro Na 24
unaonyesha mtambo wa mvuke wa kuyeyusha nta. Mtambo huu hufanya mvuke kutokea
kwenye gudulia lililo peke yake. Mvuke unaongozwa kwa kutumia mrija wenye
kilango kidogo hadi kwenye wavu au mfuko uliounganishwa na chumba cha
kuyeyushia nta. Kwa hiyo nta hutiririka chini ndani ya gudulia na kutokeza nje
kupitia kilango kingine.Mtambo huu unaweza kuyeyusha kiasi
kikubwa cha masega kwa ufanisi na unafaa kwa aina zozote za vyanzo vya nta.Lakini ni vigumu
kujitengenezea mwenyewe mtambo kama huu, kama ilivyo kwa mtambo wa nishati ya
jua na kwa kutumia maji ya moto.
Aina nyingine ya
mtambo wa kuyeyusha nta unaotumia mvuke unachemshwa kwa kutokea chini, k.m.
kutumia moto. Mvuke unapanda juu kutoka kwenye maji ya moto yaliyo sehemu ya
chini iliyo na chombo
kilichojaa masega au vifuniko vya nta. Nta iliyo katika sehemu ya juu inayeyuka
kutoka kwenye masega na kutiririka hadi ndani ya sinia la kupokea nta ambalo
linaweza kuondolewa peke yake. Vipande vya nta vinaweza kukwanguliwa kutoka
kwenye sinia baada ya kuganda. Mitambo ya kuyeyusha nta iliyo na kuta mbili
huchemsha nta katika chumba cha katikati kilichozungukwa na mvuke.
9.6 Kusindika na
kuuza
Baada ya nta
kuyeyuka, bado ina uchafu hasa upande wa chini wa nta. Uchafu huu unaweza
kukwanguliwa kwa urahisi. Halafu nta husafishwa tena ndani ya maji ya moto au
mvuke, kisha humwagwa ndani ya umbo moja au maumbo kadhaa yanayotakiwa. Haya maumbo
huweza kutengenezwa kwa bati au hata plastiki, kwa vile nta haina joto
linalozidi nyuzi joto 70 hadi 80 celsius. Ni vizuri zaidi kuruhusu maumbo hayo,
yakiwa na joto yapoe pole pole katika eneo
lisilo na upepo.
Acha yapoe angalau kwa siku moja. Nta kwa wakati huu itakuwa kwa kawaida haina
uchafu. Sehemu ya chini ya bonge la nta inaweza kukwanguliwa tena hadi kufikia
nta safi.
Kwa matumizi
kadhaa, nta inalazimu kupaushwa, stadi ambayo inaweza kufanywa kwa njia za
asili, au kwa kutumia kemikali za madawa kwa wafugaji nyuki, njia za asili
inafaa zaidi, hususan
kuanika juani.
Isage sage nta iwe vipande vidogo vidogo na uitandaze kwenye mkeka, au
tengeneza pande jembamba la nta lililotapakaa kwa kutumbukiza ubao uliolowa
maji katika nta iliyochemka, halafu kukwangua nta mara inapoganda. Iwapo kiasi
kikubwa cha nta kinaweza kukusanywa na kusindikwa, huwa zao la kupendeza kwa
wafugaji nyuki kwa ajili ya biashara na hata kwa kuuza nje ya nchi. Nta
inayotengenezwa kwa kuuzwa nje ya nchi budi isafishwe vizuri sana iwezekanavyo.
Baada ya hatua za kusafisha nta, nta inaweza kuundwa katika mapande ya kufaa
yenye uzito wa kilo 20 hadi 25. Kwa kutimiza mzigo unaofaa kusafirishwa nje ya
nchi, mavuno ya nta kutoka kwa wakulima wengi yanaweza kuunganishwa. Hii
inaweza kufanyika, kwa mfano, kupitia shirika la wafugaji nyuki
au kikundi kidogo cha wafugaji nyuki. Usichanganye nta na mbadala wowote wa
nta, kwa mfano makapi ya mafuta ya taa au mafuta ya aina nyingine. Hii
itapunguza thamani ya nta, na imani ya
mnunuzi katika mavuno yenu.
10 Gundi nyeusi
Gundi nyeusi
hutengenezwa kutokana na utomvu wa miti, gundi asili, nta na ute ute unaonata.
Vitu hivi hupatikana pembeni ya maua yanayoanza kukua, pia hutolewa nje ya gome
la mti unapokatwa au kupasuka. Nyuki huleta vitu hivi kwa kutumia miguu yao ya
nyuma, kama ilivyo kwa chavua, na kuviingiza ndani ya mzinga. Nyuki huvichanganya
vitu hivi pamoja na mate na nta. Hii huunda nta nyeusi.
Sifa na Muundo
Gundi nyeusi ina
muundo wake halisi, inanata, ni kahawia, na ina harufu nzuri. Nyuki hutumia
gundi nyeusi kuziba matundu na nyufa yasiyotakiwa katika kuta za mzinga, kisha
husafisha vichumba vya nyuki kinda wa
baadaye kwa uangalifu sana. Vile vile nyuki hutumia gundi nyeusi kurekebisha
upito wa kuingilia ndani ya mzinga.Wakati wa baridi kali vipito hufanywa finyu
zaidi. Pia nyuki hutumia gundi nyeusi ndani ya mzinga kushikanisha sehemu
zozote za mzinga zilizoachana. Hii ni faida pindi mzinga unapopaswa
kuhamishwa.Nyuki hutumia gundi nyeusi kuzuia kuoza kwa wanyama waliofia ndani ya mzinga,
kwa mfano panya. Nyuki pia huchanganya kiasi kidogo cha gundi nyeusi katika nta
itumikayo kuziba vichumba vya nyuki kinda.Aina zote za nyuki hutoa gundi
nyeusi, lakini hiihutumika kwa kazi tofauti katika aina ya nyuki wa huko bara
la Asia, na nyuki wasiouma.
Kundi lolote
linaweza kukusanya viunganisho vingi zaidi vya kuunda gundi kuliko makundi
mengine na majira mbalimbali yanaweza pia kuwa sababu. Mfugaji nyuki anaweza
kutegemea mavuno ya gramu 50 hadi 100 za gundi nyeusi kutoka kundi moja kwa
mwaka. Maada zinazounda gundi nyeusi ni pamoja na zinazotia ladha, tindikali za
ferulic (ferulic acid), gundi gundi, mafuta ya kunukia/harufu nzuri, pia
maada yenye lishe ya aina ya karoti (carotenoids).Maada nyingine zilizomo
katika gundi nyeusi ni nta za miti na zile zitokanazo na nyuki (kama asilimia
30) na maada ghafi mbalimbali.Utomvu, uteute na gundi zitokanazo na miti
zinazokusanywa na nyuki hutokana na miti mchanganyiko, ambazo kila mmoja una
aina yake ya ladha. Kwa hiyo gundi nyeusi hutofautiana kufuatana na uoto na mazingira
ya kijiografia ilipokusanywa. Ladha ya maada zilizounda gundi nyeusi inafanana
lakini ina muundo tofauti tofauti kikemia.Kwa hiyo hutumika kutambua maeneo ya
kijiografia na kiuoto ilipotoka asali. Gundi nyeusi katika nchi za baridi
kidogo ina maada asili kiwango cha asilimia 50. Katika nchi za joto, gundi
nyeusi ni kavu zaidi, ngumu, hainati sana na ina harufu ya wastani, na madawa
asili kiwango chini ya asilimia 10. Hali hii inahusu gundi nyeusi itolewayo na
nyuki aina ya Apis mellifera. Gundi nyeusi itolewayo na nyuki wasiouma inachanganywa
na nta zaidi, kwa hiyo huitwa “cerumen” kwa Kilatini. Gundi nyeusi
haiyeyuki katika maji, na haipitishi hewa. Ni kavu katika joto la kiwango
kidogo na huwa tepetepe katika joto zaidi ya nyuzi
joto 35 celsius. Rangi ya gundi nyeusi huweza kuanzia ya kahawia nyeusi hadi nyekundu au njano.
Manufaa kwa afya
Muundo
Gundi nyeusi
haina protini, wanga wala mafuta, kwa hiyo haina thamani ya kuleta joto
mwilini. Kwa vile gundi nyeusi ni mchanganyiko wa maada nyingi, manufaa yake ni
mapana. Kutokana na manufaa kwa tiba, gundi nyeusi hutumika kama kuongezea
ubora wa dawa za lishe maalum.Iwapo kimelea cha bakteria, kuvu, kirusi au
hamira kinanaswa ndani ya gundi nyeusi, hakiwezi tena kupata hewa wala maji. Kimelea
hunyauka na kufa. Hili ni tukio la kuua vijimelea, na ndiyo sababu gundi nyeusi
mara nyingi huitwa dawa asili ya kiua vijimelea. Nyama ya mwili wa binadamu na
mifupa huweza vile vile kuimarishwa kwa gundi nyeusi. Gundi nyeusi hupenya
nyama ya mwili, na kwa hiyo huongeza kasi ya kuponesha mifupa iliyovunjika, na
maradhi ya misuli, kwa mfano ugonjwa wa kuvimba misuli ya viungo (bursitis
kwa kiingereza). Inapoza ngozi ya mwili na ina hali ya kuponesha.Gundi nyeusi
inapomezwa, husafisha damu, yaani inakusanya chembechembe huru zenye madhara.
Vile vile nta nyeusi hutuliza maumivu kama inapakwa juu ya mwili.Baadhi ya
wafugaji nyuki hupata mzio (allergy) kutokana na gundi nyeusi, wanaweza
kupata vipele ambapo ngozi ya mwili huwa nyekundu na yenye magamba. Iwapo hali
hii itajitokeza, basi wasiiguse gundi nyeusi bali wavae mipira ya kufunika
viganja vya mkono (gloves).
Matumizi
Gundi nyeusi
inatumika kuponyesha vidonda, inatumika kama dawa ya asili yenye kuua vimelea kama
inamezwa pamoja na dawa za kikemia za kuua vimelea (antibiotics), na
njia ya kuimarisha afya yako na mfumo wa kinga dhidi ya maradhi.Kwa ajili ya
kupaka nje ya mwili, gundi hutengenezwa kuwa dawa za mafua, dawa za kikohozi,
dawa ya meno, mafuta laini ya ngozi, dawa ya kupunguza
maumivu (salve), mafuta mazito (cream), mafuta ya kupaka mwilini,
mafuta ya nywele na sabuni. Bidhaa za kutunza afya zenye kuwa na nta nyeusi
ndani yake hutumika kwa kuponya vidonda, makovu, maambukizo, maumivu ya misuli,
upele (eczema) mabaka (psoriasis), uvimbe, kuvu na kuvu zinazoota
kwenye makucha. Kwa matumizi katika dawa za kumezwa, unga wa gundi nyeusi mara nyingi
huchanganywa na asali. Ili kutengeneza vidonge na vidonge vya kujaza unga wa
dawa (capsules) gundi nyeusi kwanza inasafishwa kitaalamu kwa sababu nta
zitokanazo na miti, na nta halisi ya nyuki iliyomo humo kwa kawaida, hufanya
iwe vigumu gundi hiyo kunyonywa ndani ya mfumo wa mmeng’enyo wa chakula
mwilini.Kwa ajili ya matibabu ya maradhi yenye dalili zinazotatanisha gundi nyeusi
ghafi huchujwa kwa kutumia spiriti (tazama sura ya 11) ili kutengeneza kile
wanachokiita “dawa mama”. Hii hutengenezwa kwa kuunda viongezeo vya lishe, na
bidhaa za kutunza afya, pia gundi nyeusi huongezwa spiriti zaidi na kutumika
kama dawa ya majimaji.Dawa kama hii haiyeyuki katika maji kwa hiyo njia bora
zaidi ya kuitumia ni kuiyeyusha juu ya kipande cha mkate, au kwenye sukari iliyogandishwa,
au kidonge cha sukari. Matone ya dawa hii iliyo na asilimia 10
kikemikali inaweza kuongezwa ndani ya bilauri moja ya maji. Peremende za mpira za
kutafuna, vidonge vya kufunguliwa, vidonge vya kawaida, dawa ya kikohozi ya
maji, na dawa ya kusafisha kinywa hupatikana kutokana na gundi nyeusi.
Matumizi mengineyo
Katika ufugaji nyuki
Wafugaji nyuki
hutumia gundi nyeusi, mara nyingine ikichanganywa na nta, kufanya mizinga iwe
ya kuvutia kwa makundi ya nyuki. Nyuki hutambua harufu ya gundi nyeusi hata
nyuki wakiwa mbali sana.Rangi ya mbao itokanayo na gundi nyeusi huweza
kutengenezwa kwa kuchanganya na kemikali ya “ammonia” au hata spiriti na
tindi kama hizo.
Matumizi ya kiasili
Gundi nyeusi ina
matumizi mbalimbali kiasili. Inaweza kutumika kama kiongezeo katika tope la kufungia
mguu uliovunjika, na kama gundi (iliyo na nta au isiyo na nta ndani yake), kwa
mfano kwa ajili ya kurekebisha vyungu vilivyopasuka. Wakati fulani gundi nyeusi
ilitumika katika utengenezaji rangi, lakini njia hii haitumiki tena na utaalamu
huo umeishapotea.Gundi nyeusi huongeza ubora wa mbao, na kwa hiyo hutumika
zaidi kwa kung’arisha ala za muziki zilizoundwa kwa mbao. Siyo huzuia kuvu na
kuoza, bali pia ikichanganywa na nta inalainisha au inaongeza ubora wa mbao na
ngozi kavu, kwa mfano ile inayotokea katika ngozi ya kwenye ngoma. Wana muziki
wa Kiafrika wanapopiga ngoma kwanza hugusisha vidole vyao vya mikono kwenye
gundi nyeusi iliyochanganywa na nta kisha kupiga ngozi ya ngoma ili kufanya
mlio bora wa ngoma.
Uvunaji na usindikaji.
Njia mbalimbali
zimeundwa kukusanya gundi nyeusi. Njia moja ya kukusanya gundi nyeusi ni kwa
kutumia wavu au kifaa cha mviringo kilichoundwa kutokana na plastiki ngumu na
kuwekewa matundu au mianya ya upana wa mm 2 hadi 3. Chombo hiki hutundikwa juu
ya mzinga kwenye fremu au kama fremu iliyonig’inizwa katikati ya fremu
nyingine. Kwa kutumia gundi nyeusi, nyuki hujitahidi kuziba matundu hayo kwa
haraka iwezekanavyo ili kuzuia upepo usiingie ndani. Hili ni muhimu kwa kutunza
kiwango cha joto kinachotakiwa ndani ya sehemu ya nyuki kinda.Baada ya kuvuna,
mtego huo wa gundi nyeusi huwekwa sehemu iliyo na ubaridi, au unahifadhiwa
ndani ya jokofu (friji) au hata ndani ya maji ya baridi. Baada ya kila kitu
kupoa, ndipo mfugaji nyuki huvunja na kuondoa
vipande vya gundi nyeusi na anaweza kutumia mtego huo huo tena.Njia rahisi
zaidi ni kukwangua gundi nyeusi kutoka kwenye fremu zilizoisha tumika katika
mzinga. Gundi nyeusi hupatikana zaidi kwenye vipande vya mazao vilivyo juu au
chini pembeni mwa mzinga wa kisasa. Katika mizinga ya kisasa ya nyuki, gundi
nyeusi hukwanguliwa kutoka pembeni mwa vipande vinavyo elekea juu.Katika nchi
za joto, inawezekana pia kutundika ndani ya mzinga vibuyu au vijungu vyenye
matundu makubwa ya kuingilia. Nyuki huziba tundu lote kwa gundi nyeusi.
Kusindika
Gundi nyeusi ni
lazima isafishwe. Chembe chembe za nta, vipande vya rangi, misumari, na
takataka nyinginezo lazima viondolewe. Gundi nyeusi safi iliyokolea, katika
nchi zenye joto la wastani, lazima ikolee kwa kiwango cha asilimia 50. Gundi
nyeusi inaweza kusagwa, kwa mfano kwa kutumia mtambo mdogo wa jikoni wa kusaga kahawa.
Gundi hii itabidi iwe baridi sana iwezekanavyo kwa mfano inayotolewa moja kwa
moja kutoka kwenye jokofu /friji, kwa sababu hapo itakuwa ngumu na isiyonata.
Matokeo mazuri hupatikana kwa kusaga kwanza gundi nyeusi iliyoganda kwa baridi
kali, ukitumia kisagio cha kuzungusha kwa mkono, hadi iwe vipande ghafi vilivyovunjwa
vunjwa, ndipo isagwe tena kuwa laini zaidi.Gundi nyeusi iliyokusanywa inaweza
kuhifadhiwa katika ndoo za plastiki, lakini siyo katika makopo. Jinsi gundi
nyeusi inavyochemka, itavuja nje, na
hatimaye kugeuka kuwa ngumu. Hapo itakuwa vigumu sana kuitoa kutoka kwenye
kopo. Kuongeza unga unga wowote, kutazuia gundi nyeusi kuganda. Kwa ajili hii,
unaweza kutumia chavua, sukari,
unga wa mhogo au unga wowote tu, sukari za asilimiti au za kemikali tamu kwa
mfano “magnesium stearate” na “dextrin – maltose”.
11 Nyuki
Chimbuko na maumbile
Kwa sura ya nje,
nyuki wana gamba lisilo hai badala ya ngozi, miguu na mabawa (tazama mchoro Na.
25). Maumbile ya ndani ni minofu na viungo mbalimbali, kama vile tezi na viungo
vya kazi maalum mwilini vinavyotoa kemikali ziitwazo “hormone” kwa
kiingereza.Damu ya nyuki ina kiasi kingi cha protini rahisi. Hizi hupatikana
pia katika ute unaotoka katika tezi za nyuki.
Manufaa kiafya na uzalishaji wake
Manufaa ya nyuki
kiafya yanatambuliwa hasa kwa tiba za kiasili na kwa tiba zinazotibu dalili za
maradhi ujuzi uitwao “homeopathy” kwa kiingereza. Ute utokao katika tezi
una madawa yanayoua vimelea, pia una vimeng’enya. Tezi muhimu ni tezi ya sumu,
ambayo hujaa sumu ya nyuki. Mfumo wa uyeyushaji
chakula katika nyuki una chembechembe za asali na chavua. Vitu hivi vyote
huchangia kufanya mazao ya nyuki yawe na thamani kitabibu.Nyuki au viungo vyake
huyeyushwa kwa spiriti katika madawa ya kiasili ili kuundwa dawa anzilishi.
Dawa zaidi huundwa kwa kuongeza maji kidogo katika dawa anzilishi hiyo, kwa
uwiano wa 1:9 sehemu moja ya dawa anzilishi huongezwa kwenye sehemu 9 za spiriti
D1, halafu hii nayo huunda dawa nyingine kwa uwiano huo huo, na
kuendelea. Dawa iliyolegezwa nguvu kwa spiriti kama ilivyoelezwa hapo juu,
inatumika kutibu watu walio na mzio wa sumu ya nyuki, kwa kuimimina kwenye
kipande cha sukari iliyogandishwa na kumlisha mgonjwa. Dawa anzilishi
iliyoelezwa juu huuzwa katika maduka ya madawa ikiitwa jina la biashara la Apis
Mellifica. Miiba ya nyuki hukusanywa kwa kukatwa kutoka kwenye matako ya nyuki
vibarua. Miiba hii ndipo hukaushwa na kusagwa, kuchanganywa na sukari au unga
wowote kwa uwiano uliotajwa hapo juu. Dawa hii ijulikanayo kibiashara kama Apisinum
ina nguvu zaidi kuliko ile ya Apis mellifica, na bila shaka ina sumu
ya nyuki kwa wingi zaidi
12 Sumu ya nyuki
Nyuki wa kike,
yaani vibarua na malkia wana mwiba mwishoni mwa tumbo ambao wanaweza kuuchomoa
na kuufutika tena. Malkia kwa kawaida anatumia mwiba huu kutaga mayai, lakini
anaweza pia kuutumia kudunga maadui. Tone ambalo ndiyo sumu ya nyuki, huvuja kutokea
kwenye mwiba unapochomolewa. Mwiba huu pia una miiba midogo midogo
inayojitokeza kuzunguka mwiba mkuu. Sumu ya nyuki inatengenezwa ndani ya tezi
ya sumu, na inahifadhiwa ndani ya kifuko kidogo mwishoni mwa mwiba mkuu. Nyuki wachanga
wana sumu kidogo. Vifuko vyao vya sumu huwa havijazwi hadi siku ya 15 hadi 20
toka kuzaliwa ambapo huwa na sumu kiasi cha milligramu 3/10 (tatu ya kumi).
Nyuki wanaokua wakati wa majira ya maua mengi huwa na sumu nyingi na yenye
nguvu zaidi. Sumu ya nyuki huyeyuka katika maji lakini si katika mafuta.
Spiriti inadhuru sumu ya nyuki.
Muundo
Matokeo ya kuumwa nyuki
Nyuki
anapokudunga mwiba wake, anasukumiza maji ya sumu kupitia katika mwiba huo, na
kuingiza sumu mwilini mwa adui. Nyuki vibarua hawatagi mayai bali huutumia
kudunga. Kama nyuki akimdunga mwiba nyuki mwenzake, au nyigu, mjusi au nyoka, anaweza
kuuchomoa mwiba. Lakini kutokana na miiba midogo midogo inayozunguka mwiba
mkuu, mwiba hubaki mwilini mwa binadamu au
wanyama wenye damu ya joto. Mwiba huendelea kuvuja sumu kwa dakika 10 hadi 20, ambapo
1/3 ya sumu huwa
imevuja tayari kutoka kwenye kifuko cha sumu. Kiasi kikubwa cha sumu huvuja katika
dakika ya kwanza. Nyuki au mdudu mwingine anaweza kuuawa kwa kudungwa mara
moja; kuku, farasi au punda, huweza kuuawa akidungwa mara kadha, lakini
binadamu anaweza kustahimili sana hata anapodungwa mara nyingi. Hii
hutofautiana bila shaka baina ya mtu na mtu, na inategemea ni mara ngapi mtu
ameumwa na nyuki hapo zamani.Mtu ambaye amevamiwa na kundi la nyuki anaweza
kuwa na mamia ya miiba mwilini mwake. Hii miiba inaweza kuhesabiwa hospitalini
ili kujua vizuri idadi ya miiba inayoweza kufanya watu mbalimbali kupoteza
fahamu au kufa. Kwenye mwili wa binadamu, duara nyeupe ya kipenyo cha sentimita
moja (1sm) hujitokeza kuzunguka sehemu iliyodungwa, halafu sehemu kubwa zaidi
huvimba. Mara baada ya kudungwa mwiba wa kwanza, mtu atajisikia dalili mbaya
kwa mfano kuumwa kichwa, kuvimba pale palipoumwa, na mwasho. Watu wengi zaidi
hujenga ustahimilivu, lakini wengine hupata mzio baada ya kudungwa na miiba ya
nyuki hata iwe mara nyingi. Sumu ya nyuki inadhuru hata ikiwa ni kwa kiwango
cha chini sana, na baadhi ya watu wanapata mzio, hasa inapopitia ndani ya mwiba
wa nyuki mwenyewe.
Ndani ya saa moja baada ya kudungwa, mtu mwenye mzio huathirika msukumo wa damu
ambao hushuka kwa kiwango kikubwa mno kinachosababisha figo kuzorota na kusababisha
kifo kwa mtu huyo. Damu hupitapita katika mwili wa mtu, na kusababisha upungufu
wa ute ute ndani ya viungo vyote vyenye kazi maalum mwilini, hasa figo.
Kutapika na kunywa maji huweza
kurekebisha tatizo hili, kwa vile damu sasa hurudishwa katika mfumo wa
uyeyushaji chakula mwilini na kwenye viungo vingine vya mwili. Tahadhari na
njia za kujilinda ni ya muhimu sana wakati wa kujihusisha na nyuki, unapovuna
au kusindika sumu ya nyuki.
Nguvu ya sumu
Muundo wa sumu
hii hutofautiana kidogo baina ya makundi ya nyuki, pia hutofautiana kwa kiasi
kikubwa baina ya uzao husika wa hao nyuki. Muundo wa sumu ya nyuki hujumuisha
vitu mbalimbali kwa mfano kemikali ya “mellitin” asilimia 40 – 60,
kemikali ya “phospholipase “A” (asilimia 10 – 12), kemikali ya “apamine”
(asilimia 2 – 3), “MCD-peptide” (asilimia 2), “histamine”
(asilimia 1).
Uwezo wa kutibu wa sumu ya nyuki aina ya Apis cerana ni wa juu zaidi mara mbili kulinganisha na uwezo wa sumu kutokana na nyuki wa aina ya Apis mellifera. Sumu ya Apis mellifera hulingana na ya Apis dorsata kwa uwezo wa kutibu. Sumu ya nyuki wa aina ya Apis florae ina nguvu pungufu. Nyuki wasiouma hawana mwiba, wala sumu, lakini baadhi ya aina hizi huweza kung’ata na kuingiza sumu inayowasha tu ndani ya mwili wa mtu au mnyama aliyeumwa. Kemikali zinazounda sumu huyeyushwa katika uteute ulio ndani ya vifuko vya sumu. Sumu ina aina tano za kemikali kutoka kwenye damu ya nyuki, kwa mfano protini. Mtu mwenye mzio wa kudungwa miiba ya nyuki, ataathirika si kwa sumu tu bali hata damu ya nyuki.Ute ute kutoka mwiba mmoja wa nyuki una uzito wa 1/10 ya milligramu ya unga mkavu. Kwa matumizi katika uundaji dawa, kwa mchanganyo katika vyakula, na bidhaa za kulinda afya, sumu ya majimaji hukaushwa na kusafishwa sana. Katika hali hii sumu huwa na nguvu zaidi ya mara tatu kulinganisha na ilivyo katika uasili.Kiwango cha LD 50 ambacho huweza kuua, ni kiasi cha sumu ya nyuki ambacho kinaweza kuua nusu ya watu wanaoiingiza miilini – (takwimu hii hupatikana kwa utafiti kwa kutumia wanyama pori, na kuwianisha matokeo hayo na uzito wa binadamu). Kiwango cha LD 50 cha sumu ya nyuki isiyowekwa maji, ni milligram 2 8/10 kwa kila kilo ya uzito wa mwili wa binadamu. Kwa mtu mwenye uzito wa kilo 70, itatakiwa sumu kiasi cha 1/10 ya gramu, sawa na kudungwa miiba
2,000 ya nyuki. Athari ya sumu huongezeka iwapo aliyeumwa atafadhaika na kupata hofu au woga, anapoumwa na nyuki.Mfugaji nyuki ambaye ameishaumwa nyuki mara kadha huwa na
kiwango cha juu
cha kemikali iitwayo “immunoglobin E ndani ya damu mwilini mwake. Hii ni kinga
mwili iliyo ndani ya protini za damu mwilini. Ataweza kustahimili kudungwa
miiba ya nyuki kuanzia mara 40 hadi 100, ambavyo kwa mtu asiye na kinga mwili
hii atapata madhara makubwa. Mtu mwenye mzio wa miiba ya nyuki anaweza kufa
kutokana na kudungwa mwiba mmoja tu, lakini hii hali isiyo ya kawaida iitwayo “anaphylaxis”
kwa kiingereza hutokea tu pale mtu mwenye mzio anapoumwa nyuki mara ya pili.
Manufaa kwa Afya
Sifa
Kwa watu wasio
na mzio, sumu ya nyuki huongeza usambazaji damu ndani ya mwili, na kuruhusu
damu ipite kwa urahisi katika mipaka ya kila chembe chembe hai za mwili. Mshipa
inayosafirisha damu mwilini hupanuliwa, na msukumo wa damu huteremka. Sumu ya nyuki
vile vile hulegeza misuli, na huweza kupunguza maumivu ya misuli kwa kuyeyusha
kemikali ziitwazo “lactic acid” kwa kiingereza, zinapokuwa mwilini.
Kiasi kidogo cha sumu ya nyuki, huburudisha mwili, lakini kiasi kingi husababisha
kuongezeka kwa mapigo ya moyo, kukosa usingizi, sawa na matokeo ya kunywa kahawa
nyingi mno. Inaweza pia kusababisha ongezeko au upungufu wa mkojo. Kwa mujibu
wa takwimu zilizopo, wafugaji nyuki wanaepushwa kuugua maradhi kadhaa kutokana
na kudungwa miiba ya nyuki hivyo kuingiziwa mwilini sumu ya nyuki, mfululizo.
Maradhi wanayoepushwa nayo ni kwa mfano baridi yabisi, maumivu ya viungo na
saratani/kansa.Zipo kumbukumbu zinazoeleza mafanikio ya wagonjwa waliokuwa na maradhi
sugu ya kuganda viungo ambao waliweza kutembea tena baada ya kudungwa sana
miiba ya nyuki. Sumu ya nyuki inaamsha utengenezaji wa
kemikali iitwayo “cortisone” kwa kiingereza, ambayo ni dawa
itengenezwayo na tezi za figo katika sehemu iitwayo “adrenal cortex”
ndani ya figo. Hii kemikali huchangamsha mfumo wa fahamu, hasa usambazaji hisia
ndani ya fundo la neva liitwalo, “myelin”. Sumu ya nyuki inasemekana
kuweza kutibu uharibifu katika fundo la “myelin”.
Matumizi
Katika matibabu
ya kiasili barani Afrika, unga utokanao na nyuki waliosagwa, ulitumika kama
kitulizo au chai kwa kutibu maradhi pamoja na maumivu ya viungo. Watu waliweza
kujiruhusu nyuki wawadunge miiba kwenye sehemu zilizokusudiwa. Sumu ya nyuki
hutumika kwa njia mbalimbali. Inavutwa kupitia puani, inamezwa ikichanganyika
na asali, inadungwa mwilini kwa kutumia sindano,
au kufungwa juu ya mwili kama madawa yaliyolowa. Sumu ya nyuki inafika mwilini
kwa kudungwa miiba ya nyuki kwa makusudi, kama tiba peke yake au kwa
kuchanganya utaalamu wa tiba
ya nishati ya umeme (electrotherapy, kwa kiingereza), au utaalam wa tiba
ya Kichina iitwayo kwa kiingereza “acupuncture”, na “acupressure”.
Huu utaalam husababisha maumivu makali, na ni wa hatari. Nchini China na Japani
hutumika mwiba tu ulionyofolewa unaofanywa sindano ya kudunga katika sehemu zinazotibiwa
kwa “acupuncture”. Maumivu yanatokea, lakini siyo makali sana.Kiasi
kidogo cha sumu ya nyuki bila shaka kinapatikana ndani ya asali. Vile vile
kiasi kidogo kinapatikana ndani ya dawa anzilishi iitwayo Apis,
inayotumika kwa matibabu ya dalili zinazotatanisha (homeopathy) na
katika matibabu kwa dawa za asali.
Uzalishaji na utayarishaji
Sumu ya nyuki ni
sumu halisi na inaweza kuua wanyama na binadamu. Kwa ukusanyaji wake, uvunaji
na uzalishaji, tahadhali maalum zinahitajika, kama vile mipira ya kuvaa
mikononi (glovu), mpira wa
kufunika mdomo, na kadhalika. Usivute hewa au kumeza sumu ya nyuki kwa njia
yoyote bila kufuata kwa uangalifu maagizo ya daktari, na kiasi cha dawa.
Uzalishaji
Sumu ya nyuki
huvunwa kwa kutumia kikusanyio maalum. Hiki chombo kina umbo la sahani ya kioo,
ambacho waya zimewambwa juu yake na kuunganishwa na chanzo cha umeme kwa mfano
beteri moja kubwa au ndogo ndogo kadhaa. Hapo nyuki watakapogusa nyaya zenye
umeme, watamwaga kwa hasira sumu kutoka vifuko vyao vya sumu. Baada ya nyuki
wachache kumwaga sumu yao, kundi zima la nyuki litavamia sahani yote kwa maelfu
na nyuki watamwaga sumu kwenye sahani hiyo.Sumu hiyo itakauka pale juu ya
sahani na unga unga tepe tepe unakwanguliwa. Chunga mikono yako kwa kuvaa
mipira ya kuvaa mikononi kuhakikisha kuwa huwezi kugusa sumu, pia funika uso wako
ili usivute sumu hiyo kupitia mdomoni au pua. Chombo cha kukusanya sumu ya
nyuki huwekwa ndani ya mzinga wenye nyuki kwa muda wa saa moja kisha
huondolewa. Wakati wa kutumia hicho chombo, na baada ya kukitumia, nyuki walio
kwenye mzinga huo, na walio ndani ya mizinga katika eneo hilo huweza
kukasirika. Kwa hiyo ni vizuri zaidi kufanya shughuli hii katika eneo
lililojitenga.Sumu kutoka mzinga mmoja huweza kukusanywa mara chache tu kila mwaka,
vinginevyo hii itadhoofisha sana kundi hilo la nyuki. Uvunaji wa sumu unaweza
pia kupunguza uzalishaji wa asali. Kundi imara la nyuki huweza kutoa gramu moja
hivi ya sumu ya nyuki kila unapovuna.Sumu
ya nyuki ambayo haijasindikwa huweza kuongezwa katika bidhaa au huweza
kusafishwa kwanza. Kanuni kali hutumika wakati wa shughuli hii, nazo lazima
zitekelezwe. Hata hivyo wafugaji nyuki wanaweza kuleta sumu ya nyuki
isiyosindikwa kuwauzia wanunuzi walioruhusiwa na
wenye utaalamu na maabara.
Utayarishaji
Ili kuhakiki
viwango vya ukoleaji, sumu ya nyuki huongezwa hatua kwa hatua katika asali. Kwa
mfano, 1/10 ya gramu ya sumu ya nyuki huongezwa katika kilo moja ya asali,
halafu hii kilo moja na gramu 1/10 ya mchangayiko huu huongezwa katika kilo
nyingine ya asali.Huu mchanganyiko utakuwa na ukoleaji wa kiwango cha gram
1/100 kila gramu moja ya asali.Kukupa picha ya hali halisi kuhusu kiasi gani
cha sumu ya nyukihuhitajika na kuepusha hatari ya kuzidisha kiasi cha dawa
inayotosha kutibu, kiasi kinachoongezwa hutajwa kwa kulinganishwa na sumu iliyo
katika mwiba mmoja wa nyuki (mg 1/10) kwa kila kijiko kimoja cha chakula (gm
10) kilichojaa asali. Katika mafuta ya tiba, kiasi kinachoongezwa kinahusishwa
na sumu iliyo katika mwiba mmoja wa nyuki (yaani 1/10 ya milligram) kwa kila
gramu ya mafuta. Kiwango hiki cha dawa hakizidi kamwe ujazo wa 2/10 ya
miligramu kwa kila gramu ya mafuta, sawa na sumu iliyo katika miiba miwili ya
nyuki.
13 Ubora na uthibiti
13.1 Masuala ya ubora
Ubora wa asali
huandaliwa kwanza kabisa wakati inapoundwa ndani ya mzinga. Mfugaji nyuki
anachangia sana katika suala hili, pamoja na ukubwa wa mzinga, pia na muda
muafaka wa uvunaji.
Ubora wa mavuno
hauwezi kuongezwa sana kama mavuno tayari yametolewa katika mzinga, lakini
ubora huweza kupotea wakati wa uvunaji (tazama mchoro Na. 26), wakati wa
kukamua, au kusindika zaidi na kuhifadhi.Uwezo wa kuhifadhika wa asali unaweza
kuongezwa kwa kusindika, lakini hii pia hupunguza ubora
kwa njia kadhaa: asali hupoteza upya wake na thamani ya kitabibu hupungua.
Mazao ya lishe
(kwa mfano asali, chavua, mkate wa nyuki, maziwa ya nyuki, na nyuki kinda) huwa
na kemikali zenye uwezo kielimu viumbe ambao huweza kudhoofika kwa kiasi
fulani. Nta, gundi nyeusi na sumu ya nyuki, kwa kulinganisha na mazao ya lishe,
hivi hubaki vizuri zaidi na ubora wake wa awali baada ya kukamuliwa na kusindikwa
zaidi.
Mfugaji nyuki adhibiti ubora
Wafugaji nyuki
hawahitaji hasa kufanya vipimo mahsusi vya kutambua ubora wa asali yao, kwa
sababu wanafahamu iwapo asali hiyo ni mpya (mbichi) na haijachujwa, pia iwapo
ina unyevunyevu unaotakiwa.
Wanaweza kuona hali hizi, kwa mfano, kwa kuangalia kama asali ni laini mno.
Mfugaji nyuki pia ameweza kuwapo wakati wa uzalishaji, uvunaji, uchujaji na
usindikaji wowote na hivyo anafahamu
historia yote ya uzalishaji wa mavuno hayo. Njia rahisi za kupima ubora
zinafahamika kwa wafugaji nyuki. Hizi zinapendekezwa, hasa kwa wafugaji wakubwa
wa nyuki na kwa vyama vyao, kwa
sababu kwa kupima matokeo, wafugaji nyuki huweza kuongeza ubora wa mbinu za
uzalishaji. Hii itamwezesha mfugaji nyuki kuuza vizuri zaidi mavuno yake. Zana
na mbinu ambazo zinaweza
kutumika kuhakiki ubora zinaelezwa hapa chini. Tazama jedwali Na. 4 kuona
vigezo vya ubora wa asali.Hatuorodheshi vigezo thabiti, kwa sababu hivyo ni vya
kitaalamu mno visivyobidi kwa
uelewa wa wastani. Taarifa za kina zaidi zinaweza kupatikana miongoni mwa zile
zitolewazo na Umoja wa Ulaya (EC), Shirika la Chakula na Kilimo la Dunia (FAO),
au Shirika la Afya la Dunia (WHO) (tazama orodha ya tovuti katika kurasa za viambatisho).
13.2 Kanuni za
Kimataifa
Kanuni iitwayo European
Community Council Directive on Honey (EU) ilianzisha mwongozo 2001/110/EG
tarehe 20 Desemba 2001 kwa ajili ya Nchi za Umoja wa Ulaya. Mwongozo huu
uliunganishwa katika kanuni za nchi husika mnamo mwaka 2003. Shirika la
Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO) na Shirika la Afya Duniani (WHO) la Umoja
wa Mataifa lilianzisha kiwango cha Ubora wa Asali katika orodha iitwayo Codex
Alimentarius, ambayo pia ilianza kutumika karibu mwaka huo huo 2003.
Sababu za kuanzishwa zilikuwa kulinda afya za wananchi na kukuza
biashara ya ulinganifu.Kanuni zote mbili zilibadili kanuni zilizotangulia,
lakini tofauti na hapo mwanzo, zote mbili zina masharti yanayofanana
sana. Tofauti iliyopo kwa sasa ni kwamba asali inayokusudiwa kuingizwa
katika nchi za Umoja wa Ulaya budi itoke kwenye nyuki aina ya Apis mellifera,
ambapo kanuni ya Codex inaruhusu vitu vitamu vinavyotokana na aina
nyinginezo za nyuki, kwa mfano Apis cerana na Apis dorsata kukubaliwa
kuitwa asali. Zaidi ya hayo, Umoja wa Nchi za Ulaya umeweka kanuni za
kuthibiti mabaki ya madawa ya kuua wadudu waharibifu na madawa ya kuua
vimelea vya maradhi.Mabaki yatokanayo na madawa ya kilimo, na madawa ya
kupambana na kupe wa aina ya Varroa haviwezi kuwa katika asali (au
vinaruhusiwa vikiwa ni kiasi kidogo sana). Mabaki ya madawa ya kuua
vimelea vya maradhi, kwa mfano yale yanayotumika kupambana na ugonjwa wa
harufu mbaya ya nyuki kinda (foul brood disease) hayaruhusiwi. Kanuni
ya Codex Alimentarius inatafsiri asali kuwa ni “kitu kitamu kinachotengenezwa
na nyuki kwa kutumia maji maji asili yenye utamu (nectar),
uteute wa seli za miti au ute ute wa wadudu wanaofyonza utomvu wa miti”. Nchi
za Umoja wa Ulaya na Codex wote hutambua kile wanachokiita “asali ya
waokaji mkate” ambayo ni ya kiwango cha
chini, ambayo imechemshwa kupita kiasi, au ambayo imechachuka.Uwekaji wa alama
za biashara kwenye asali kama hiyo (tazama mchoro Na. 27) unabidi kutimiza
matakwa yafuatayo. Alama hiyo ni lazima ioneshe jina la bidhaa (asali), ujazo
katika gramu, jina na anwani ya
mtengenezaji au aliyeingiza nchini bidhaa hiyo, namba ya idadi ya uzalishaji wa
kiwandani, na tarehe ya mwisho wa ubora wa bidhaa hiyo. Kwa ajili ya asali
bora, hii huwa ni miezi 18. Alama hizi pia huweza kutaja majina ya miti ya
vyanzo vya asali iliyomo katika pakiti au chupa (k.m. asali ya jamii ya miti ya
machungwa) iwapo asali inatokana na maua ya miti/mimea ya aina moja, na hii itajionyesha
katika rangi, harufu, ladha na muundo wa kikemikali na mwonekano na hata sifa za
kimaabara kwa darubini kali. Inaweza pia kuonesha eneo la kijiografia au chanzo
cha uoto iwapo bidhaa ni aina moja tu ya asali.
Kupeleka katika nchi za Umoja wa Ulaya
Asali
inayopelekwa katika nchi za Umoja wa Ulaya inahusishwa na kanuni iitwayo
Masharti ya Kiafya ya Nchi za Umoja wa Ulaya Kuhusu biashara na Uingizaji Asali
Nchini, ambayo huorodhesha hata baadhi ya nchi zinazoendelea. Ili kuongezwa
kwenye orodha hii, nchi inayoendelea budi itume maombi kwanza kwenye Umoja wa
Ulaya huko mjini Brussels, baada ya hapo ukaguzi utafanyika. Kampuni inayosafirisha
pia itabidi kupata idhini kupeleka nje asali. Anayepokea asali, kwa kawaida
atahitaji kwanza kupelekewa sehemu ya bidhaa na kuihakiki ubora. Vile vile
anaweza kuweka masharti ya ziada kabla ya kununua bidhaa.
Nchi nyingine
zina hiari ya kuingiza kanuni hizo za Umoja wa Ulaya katika masharti ya nchi
zao. Nchi nyingi zina viwango vya ubora wa asali, na viwango vya ubora wa nta, na
nchi chache zina viwango vya ubora wa mizinga ya nyuki. Shirika la viwango hutoa
hati ya ubora wa asali itokayo kwa wafugaji nyuki, wafanya biashara, na
wapakiaji asali katika kopo au chupa, wanaouza asali nchini. Hati ya ubora kwa kawaida
huwiana na kanuni za nchi za nje, lakini hutofautiana katika masuala
machache. Kanuni za Kimataifa za kuhakiki ubora hutumika hasa kuhusu asali
iliyofungwa kwa kuuzwa katika maduka ya kuuza vyakula tu, ambavyo katika nchi
nyingi vipo viwango A na B vya ubora. Asali ya ubora wa kiwango cha chini
inaweza kuuzwa nchini humo humo, kama kiwango cha B au asali ya kutoka katika
mizinga ya kienyeji.Kuhusu chavua, mkate wa nyuki, jeli ya kifalme, gundi
nyeusi na sumu ya nyuki, kwa kawaida, hakuna viwango vinavyotambulika.Hati ya
uchunguzi hutolewa na shirika la viwango kuonyesha kwa maafisa wa forodha iwapo
bidhaa inatakiwa kusafirishwa nje ya nchi.
Uingizaji katika nchi ya tatu
Kwa baadhi ya
mazao ya mifugo au kwa mazao yote yatokayo au yaendayo kwa wafugaji nyuki,
sheria ya kufungia uingizaji holela inaweza kutumika ili kuzuia uingizaji wa
magonjwa. Baadhi ya nchi, kwa mfano Kenya na Trinidad na Tobago haziruhusu
uingizaji wa mazao ya nyuki au vifaa vya ufugaji nyuki vilivyotumika. Kwa
habari zaidi tazama sura ya 14.5.
13.3 Kiwango cha
unyevunyevu wa asali
Kiwango cha
unyevunyevu cha asali bora huweza kuwa kati ya asilimia 14 hadi 19. Viwango vya
juu vya unyevunyevu, kufikia asilimia 30 hutokana na uvunaji wa mapema mno au
kuchanganya na maji au vitu
vyenye majimaji kwa mfano nyuki kinda. Jedwali Na. 5 inaonesha ni kwa muda gani
asali yenye viwango vya unyevunyevu mbalimbali itabaki na ubora wake. Namba
hizi zinatoa picha ya
kuridhisha kwa asali katika sehemu mbalimbali, lakini zimekusudiwa kwa tabia
nchi za wastani.Asali inaweza kuhifadhiwa kwa muda mrefu mradi tu kiwango cha unyevunyevu
ni chini ya asilimia 18. Ikiwa kiwango cha unyevunyevu ni cha juu zaidi,
mwishowe asali itachachuka. Iwapo kiwango cha unyevunyevu ni cha chini sana,
asali itaganda mapema, kutegemea kwa kiasi fulani na chanzo cha maji maji ya
sukari (nekta) na pia kiwango cha sukari ya wanga (glucose) na sukari ya
matunda (fructose) iliyomo, vile vile kuwapo kwa kokwa zinazotokana na kuganda
asali, lakini hali hii inaweza kupunguzwa kiasi kwa kuchemsha na kuchuja.
Kupima kiwango cha unyevunyevu
Kiwango cha
unyevunyevu huweza kupimwa kwa kifaa kinachoweza kushikwa mkononi cha kupimia unyevu
wa asali (tazama mchoro Na. 28). Hiki chombo huweza kuwa na vipimo vitatu:
kipimo cha kizio cha uharibifu (breaking index), kipimo cha asilimia ya sukari,
na kipimo cha asilimia ya maji
yaliyomo kwenye asali. Baadhi ya aina hizi za vipimo vya mkononi huwa na kipimo
kimoja tu, yaani cha kupima tu asilimia ya unyevunyevu ulio ndani ya asali. Huweza
kupima kuanzia unyevunyevu wa
asilimia 13 hadi 28 hivi.Vipimo hivi vya sukari vimeundwa kufanya kazi katika
joto la nyuzi 20 celcius. Kwa kupima unyevunyevu katika joto zaidi au pungufu
ya hapo, lazima kukokotoa tofauti ya nyuzi joto zilizozidi au kupungua.Kwa
kupima unyevunyevu wenye nyuzi joto zaidi ya 20 celsius, jumlisha 1/10% kwa
kila nyuzi joto inayozidi kwenye tarakimu zinazooneshwa kwenye kipimo. Kwa
kupima unyevunyevu wenye nyuzi joto chini ya 20 celcius, toa 1/10% kwa kila
nyuzi joto inayopungua kwenye tarakimu zinazooneshwa kwenye kipimo. Vipo vipimo
vya unyevunyevu wa asali vyenye kujirekebisha vyenyewe.Unyevunyevu wa asali
huweza kupimwa kwa kukokotoa usongo wa maada, yaani uzito kwa kila chembe ya
ujazo. Umakini wa kipimo hiki hutegemea na vifaa vilivyotumika, na ujazo. Asali
ina usongo maada wa kilo 1.4 hadi 1.44 kwa lita moja katika joto la nyuzi 20 celcius,
kutegemea na kiwango cha unyevunyevu
13.4 Kiwango cha
sukari katika asali
Kiwango cha
sukari katika asali ni karibu kinyume cha unyevunyevu wa asali hiyo. Kwa pamoja
hutimiza asilimia karibu 100. Asali ambayo ina asilimia 18 maji, ina asilimia
82 sukari mbalimbali, yaani sukari rahisi asili ya wanga (glucose),
(dextrose) na sukari asili ya matunda (fructose) (laevulose).
Asilimia hizi hutegemea asili za miti zilizo husika.Aina zote za asali hatimaye
hubadilika kuwa kavu pale sukari ya wanga itakapoganda. Jinsi sukari ya wanga
iwavyo nyingi, ndivyo asali itakavyoganda haraka, ambapo punje nyembamba na
zile zenye umbo baya zitaundwa, hapo asali itakuwa ngumu kabisa. Kwa kuikoroga
asali kama hiyo, itakuwa laini kisha huwa tepetepe badala ya kuwa kama
bonge.
Kuongeza sukari
Sukari inaweza
kuundwa kiudanganyifu kwa kuongeza sukari halisi kama ile itokanayo na nafaka (maltose)
au itokanayo na miwa (saccharose) au matunda. Katika maabara
ndogo,sukari halisi inaweza kufahamika kwa uchunguzi wa kimaabara. Hata hivyo
hii ni njia ngumu kufanywa mashambani.Uchunguzi wa moja kwa moja kuona kiwango
cha sukari ya wanga au ya matunda huwezekana, kwa kutumia vifaa rahisi ili
kufahamu mzunguko wa mwanga unaopita ndani ya asali inayochunguzwa kitaalamu
kwa njia hii.
13.5 Vimeng’enya
katika asali
Asali inavyo
vimeng’enya aina za “diastase”, “invertase” na “glucose –
oxidase”. Vimeng’enya hivi hulegezwa nguvu na kuharibika iwapo vitachemshwa.
Mazingira ya ufanisi wa vimeng’enya aina za “invertase”
na “glucose – oxidase” hutimizwa mara chache sana.
Kizio cha kimeng’enya cha diastase (Diastase
Index)
Kimeng’enya cha
“diastase”, ambayo pia huitwa “amylase”, huyeyusha wanga kikemia
kuunda sukari iitwayo “maltose”. Kizio cha “diastase” hutumika
kama kigezo cha upya na ubichi wa asali.
Ikiwa asali
itachemshwa kwa muda wa masaa 24 kwa joto la nyuzi 50 celcius, kimeng’enya hiki
kitakuwa bado ki salama kuweza kufanya kazi zake.
Kiwango cha HMF
Pamoja na
unyevunyevu, kiasi cha HMF (hydroxymethylfurfural) ni mojawapo ya vigezo
muhimu vya ubora wa asali. HMF ni ufupisho wa jina la kemikali inayoundwa kwa
sukari mojawapo ndani ya asali wakati inachemshwa au kupashwa joto kwa muda
mrefu. HMF inapatikana pia kwa wingi katika sukari ya miwa iliyochemshwa na pia
katika sukari iliyochacha. Kuwapo kwa HMF huweza kuonyesha kuundwa
kiudanganyifu na kuchanganywa na sukari mbalimbali. Kemikali hii haina sumu kwa
binadamu, lakini ni sumu kwa nyuki.
Kanuni
zitumikazo
Nchi za Jumuia
ya Ulaya na Codex Alimentarius zimeamua kwamba kiwango cha HMF ndani ya
asali kiwe chini ya mg 40 katika kilo ya asali. Asali ya masega, na asali
iliyochujwa kwa mtambo wa kujizungusha kwa
kasi, huwa na kiasi cha HMF chini ya mg 5 katika kilo ya asali. Asali
inapohifadhiwa, kiwango cha HMF huongezeka kwa mg 1 hadi mg 2 kwa kilo kila
mwezi katika joto la nyuzi 20 celcius. Baada ya miaka miwili (2) kiwango cha
juu kinachoruhusiwa cha mg 40/kg kitafikiwa katika hali ya kawaida. Katika
mazingira ya nchi za joto kizio hiki kitafikiwa mapema zaidi. Asali kutoka nchi
za joto huruhusiwa kisheria kuwa na kiwango cha HMF cha mg 80/kg mradi tu
yaoneshwe maandishi kwamba ni asali kutoka nchi za joto.
Kupima kwa uwiano kwa kutumia kemikali
ya “peroxide”
Siyo rahisi
kupima kiwango cha kimeng’enya cha “diastase” na HMF katika maabara
ndogo. Njia tofauti ya kutumia “peroxide” huweza kutumika, iwapo vipande
vya peroxide vya kupimia vinapatikana.Vipande hivi hugharimu kama Euro
50 hivi kwa kila pakiti, na ni lazima vihifadhiwe ndani ya jokofu (friji). Hivi
vipande hutumika kupimia kwa uwiano kupitia kimeng’enya cha “glucose –
oxydase” badala ya “diastase” moja kwa moja. Kanuni itumikayo ni :
wakati nyuki wanapunguza maji katika asali (ili iwe nzito), asali hulindwa isichachuke
kwa hewa iitwayo “hydrogen peroxide” ambayo hutengenezwa na vimeng’enya
katika kundi la “glucose – oxidase”.
Msaada wa
kimeng’enya hiki husitishwa pale kiwango cha sukari kinapozidi asilimia 80.
Iwapo asali inaongezwa maji, vimeng’enya huanza kazi tena. Kwa kupima msongo wa
hewa hii ya “hydrogen peroxide” saa moja baada
ya kuongeza maji katika asali, ukilinganisha na kiasi kile kile cha maji,
uwiano unaweza kufahamika kwa kusoma vipimo vinavyooneshwa kwenye vipande vya “peroxide”.
13.6 Uchambuzi wa
kimaabara
Maji maji yenye
sukari katika maua huwa na kiasi kidogo cha chavua kutoka kwenye ua hilo. Hii
huwezesha kutambua chanzo cha maji maji hayo katika asali. Uoto ambao nyuki
wameupitia na ambamo walijikusanyia chavua huweza kutambuliwa kwa kiasi fulani
kutokana na chavua. Kila kundi la mmea, aina yake na spishi yake huweza kutambuliwa
kwa uchambuzi wa kimaabara. Si vizuri kuwa na chavua nyingi mno ndani ya asali,
wala kuchuja hakuruhusiwi.Chavua inayoweza kuandaliwa kwenye vioo vya
kuchunguzia kwa darubini kali hutoka kwenye chavua ya mti katika sehemu ya
kiume ya ua, kwenye vifuko vya chavua vilivyo kwenye miguu ya nyuki, kwenye
mkate wa nyuki katika masega, na kwenye asali katika masega au baada ya
kukamua. Uchambuzi wa chavua hufanywa kama njia ya kuthibitisha chanzo cha
kijiografia au cha kiuoto wa asali. Asali itokanayo na jamii moja ya maua
hulazimu kuwa na asilimia kiasi fulani cha maji maji ya sukari ya maua kutoka
eneo husika. Hii ni muhimu kwa ajili ya uwekaji alama sahihi za bidhaa. Kwa
kufanya tafiti juu ya
chavua, au uchambuzi inasaidia kuwa na maarifa kuhusu mimea.Ni rahisi kuona
kama asali imechachuka, kwa sababu ya tabaka la povu ambalo hutokea juu ya
asali na harufu ya spiriti. Minyororo ya povu la hamira huweza kuonekana iwapo
tone la asali iliyochachuka itachunguzwa kwa darubini kali.
13.7 Rangi, harufu na
ladha ya asali
Rangi, harufu,
ladha, na utepetevu wa asali huitwa “sifa za kihisia” za asali. Ladha na harufu
ya asali kimsingi kabisa huundwa kwa maua na mimea iliyotoa asali. Lakini sifa
hizi huweza kuingiliwa na mabadiliko
yanayoweza kutokea ndani ya masega, hasa kwenye masega ambayo hapo awali
yalijaa nyuki kinda iwapo asali itakaa humo kwa muda mrefu.
Kanuni
Sheria inaagiza
tu kwamba asali inaweza kutofautiana kwa rangi kutoka rangi nyeupe nyeupe hadi
ile ya kahawia nyeusi, vile vile kwamba isiwe na ladha na harufu isiyo ya
kawaida. Nchi kadha huwa na masharti kwa
ajili ya rangi ya asali inayouzwa. Vielelezo vya rangi vinapatikana kwenye
masoko kusaidia kutambua rangi hizo, kwa mfano nyeupe isiyo nzito, nyeupe ya
wastani, nyeupe yenye giza, nyeupe yenye
karahabu (amber) karahabu halisi, na karahabu yenye giza. Rangi ya asali
iliyoganda ni nyeupe nyeupe. Umuhimu wa vigezo vyovyote hutofautiana baina ya
nchi na nchi, lakini pia baina ya walaji
binafsi.
13.8 Ubora wa mazao
mengine ya nyuki
Chavua
Chavua (ikiwa
katika hali ya malundo madogo) budi ikaushwe mnamo siku moja baada ya kuvuna,
na ihifadhiwe katika sehemu kavu ili kudumisha sifa zake za kibiashara. Sifa
zinazohusu lishe na uwezo wa kutoa joto la mwili hutajwa kwa kila gramu 100
(mia) za chavua (au kama asilimia) baada ya kukaushwa. Kiwango cha unyevu hupungua
wakati wa kukausha kutoka asilimia 25 (mbichi/mpya) hadi asilimia 12, au chini
yake. Viambato vingine kama vifuniko vya nta na taka sakafuni mwa mzinga,
sharti zisiwemo. Chavua ni lazima ikaushwe ili kuzuia kuvu lisiote. Sumu ya
kuvu (aflatoxin) ambayo inatengenezwa na baadhi ya kuvu, hairuhusiwi
kupatikana ndani ya
unga wa chavua.
Chavua ambayo inakusanywa kutoka katika mimea iliyopuliziwa madawa ya kuua
wadudu waharibifu yawezekana kuwa na masalia ya madawa hayo. Unga unga wa aina
nyingine, kwa mfano unga wa mihogo, huweza pia kukusanywa na nyuki.
Mtengenezaji anapaswa kufuatilia na kuepusha taka katika unga wa chavua.
Mkate wa nyuki
Mkate wa nyuki
unabidi kukaushwa mnamo siku chache baada ya kuvunwa au uhifadhiwe ndani ya
jokofu kabla ya kusagwa.
Jeli ya kifalme
Jeli ya kifalme
iliyo mpya inaweza kuhifadhiwa katika joto la hali joto ya kawaida, kwa siku
chache tu. Kwa hiyo ni bora zaidi kuihifadhi ndani ya jokofu. Moja wapo ya
viini lishe vinavyoweza kupimwa vilivyomo katika jeli ya kifalme ni 10-HDA (hydroxy-2-decenoid
acid) ambayo ni asilimia kati ya 2 hadi 10 ya maada. Hiyo asilimia ya 10-HDA
huandikwa kwenye hati ya uchambuzi wa kimaabara. Jeli ya kifalme yenye ubora wa
kutosha huwa na asilimia tano (5%) ya 10 – HDA. Jeli ya kifalme budi pia isiwe
na makapi kama vile ya madawa ya kuua vimelea.
Nyuki kinda wapya
Nyuki kinda
wapya (wabichi) waliovunwa huweza kuhifadhiwa kwa siku moja tu, na ni lazima
waliwe siku hiyo hiyo, au kukaushwa, kuwekwa chumvi kwa kuhifadhi au kukaushwa
kwa moshi, au kukaangwa. Pia
huweza kuhifadhiwa katika jokofu (friji) au kuchanganywa na asali.
Nta
Nta ni lazima
iyeyushwe kwa joto la wastani (chini ya nyuzi 80 celcius). Iwapo nta
itachemshwa kupita kiasi itakuwa na rangi ya kahawia na ubora wake utashuka.
Njia rahisi za kukamua ndizo zinazofaa
kuhifadhi ubora wa nta. Kigezo kikuu cha ubora wa nta ni kutokuwa na uchafu.
Nta iliyochanganywa na mafuta maalum ya taa (liquid paraffin), mafuta
mazito, au mafuta mapesi huwa duni, haiwezi kununuliwa na kwa hakika haipaswi
kupelekwa nchi za nje. Vichafuzi vinaweza kutambuliwa kwa kupima kizio cha
kuyeyuka kwa bidhaa.
Gundi nyeusi
Gundi nyeusi
iliyokwanguliwa kutoka kwenye mbao za mzinga kwa kawaida huwa na vipande vya
nta, nyuki au miguu ya nyuki, nywele, vipande vidogo vya vumbi la mbao, na taka
nyingine. Hizi lazima ziondolewe kama bidhaa inatakiwa kuliwa hapo hapo.
Tofauti na hivi, haidhuru sana kwa ubora wa gundi nyeusi ikiwa chafu au safi,
kwa mfano ikitumika spiriti kuiengua gundi nyeusi.Gundi nyeusi
kutoka nchi za joto ina kiwango kidogo cha kemikali zenye uwezo. Hizi zinaweza
kuwa hata chini ya asilimia 10, ambavyo gundi nyeusi iliyosafishwa itokayo
katika tabia nchi wastani huweza kuwa na kemikali hizi hadi asilimia 50. Maada
nyinginezo huweza kuwa nta za miti, nta halisi, na taka ngumu kwa mfano nyuzi
za mbao, na nywele nywele kutoka katika sehemu za mimea, singa za kondoo, au
vipande vya rangi au vanishi ya kulainisha mbao. Vitu hivi hunata kwenye miti au
vitu vingine ambavyo hukusanywa na nyuki.
Sumu ya nyuki
Sumu ya nyuki
ambayo imekaushwa kwenye kisahani cha kioo na baadaye kukwanguliwa, huonekana
kama unga unaonata wenye rangi ya krimu hadi nyeupe – nyeusi. Ubora wa sumu ya
nyuki hutambuliwa kwa kiasi kilichomo cha kemikali ya mellitin, ingawa
vipo vigezo vingine vya utambuzi. Sumu ya nyuki iliyokaushwa huwa na sumu ya asilimia
40 hadi 60 ya mellitin.Sumu ya nyuki iliyosafishwa inaorodheshwa katika
makala nyingi za kitabu cha orodha za madawa (kiitwacho Pharmacopoeia) kwa jina
la Apium venenum, lakini pia hutumika katika utabibu wa kutumia mazao ya
nyuki kama nyongeza kwenye vyakula au lishe. Hadhi ya bidhaa hii siyo wazi
katika kila nchi. Katika nchi nyingi, sumu ya nyuki huweza kusafishwa katika
maabara zilizopewa vibali.Sumu ya nyuki ina madhara hata kwa kiwango cha chini
sana, na watu wengine hupata mzio kwa sumu hii. Tahadhari na kanuni za
tahadhari ni vya muhimu sana katika uzalishaji na usafishaji wa sumu ya nyuki
14 Uuzaji
Asali, chavua,
mkate wa nyuki, nyuki kinda, masega, na jeli ya kifalme ni vyanzo vya lishe
bora kutoka kwenye mzinga wa nyuki.Huweza kuliwa moja kwa moja au baada ya
kusindikwa.
Ø Asali kwa
kawaida hukamuliwa kutoka kwenye masega
Ø Chavua hukaushwa
mara baada ya kuvunwa.
Ø Mkate wa nyuki
humenywa kutoka kwenye masega na kukaushwa.
Ø Nyuki kinda
huliwa baada ya kuvunwa au hukaushwa nakutengenezwa nyongeza za bidhaa za lishe.
Ø Masega huliwa
baada ya kuvunwa au hutumika katika mapishi mbalimbali.
Ø Jeli ya kifalme
huliwa baada ya kuvunwa au huhifadhiwa ikiwa imewekwa katika jokofu (friji) au
ikiwa kavu.Nta, gundi nyeusi, na sumu ya nyuki pia ni mazao ya awali, lakini
haviwezi kuliwa katika hali hiyo. Huweza kuwa sehemu ya bidhaa zinazoliwa au
kuweza kusindikwa kuwa nyongeza kwa bidhaa za lishe, au bidhaa za madawa. Baada
ya kuvunwa (au kukamuliwa, katika suala la nta), bidhaa hizi huweza kuhifadhiwa
kwa muda mrefu bila kufanyiwa mbinu za kuhifadhi. Kiasi kingi huweza
kukusanywa, kutoka kwa wafugaji nyuki wengi, na kuwekwa ghalani kwa miaka kadhaa.
Bidhaa nyingi sana huuzwa sana nchini katika vipimo vidogo vidogo, ambavyo pia
huweza kupelekwa nchi za nje kwa mzigo mkubwa.
Ubora wa bidhaa
hufahamika katika hatua mbalimbali katika mnyororo wa thamani jinsi inavyooneshwa
katika sura ya pili na katika jedwali kwenye kiambatisho Na. 2.
14.1 Bidhaa za awali
Sifa zake
Lishe iliyomo
katika mazao ya nyuki ina uwezo wa kutoa joto la mwili, kutokana na kuwa na
protini, mafuta na wanga. Vile vile huwa na vitamini, na madini, pamoja na
maada nyinginezo, baadhi yake vikiwa na
thamani kwa tiba. Nta, gundi nyeusi, na sumu ya nyuki havina uwezo wowote wa
kutoa joto la mwili, na vina kiasi kidogo cha madini na vitamini, kwa hiyo
havifanyi kazi kama lishe au nyongeza kwenye
lishe katika hali ya awali, labda tu gundi nyeusi. Nyuki wenyewe ni bidhaa ya awali,
na hutumika kutengeneza dawa za asili.
Uzalishaji
Mazao ya awali
huvunwa kutoka ndani ya mzinga wa nyuki, kwa mfano asali, chavua, nyuki kinda,
masega, nta, jeli ya kifalme, na gundi nyeusi. Mazao mengine, kama chavua
iliyokusanywa na sumu ya nyuki
hukusanywa na mfugaji nyuki kutoka kwenye kundi la nyuki, kwa kutumia vifaa
kama vile mtego wa chavua na chombo cha kukusanya sumu kinachowekwa nje ya
mzinga. Nyuki hukusanywa kutoka kwenye
mzinga, au kutoka kwenye makundi ya nyuki wasiofugwa, kwa jitihada za wawindaji
makundi ya nyuki wa porini.
14.2 Mazao yatokanayo
Mazao ya awali
ya nyuki huweza kuwa sehemu ya bidhaa nyingine, yakiongezwa kwenye bidhaa hizo,
au yanaweza kutengenezwa kuwa bidhaa tofauti. Hizi bidhaa zilizoundwa huweza
kuingia katika mafungu kadhaa. Chakula, lishe za kiafya, nyongeza kwenye
vyakula, madawa yatokanayo na nyuki, madawa, bidhaa za urembo, bidhaa za kulinda
afya, au bidhaa za viwandani. Viambatisho Na. 1 na 2 vimeorodhesha bidhaa za
awali na zile zitokanazo na hizo za awali, kwa matumizi nje ya mwili au ndani
ya mwili.
Uchavushaji
Zao jingine ni
uchavushaji wa mbegu na matunda, kwa kuweka kundi la nyuki ndani ya shamba au
jirani na shamba. Kwa kawaida uchavushaji ni zao muhimu kuzidi mazao yote ya
mzinga wa nyuki.Ongezeko la
mavuno ya mbegu na matunda ni kubwa mara kadhaa zaidi kuliko asali kwenye
shamba hilo. Kama ilivyoelezwa katika sura ya tatu, mwenye mazao ndiye
mnufaikaji wa kwanza wa zao hilo la kundi la nyuki. Kwa hiyo malipo kwa mfugaji
nyuki huweza kuandaliwa kimkataba. Uchavushaji huweza kuuzwa lakini hauwezi kusafirishwa
nje ya nchi. Biashara katika aina mbalimbali za wadudu wanaochavusha mazao
inaendelea kukua na uzalishaji wa spishi maalum za wadudu wanao chavusha hutoa
fursa za biashara hii kwa wafugaji nyuki.
14.3 Uuzaji nchini
Ubora
Vigezo vikuu
katika uuzaji wa mazao ya nyuki ni ubora, uhakika wa kupatikana bidhaa muda
wote, na uendelevu. Mahitaji ya asali kwa kawaida ni ya kiwango cha juu, na
hivyo siyo kikwazo kwa uuzaji wenye faida. Ubora ndiyo kigezo cha kwanza. Iwapo
mavuno yana ubora wa kiwango cha juu, mnunuzi atarudi tena na tena, wala hataenda
kwa wauzaji wengine wa bidhaa hii, hata waweke bei ya chini. Mazingira
bora ya kutoa mavuno bora, uvunaji, usafirishaji, kuhifadhi, kusindika na
kufunga kwa ujazo katika pakiti au kopo yameelezwa katika sura ya 2 hadi 12 kwa
mazao mbalimbali.Kwa jumla, kila
zao lisiwe na mabaki ya vitu hai au visivyo hai, kama vile madawa ya kuuwa
vimelea, madawa ya kuua kupe, au madawa ya kuua wadudu waharibifu, pia yasiwe
na taka zozote. Ili kuepuka uchafuzi wa aina hizi, ufugaji nyuki kwa mitindo
isiyohitaji madawa ndio mtindo ufaao. Mbali na faida ya kutokuwapo mabaki ya
kemikali na taka nyinginezo, kama vile sukari kwa mfano, mazao yaliyopata hati
ya uasilia (organic) huweza kuuzwa kwa bei nzuri zaidi. Soko la dunia
pamoja na mahitaji yake yanayoongezeka ya mazao ya uasilia, hulipa vilevile
fedha zaidi kwa mazao ya uasilia ya nyuki.
Mazao ya awali
Asali, chavua,
mkate wa nyuki, nyuki kinda, jeli ya kifalme, nta, gundi nyeusi, sumu ya nyuki
na uchavushaji hufaa kwa kuuzwa ndani ya nchi. Uuzaji rejareja, kama
inavyooneshwa katika mchoro Na. 5, ni chaguo bora zaidi. Wakati mwingine
wanunuzi wanazidi mazao yaliyopo kununuliwa. Uuzaji wa jumla wa pakiti
ndogondogo, au kuuza kwa wachuuzi wadogo wadogo au migahawa, ni njia nzuri ya nafasi
pili.Kwa sababu ya bei ndogo ya uuzaji nchi za nje, kusafirisha nje ya nchi siyo chaguo la
busara kwa wafugaji wadogo wadogo wa nyuki.Lakini kwa ufugaji nyuki kwa kiwango
kikubwa,ambao unazidi mahitaji ya wanunuzi wa nchini, bila shaka, ziada inaweza
kuuzwa kwa jumla au kusafirishwa nje ya nchi.
Uuzaji asali nchini
Kwa kawaida,
mfugaji nyuki au chama cha wafugaji nyuki hutoa asali ya aina mbalimbali. Asali
nyeupe nyeupe, na yenye weusi kidogo huweza kutenganishwa kwa urahisi wakati wa
kuvuna au inaweza kukamuliwa na kutunzwa katika vyombo tofauti. Asali
inayotokana na maua ya aina moja huweza kuhifadhiwa peke yake ili kupata asali
ya aina mbalimbali.Asali huweza kuuzwa ikiwa majimaji, au iliyochujwa, au kama masega
au mapande, au kama iliyopondwapondwa (mchoro Na 29). Asali iliyofungwa
mchanganyiko wa aina 3 za asali katika kopo / pakiti ikiwa na rangi
zinazotofautiana ni bidhaa ya kupendeza. Chupa za kioo au za plastiki
inayopitisha mwanga ni chaguo bora kwa vile mnunuzi huweza kutambua rangi kwa
kuona asali iliyo ndani ya chupa. Chupa za kioo zinaweza kuwekwa katika vikapu
na mapambo ya kienyeji kuchapishwa kwenye karatasi la utambulisho wa bidhaa.Jeli
mpya ya kifalme huweza kuuzwa kama bidhaa isiyochanganywa, au iliyochanganywa na
asali, ili kuihifadhi vizuri.
Mazao yatokanayo
Kuuza mazao
yatokanayo na mazao mengine ya nyuki ni njia ya kupanua idadi ya bidhaa
mbalimbali. Kuongeza asali kwenye mazao yatokanayo na nyuki hukuza thamani ya
mazao haya. Kwa mfano, asali pamoja na jeli ya kifalme, au asali
iliyochanganywa na chavua au unga wa gundi nyeusi huweza kuuzwa kwa bei nzuri
zaidi kuliko vikiwa pekee pekee. Bidhaa zilizotengenezwa pamoja na nta, asali, chavua,
jeli ya kifalme, gundi nyeusi, na sumu ya nyuki, ni nzuri kwa uuzaji ndani ya
nchi, hasa kwa rejareja. Viambatisho Na. 1 na 2 vinatoa ushauri na mapendekezo.
14.4 Upangaji bei
Upangaji bei ya
bidhaa hutegemea wanunuzi, upatikanaji, ubora, sifa za kipekee, pakiti (aina ya
ufungashaji), na kama ni bidhaa toka nje au ndani ya nchi. Matumizi na manufaa
na vigezo vingi mbalimbali.Wanunuzi wa mazao ya nyuki ni wengi. Bei za nchini
zinalingana duniani kote, bila kujali thamani ya sarafu. Kwa suala la mazao ya awali
ya nyuki, ni vema kufahamu kama bidhaa inatumika zaidi kama chakula, nyongeza
katika vyakula, au kwa madawa, pia kama kutokana na hali hiyo mazao yanauzwa
katika masoko ya vyakula, katika zahanati au maduka ya dawa. Hii hutofautiana
sana katika sehemu mbalimbali duniani na mazingira asilia ya masoko hayo.
Mazao yenye
thamani ya kitabibu yana bei kubwa zaidi kuliko kwa vyakula.Kutokana na
maendeleo ya mbinu za ufugaji nyuki, na uingizaji wa aina bora za nyuki,
kusababisha ongezeko la uzalishaji katika nchi fulani fulani, upo mwelekeo wa
ununuzi zaidi wa asali zenye rangi nyeupe nyeupe na ladha nyepesi. Katika nchi
ambamo asali inatumika zaidi kama dawa, matumizi ya asali huweza kuwa pungufu
ya gramu 10 kila mtu kwa mwaka ambavyo katika nchi ambamo asali inatumika kama
chakula, huweza kuwa gramu 500 hadi zaidi ya gramu 1000 kila mtu kwa mwaka. Hii
huitwa “ulaji wa kila mtu” kwa bidhaa.
Upangaji bei za reja reja
Duniani pote,
asali huuzwa moja kwa moja kutoka kwa mfugaji nyuki hadi kwa mnunuzi. Mfugaji
nyuki anajivunia mno zao lake kiasi cha kupuuza kuruhusu watu wengine wauze
bidhaa yake, na mnunuzi anaamini zaidi bidhaa hiyo iwapo mfugaji nyuki ni mtu anayefahamiana
naye. Hata hivyo, katika uzalishaji wa kiasi kikubwa cha asali, au kukusanya
pamoja asali katika vyama vya ushirika, asali huuzwa kama bidhaa nyingine
yoyote kupitia wauzaji wa rejareja na maduka. Upakiaji wa asali kwa kiwango
kikubwa unahitaji mbinu za uchemshaji na usafishaji ambavyo hufanya asali kuwa
aina ya bidhaa za kiwandani. Hii haiathiri sana bei ya rejareja. Kwa hiyo
wafugaji nyuki wa vijijini watapenda zaidi kuuza asali moja kwa moja kwa wateja
au kupitia wauzaji wa reja reja, ili wauze kwa wingi badala ya kuhangaika na
kutumia mbinu za kusindika asali na kuuza asali katika kopo au chupa
kwenye maduka ya kifahari ambamo wanunuzi ni wachache (tazama mchoro Na. 30).
Upangaji bei za jumla
Mwuzaji wa
kwanza wa asali iliyosindikwa huweza kupata punguzo la asilimia 20, kutoka
kwenye bei ya reja reja. Kama wapo wauzaji wawili katikati, mwuzaji wa kwanza
kwa kawaida hununua kiasi kingi, na kwa hiyo atapata punguzo kubwa zaidi, kama
asilimia 30 hadi 40 kutoka kwenye bei ya reja reja.Mnunuzi wa asali kwa wingi
anaweza kupata punguzo la asilimia 50 kutoka kwenye bei ya reja reja. Katika
hali ya kuwa na wanunuzi wa katikati au kiwanda cha usindikaji na upakiaji
katika chupa, punguzo linaweza kufikia asilimia 80 chini ya bei ya reja reja.
Bei katika soko la dunia ya Euro 1 hadi 1½ kwa kilo moja ya asali iliyouzwa
nchi za nje, hupanda mwaka hadi mwaka na mwaka 2003, bei ilikuwa zaidi ya Euro
3 kwa kilo, lakini mwaka 2005 bei za asali ziliporomoka kasi sana hadi chini
ya Euro 1 kwa kilo katika soko la dunia. Kwa upande mwingine, bei ya jumla
huleta Euro 6 na bei ya rejareja ni Euro 6 hadi 8 kwa kilo. Kwa hiyo
usafirishaji bidhaa nje ya nchi ni mara chache kumnufaisha mfugaji nyuki wa
kiwango cha chini.
Utangazaji bidhaa
Kutangaza bidhaa
humaanisha kuwafahamisha wanunuzi wa jumla, maduka ya reja reja, na wanunuzi na
walaji, kuhusu sifa maalum au ubora wa bidhaa yako. Kwa nini wanunue bidhaa
yako? Masuala muhimu ni utofauti, bidhaa tokanishi, ladha, thamani kwa tiba, na
ubora wa bidhaa kuliko bei ya bidhaa yenyewe. Habari kwa wanunuzi kuhusu
thamani ya bidhaa ni suala la lazima. Yapo mawazo na mbinu nyingi sana za
kutangaza bidhaa ambazo huweza kutumika mahsusi kwa mazao ya nyuki. Tazama pia
Agrodok Na. 26: Uuzaji Bidhaa kwa wazalishaji wadogo wadogo.
Mahali pa kuuzia
Kufuatana na
habari zilizokusanywa mahali ulipo, unaweza kuamua kulenga sehemu kadhaa za
kuuzia bidhaa. Wauzaji wa reja reja hupenda masoko madogo sana na vituo vya
mafuta ya magari vilivyo na wanunuzi wengi huweza kuchaguliwa. Katika suala la
maduka ya vyakula vya kifahari au masoko ya kimataifa, utalazimika kutoa bidhaa
zako kwa mzigo mkubwa wenye aina mbalimbali kwa idadi uliyoagizwa. Katika hali
hii, unaanza kutoa bidhaa aina moja mpaka ianze kununuliwa vizuri, kisha
uongeze aina mbalimbali. Unatakiwa vile vile kufahamu ujazo wa pakiti ambazo
zinapendwa kununuliwa zaidi, makaratasi ya kufungia bidhaa, pia kasi ya ununuzi.
Sehemu bora sana za kuuza na kuanzisha soko la daima ni kwenye maonesho maalum
ya asali.
14.5 Viwango vya
ubora na ithibati
Kama tulivyoona
katika ibara 13.2, katika nchi nyingi, Shirika la Viwango huweka masharti
katika kiwango cha kisheria cha ubora wa asali, kiwango cha ubora wa nta, na
kiwango cha ubora wa mizinga ya nyuki. Hiki cha mwisho kwa kawaida
hakidhibitiwi, lakini hutumika kuhamasisha watengenezaji wa mizinga wafananishe
muundo ili kuwezesha mwingiliano wa zana na vipuri vya mizinga hiyo, kwa mfano
papi za juu ya mzinga wa nyuki na fremu na kadhalika. Mfugaji yuko huru kuunda
mzinga kwa kadri atakavyo.
Hati na ithibati
Hati
za kawaida
Kama
ilivyoelezwa katika ibara 13.2 hati ya uchambuzi wa bidhaa ni muhimu kwa ajili
ya soko la nchi za nje. Inawezekana vile vile kupata hati za uthibiti ambazo
zinawiana na kanuni mbalimbali, kwa mfano, hati ya ithibati ya mazao ya uasilia
(organic produce). Kanuni katika masuala haya hulenga siyo asali iliyo
na makapi, bali kwamba imezalishwa kwa kufuata masharti ya uzalishaji wa
uasilia (organic production).
Hati
za ithibati ya uasilia
Kwa ajili ya
biashara katika mazao ya uasilia, (organic products) mzalishaji, na
mfanyabiashara anayeingiza bidhaa nchini, wote budi wapate hati za
ithibati mahsusi. Masharti ya muhimu sana katika uzalishaji wa uasilia
kwa mazao ya nyuki ni:
Ø mazingira yasiwe
na madawa ya kuua wadudu wala mazao yaliyoundwa kwa kubadili uasilia wa chembechembe
(genetically modified crops)
Ø maradhi yatibiwe
kwa kutumia madawa asilia yaliyoruhusiwa tu
Ø nyuki walishwe
tu asali yao wenyewe
Ø papi za
kuanzisha masega zilizotokana na mbao za uasilia ndizo tu zimetumika Hati ya
ithibati ya uasilia ni ya gharama kubwa sana, lakini matumizi hayo kwa jumla
hufidiwa na bei ya juu ya kuuzia inayolipwa kwa ajili ya mazao ya uasilia. Hata
hivyo, hii inaleta faida kwa kiasi kingi cha mazao.
Hati za ithibati kwa biashara ya
ulinganifu (fair trade)
Baada ya
kuanzishwa kwa hati ya ithibati kwa biashara ya ulinganifu, vyama vya biashara
za ulinganifu vinapenda kuwabana wafanyabiashara walanguzi katika biashara hii
katika nchi zinazoendelea. Kwa kuondoa hawa walanguzi ambao mara nyingi hupata fedha
zaidi kutoka kwenye zao husika, kuliko wazalishaji wenyewe, hawa wazalishaji
wataweza kupata fedha hizo badala ya walanguzi. Bei ya wanunuzi, kwa jumla huwa
haibadiliki, au ni ya juu kidogo kufuatana na gharama ya juu ya kufuatilia hati
ya ithibati.Lakini lengo linalokusudiwa hufikiwa mara nyingi na ithibati kwa kweli
hufanya biashara kuwa linganifu.
Kupeleka bidhaa nje ya nchi
Ili kuweza kuwa
na faida katika kupeleka asali au nta nje ya nchi, mazao ambayo kwa kawaida
huuzwa pekee yanaweza kufungwa pamoja ili kujaza sanduku la mizigo ya melini.
Masanduku haya huweza kutunza
mapipa ya ujazo wa lita 70, 200, 205 au 210 za asali, kila pipa likiwa na uzito
wa kilo 300. Nta inaweza kusafirishwa ikiwa mabonge ya kilo 50, kufikia uzito
wa tani 18 katika sanduku moja la mzigo. Ziada lazima iandaliwe mapema na
kuwekwa kando kuzuia asali au nta isiuzwe kwa wateja wengine kabla ya kupelekwa
nchi za nje, kwa vile wanunuzi wa hapo hapo nchini ni wengi pia.Njia nyingine
ya kupeleka asali nje ya nchi ni kupitia watu wanaosafiri nje ya nchi.
Wanapofika kuwatembelea ndugu zao, mara nyingi wanaondoka na bidhaa asili za
nchini. Hii ni fursa kubwa ya soko. Faida kubwa ni kwamba masharti ya kawaida
huwekwa kando, kwa sababu huwa ni kiasi kidogo tu ambacho kanuni za viwango na ushuru
wa forodha havihusiki.
Bei ya ntaa kilo 25 ni shilingi ngapi??
ReplyDeleteasali huchukua mda gani hadi kurinwa?
ReplyDeleteNaomba kupata andino la mazao ya nyuki kwa afya pelee
ReplyDelete