Habari

   UTARATIBU WA KUOMBA VIBALI KWA AJILI YA KUSAFIRISHA MAZAO YA MISITU NA NYUKI
Mazao ya Misitu na nyuki ni kati ya mazao yanayozalishwa nchini na kuuzwa nje ya nchi na kuliletea taifa fedha za kigeni. Ili kuhakikisha kuwa biashara ya mazao ya misitu na nyuki inafanyika kwa njia halali, serikali imeweka sheria, kanuni na taratibu zinazopaswa kufuatwa na wafanyabiashara wote wanaosafirisha mazao hayo nje ya nchi. Zifuatazo ni taratibu za kuzingatia katika kusafirisha mazao ya misitu na nyuki nje ya nchi.
Mazao yanayoruhusiwa;
  • Mbao
  1. Mbao za miti laini za pine na cypress
  2. Mbao za miti migumu yote yenye unene usiozidi nchi nne
  3. Mbao za sakafu za miti yote
  4. Mbao za mpingo zilizochanwa na kurandwa kwa saizi maalum hususani vifaa vya muziki
  5. Samani, milango, madirisha, vitanda, meza, fremu za milango na madirisha
  • Magome ya miti
  • Vinyago na sanaa
  • Mafuta ya msandali
  • Gundi ya miti
  • Mazao ya nyuki kama asali, nta, gundi ya nyuki, maziwa ya nyuki
  • Nyuki
  • Chavua
  1. Magogo ya miti ama yoyote na umbo lolote
  2. Msandali usiokamuliwa mafuta
  3. Mkaa
Kuomba kibali
Uuzaji wa mazao ya misitu na nyuki nje ya nchi unaruhusiwa baada ya kupata kibali/idhini kutoka kwa katibu mkuu, wizara ya maliasili na utalii.
Maombi ya Kibali
Mfanyabiashara anayetaka kibali cha kuuza mazao ya misitu nje ya nchi atapata kibali baada ya kujaza fomu ya maombi.
Katika fomu hiyo mhusika atatakiwa kujaza mazao yote ambayo anategemea kuuza nje kwa mwaka mmoja wa fedha. Kibali kitatolewa ambapo mwombaji atajaza fomu itakayomgharimu kiasi cha Tsh 5,000/= .
Pamoja na fomu hiyo ataambatanisha vielelezo vifuatavyo:-
  1. Hati ya usajili wa kampuni kutoka kwa msajili wa makampuni
  2. Hati ya leseni ya biashara ya nje kutoka wizara ya viwanda na biashara
  3. Hati ya kadi ya mapato au usajili (TIN) kutoka kwa mamlaka ya mapato Tanzania (TRA)
  4. Mkataba wa mauzo kutoka kwa mnunuzi utakaoonyesha bei ya mazao hayo kwa thamani ya dola za kimarekani au fedha zinazokubalika kimataifa, ujazo, uzito au idadi ya mazao
  5. Taarifa ya mapato kwa mauzo ya mwaka uliopita. Taarifa ithibitishwe na benki inayotumiwa na mhusika kuweka fedha (hii ni kwa ajili ya wanaooomba kuendelea na biashara)
  6. Hati ya usajili ya kusafirisha mazao ya misitu na nyuki nje ya nchi kutoka wizara ya maliasili na utalii
  7. Barua ya kutoka kwa meneja wa shamba la miti, afisa misitu/ hifadhi wilaya kuonyesha kuwa mazao yanayoombewa kibali yatavunwa katika wilaya/eneo husika
  8. Uthibitisho wa kumiliki kiwanda cha misitu au mkataba kutoka kwa mwenye kiwanda kuwa mazao yatakayosafirishwa yatazalishwa katika kiwanda chake
Maombi yakikubalika, kibali cha mwaka mmoja wa fedha (Julai hadi Juni) kitatolewa.



  SIKU YA ASALI TANZANIA
Siku ya asali Tanzania ni siku ambayo imetengwa maalumu kwa ajili ya kuonesha mazao na teknolojia mbalimbali za ufugaji nyuki.Siku hii ya asali Tanzania (Honey Day) itakuwa inafanyika kila mwaka mwezi wa saba.Kwa mwaka huu "Honey Day" itafanyika katika maenesho ya saba saba uwanja wa mwalimu Nyerere Dar es Salaam.Siku hii itakuwa na lengo kubwa la kuhamasisha wadau mbalimbali wa idara ya nyuki kuweza kuhudhuria katika maenesho makubwa ya mazao ya nyuki na teknolojia yatakayofanyika mwezi wa kumi hapo hapo katika uwanja wa mwalimu Nyerere Dar es salaam.Maonesho haya yameandaliwa kwa kusaidiana na Tan Trade, Wizara ya maliasili na Utalii, Ofisi ya Waziri Mkuu pamoja na wadau wengine wa nyuki.Kwa maelezo zaidi kuhusu maonesho haya ya jinsi ya kuhudhuria tadhali wasilina na mwenyekiti na msimamizi wa kamati Mr Kamara Kaizerage kwa namba 0788-326309.
Tafadhali tunaomba maoni yako kuhusu maonesho haya ili kuboresha zaidi.

ASANTE BOLENY INTERNATIONAL
Boleny International ni kampuni kubwa inayojishughulisha na shughuli mbalimbali Africa, Hivi karibuni kimejikita nchini Tanzania na kufungua kampuni nyenza Organic Honey ambayo itajihusisha na usindikji wa asali Tanzania.Tunatoa shukrani zetu za dhati kma wadau wa idara ya nyuki Tanzania kwa Boleny International kwa kuokoa idara yetu ya nyuki.Kwa habari zilizopo kiwanda hiki kinauwezo wa kusindika zaidi ya tani 1000 ila kwa kuanzia wanahitaji tani 700 tu kutoka katika Mikoa yote nchini Tanzania.Kazi n kwetu wafugaji tuongeze jitihada za kufuga kwani mkombozi amekuja.
                                  
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akifungua kiwanda cha kusindika asali cha Organic Honey katika kijiji cha Visiga mkoani Pwani kinachomilikiwa na kampuni ya Boleyn International, Juni 9, 2012.Kushoto ni mkuu wa mkoa wa Pwani Mwantumu Mahiza na anyepiga makofi katikati ni Mkururugenzi Mtendaji wa kampuni hiyo, Jack Liu. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

RAW COMB HONEY CAN ADD VALUE.
                                         
Ni vigumu sana kupata asali halisi ikiwa katika sega halisi lililotengenezwa na nyuki.Na kwa kutumia asali iliyokuwa bado ipo katika sega halisi la nyuki unajihakikishia kuwa unatumia asali ambayo bado ipo katika ubora wa hali ya juu.Hivyo ni vyema kama mfugaji nyuki au wauzaji wa mazao ya nyuki kuweza kuanza biashara ya kufungasha asali ikiwa bado ipo katika sega lake halisi kwa kutumia vifungashio maalumu.
                                             WATOAJI NYUKI (BEE REMOVER)

Kwa mahitaji yako yote ya kuondoa nyuki sehemu yoyote ambayo wanaweza kuleta madhara kama vile majumbani, kanisani, hospitalini, hotelini, kwenye majengo mbalimbali, minara ya simu na maeneo mengine, tafadhali wasiliana nasi kwa huduma hiyo.
Huduma zetu ni za haraka na kwa bei nafuu sana.Kwa sasa tupo Dodoma, Dar es salaam, Morogoro na Tabora.Tupigie kwa simu namba 0762-630050

             KITABU KIPYA-(KIONGOZI CHA MFUGAJI NYUKI) KIPO MADUKNI

Hiki ni kitabu kipya ambacho kitatumiwa na wafugaji wa nyuki kwa ajili ya kuwaongoza katika maswala mbalimbali ya ufugaji wa nyuki, kitabu hiki kimekusanya mambo mbalimbali ambayo yatamsaidia mfugaji wa nyuki kubadilika na kubadilisha kabisa ufugaji wake kutoka ufugaji nyuki wa kitamaduni na kuhamia katika ufugaji wa nyuki wa kisasa.
Hivyo ni vyema kila mfugaji nyuki mmoja mmoja au kwa vikundi kujipatia nakala yao kwa ajili ya kujisomea kwa lengo zima la kuiendeleza idara ya ufugaji wa nyuki Tanzania.
Kwa maelezo zaidi wasiliana nasi kwa simu namba 0762-630050

                ULISHAJI BORA WA NYUKI KIPINDI CHA KIANGAZI


Kwa ujumla kipindi cha kiangazi huwa ni kipindi kigumu sana kwa nyuki, huwa ni msimu ambao huwa hukumbwa na njaa pamoja na kiu kubwa ya maji, kwani huwa na ukame mkubwa kwa kuwa hakuna mvua zinazoendelea kunyesha hivyo kwa mfugaji wa nyuki ni vyema akajiandalia mazingira mazuri kwa ajili ya nyuki wake kwa kuwatengenezea vyombo vya kuwawekea maji, picha hapo juu ni mfano wa vijengeo kwa ajili ya kuwawekea maji nyuki hasa kipindi cha kiangazi, vijengo hivi vina majani ya majini, majani haya yana kazi kubwa sana kwa nyuki kwani nyuki huwa wanatua katika majani haya na ndip;o kufyonza maji.Bila majani haya nyuki watakuwa katika mazingira magumu sana ya kujipatia maji kwani watakosa sehemu ya kutua ili kufyonza maji na mwisho wake wataishia kuzama ndani ya maji.Hivyo katika uandaaji wa visima hivi ni vyema kuzingatia kuweka majani au vijiti ambavyo nyuki watatumia kutua kwa urahisi ilki kunyonya maji vizuri bila kuzama ndani ya vidimbwi hivyo.
Utengenezaji wa mazingira mazuri kwa ajili ya nyuki kunywa maji husaidia sana kupunguza kasi ya makundi ya nyuki kuhama hasa kipindi cha kiangazi kutokana na ukame na uhaba wa maji, hivyo wafugaji nyuki na wataalamu wa nyuki ni vyema kuelimishana juu ya maandalizi ya sehemu za kunyweshea maji nyuki hasa kipindi cha kiangazi.

                                      UFUNGASHAJI WA MAZAO YA NYUKI
Kwa ujumla ufungashaji wa asali kwa kiwango kama hiki unaongeza thamani za mazao ya nyuki, ni vyema wafugaji wa nyuki kuanzisha vikundi vya ufugaji nyuki vya kufungasha mazao ya nyuki kama asali kwani yanaboresha kibato mara dufu kuliko kuuza ikiwa mali ghafi.Kwa pamoja tujenge kwa pamoja na kuiendeleza idara ya ufugaji nyuki Tanzania.
                   TUNATUMIA VIPI MISITU YETU KWA KUFUGIA NYUKI?


Tanzania tumejalisha maeneo mengi sana na makubwa yenye misitu minene yenye chavua na nectar kwa wingi, maeneo haya yapo karibu Tanzania nzima hayana matumizi yoyote yale ya ufugaji wa nyuki, kwa nchi nyingi Africa kama vile Ethiopia na nchi nyinginezo ambazo zinasemekana kuongoza kwa ufugaji nyuki zinatamani sana maeneo mazuri tuliyonayo.
Ukizunguka maeneo mbalimbali ya Mkoa wa Tabora, Rukwa, Katavi, Kigoma, Singida,Dodoma, Shinyanga na Mikoa mingine mingi, rasilimali hizi za misitu zimebweteka na hakuna hatua zozote zinazochukuliwa na serikali yetu ya kuwekea mkazo katika kuwekeza kwa ufugaji wa nyuki.
Tungeweza kuzalisha “Organic Honey” kwa wingi ambayo ndio inahitajika kwa wingi katika soko la dunia kwa kiasi kikubwa, lakini ipo wapi? Pia ni vyema tukapanda miti maalamu kwa ajili ya kuzalisha asali kwa matumizi maalumu kama vile milonge na miti mingine ambayo inaaminika kuwa ina tiba mbalimbali katika miili ya binadamu, kwa kufanya hivi tutaweza kuzalisha asali ambayo nayo itakuwa na tiba maalumu kama “manuka honey”.
Tusisitize serikali za vijiji kutoa maeneo hayo ya mizitu yenye mahitaji ya nyuki kwa vikundi mbalimbali vya wafugaji nyuki ili kuweza kuiboresha na kuiendeleza idara hii ya ufugaji nyuki

  UZALISHAJI WA MALIKIA KWA KUTUMIA -JENTER SYSTEM


Kwa nchi nyingi zilizoendelea wanatumia njia mbalimbali za kuzalisha malikia kutokana na tabia zao wanazozihitaji kama vile:-

1. Uwekaji wa asali kwa wingi.
2. Uzalishaji wa kundi kwa kasi kubwa.
3. Utendaji wa kazi kwa kasi kubwa.
4. Uchavushaji wa kasi nzuri zaidi na nyinginezo.
Hizo ni miongoni mwa tabia ambazo wafigaji huwa wanazitumia kwa ajili ya kuchagua kundi la kuzalishia malikia.
Miongoni mwa njia rahisi nay a haraka ya kuzalisha malikia ni kwa kutumia Jenter Method.Hiki ni kifaa ambacho kinawekwa ndani ya mzinga na malikia hutaga ndani yake, mara baada ya mayai kuangulia na kufikia siku mbili au tatu mayai yale husambazwa katika mizinga mbalimbali kwa ajili ya kulishwa royal jelly.
Hii ni changamoto kubwa kwa serikali yetu ya kuanzisha kituo cha kuzalisha malikia ambayo yatakuwa chanzo kikubwa cha makundi yenye tabia zinazohitajika.Tunaamini kuwa wapo wataalamu wa nyuki wengi waliosomea uzalishaji wa malikia kutoka Tanzania na kusomeshwa katika nchi mbalimbali, wapo wapi?
Naamini idara ya nyuki ni miongoni mwa idara chache ambazo zipo kwenye nafasi nzuri za kumkomboa mfujai mmoja mmoja katika kipato chake.Hivyo ni jukumu la serikali kuweka mkazo kuanzia ngazi za halmashauri mpaka kushuka chini juu ya ufugaji nyuki wa kisasa wenye tija.

12 comments:

  1. napenda kujua nyuki uchukua muda gani kwa kuitengeneza asali na kuwa tayari kwa kuvunwa?

    ReplyDelete
  2. nakipataje kitabu chenu kuhusu ufugaji nyuki? na je ni shilingi ngap? mim nipo tabora

    ReplyDelete
  3. can i get market for my bee products outside the country?
    Nina asali ya masega, asali ya kimiminika, poleni na propolis

    ReplyDelete
  4. Mpango mzuri tunafikiwaje sisi wazalishaji wadogo shida ni soko sio uzalishaji ,tunahitaji right price at a right time

    ReplyDelete
    Replies
    1. Yeyote mwenye asali nzuri inayokizi viwango vya kuuza nje tafadhari piga 0757239250

      Delete
  5. Nahitaji mizinga ya kisasa. Mwenye kujua inapopatikana naomba tuwasiliane kwa namba yangu ya WhatsApp 0677892261

    ReplyDelete
  6. Nahitaji kujua jinsi yakutengeneza mizinga ya kisasa.napatikana kwa namba ya WhatsApp:0754071757.

    ReplyDelete
  7. Kwa mizinga bora ya nyuki
    Weka order 0747 338 055

    ReplyDelete
  8. Kwa maitaji ya nyuki wasio Uma Yani mzinga na nyuki nichek WhatsApp namba 0783268025

    ReplyDelete