Ufugaji Nyuki



Kwa kawaida makundi ya nyuki katika nchi ya Tanzania na baadhi ya nchi zinazolingana kwa tabia za nchi, makundi ya nyuki huanza kutafuta sehemu salama na yenye chakula kwa wingi kuanzia mwezi wa kumi katika mwaka mpaka mwezi wa nne kwa mwaka unaofuata.Kipindi hiki huwa na makundi mengi yanayozunguka hapa na pale kutafuta nyumba ambayo itawafaa kwa ajili ya makazi yao na kwa ajili ya kuhifadhia chakula.

Hiki ndio huwa kipindi muafaka sana kwa wafugaji kuanza kutega mizinga ambayo imeshaandaliwa kwa ajili ya kufugia nyuki.Kwa kuwa makundi mengi huwa yanatafuta sehemu za makazi hivyo ni rahisi sana kuyakama na kuyahifadhi makundi hayo kwa ajili ya uzalishaji wa mazao ya nyuki.

Kutokana na hilo, mfugaji anapaswa kuanza kuandaa sehemu ya kufugiua nyuki na mizinga yake mapema zaidi kabla ya msimu huo kufika ili asiweze kukosa makundi ya nyuki.Unashauriwa kuanza kuandaa mazingira ya kufugia nyuki na mizinga angalau mwezi mmoja kabla kwa kusafisha, kukarabati au kutengeneza kile unachokihitaji.


VIFAA VINAVYOPASWA KUANDALIWA.
Kabla ya kuanza kufuga nyuki kuna vifaa ambavyo mfugaji wanyukiu anapaswa kuanza kuviandaa mapema kabla ya msimu wa ufugaji wa nyuki kufika.Vifaa hivyo ni kama vifuatavyo:-

UJENZI WA MABANDA YA KUFUGIA NYUKI.
Eneo ambalo kuna wanyama wa aina mbalimbali ambao wanaweza kufanya uharibifu mbalimbali wa mizinga pindi ikiwa na nyuki na kusababisha uharibifu wa mizinga, kuua nyuki au hata mnyama mwenyewe kufa kutokana na kudungwa na nyuki.Hivyo ujenzi wa mabanda ya kufugia nyuki ni vyema ukafanyika.

DHAMIRA YA UJENZI WA MABANDA YA KUFUGIA NYUKI.
Mabanda hayo ya kufugia nyuki yanaweza kuwa ya udongo, tofali au ya miti pekee pande zote, milango pamoja na kuezekwa kwa nyasi.
Kuna sababu mbalimbali ambazo zinasababisha mfugaji nyuki kuweza kujenga mabanda ya kufugia nyuki, miongoni mwa sababu hizo ni:-
1.      Kukinga mizinga na jua na mvua.
Hii ni sababu moja wapo ambayo inasababisha mfugaji wa nyuki kuamua kujenga mabanda ya kufugia nyuki, mzinga unapokuwa kwenye kivuli huusaidia mzinga kuweza kudumu kwa kipindi kirefu, pia kivuli husaidia nyuki kufanya kazi zao kwa juhudi.Iwapo mzinga utakuwa upo kwenye jua nyuki hutumia muda mwingi kupunguza joto la ndani ya mzinga badala kutumia muda huo kwa ajili ya kutafuta chakula.

Nyuki wanapoona jua ni kali zaidi na kusababisha joto kali ndani ya mzinga huamua kuhama katika mzinga huo na kwenda kutafuta makazi sehemu nyingine.Hivyo nio vyema mzinga ukakaa kwenye kivuli na sehemu isiyoweza kunyeshewa na mvua.

Pia mvua inaponyeshea mzinga husababisha mbao kuweza kuoza ndani ya muda mfupi, hivyo kwa kujengea banda la kufugia nyuki huweza kuukinga mzinga wako dhidi ya mvua ambayo inasababisha kuozesha mbao za mzinga wako.

2.      Kukinga na wanyama waharibifu
Mabanda haya ya kufugia nyuki husaidia sana kwa wanyama waharibifu wa mizinga kushindwa kuifikia mizinga lakini pia husaidia sana kupunguza mashambulizi ya nyuki kwa viumbe wengine.Mizinga huwekwa ndani ya banda na banda kufungwa milango.

3.      Ulinzi na ukaguaji
Ujenzi wa mabanda ya kufugia nyuki husaidia sana kuiweka mizinga yako sehemu salama dhidi ya wezi wa mizinga au asali lakini pia husaidia sana wakati wa uangalizi wa mzinga.Mizinga inapokuwa pamoja uangalizi wa mizinga hiyo huwa ni rahisi sana na pia huweza kusaidia kipindi cha uvunaji na uwekaji wa kumbukumbu za kila mara.

Pembeni ya banda hilo sehemu ambazo mizinga inawekwa huwekwa matundu maalumu ya kutoka na kuingia nyuki kwa ajili ya kujitafutia chakula chao.

MIZINGA YA KUFUGIA NYUKI.
Mizinga ya kufugia nyuki inapaswa kuandaliwa mapema kabla ya msimu wa kukamata makundi ya nyuki haujafika.Mizinga inayopaswa kuandaliwa ni kama ifuatayo:-

1.      Mzinga wa kibiashara
Huu ni mzinga wa kisasa unaotumika kwa wafugaji wa nyuki hasa wale wanaotaka kuvuna asali kwa wingi kwa ajili ya kuuza.Mzinga huu huweza kuzalisha asali kwa wingi kadri misimu ya uvunaji inavyoongezeka mwaka hadi mwaka.
Mzinga huu una sehemu kuu tatu kama zifuatazo:-
a.      Box la kuzalishia watoto wa nyuki
Ni box ambalo kwa kawaida huwa la kwanza kwa upande wa chini.box hili ndilo ambalo huwa na mlandfo wa nyuki kuingia na kutoka pindi wanapokwenda na kutoka kwenye utafutaji wa chakula.Box hili hutumika na malikia wa nyuki kwa kutagia mayai pamoja na kulelea watoto ambao husubiri kuanguliwa na kuwa nyuki kamili.
Pia box hili hutumika kwa ajili ya nyuki kuhifadhia chakula chao kwa ajili ya msimu wa kiangazi, msimu ambao huwa hauna maua yenye chakula cha nyuki cha kutosha,Hivyo mfugaji hapaswi kuvuna asali anayoikuta katika brood box, kwa kuvuna asali unayoikuta katika brood box husababisha kundi lako kuhama kwa kukosa chakula.
Kwa kawaida matumizi ya mzinga huu huanza kuvuna asali baada ya wastani wa misimu miwili mikubwa yaani sawa na miaka miwili.Na mara baada ya kipindi hicho kipita mfugaji huweza kuanza kuvuna kwa vipindi tofauti tofauti vya mwaka na kuendelea.
b.      Kitenga malikia
Hiki ni kifaa kama nyavu ambacho huwekwa kati ya brood box na super box, wavu huu huweza kumzuia malikia asiweze kupanda katika super box kwa lengo la kutaga mayai.matundu ya waya huu ni madogo kulingana na umbile la nyuki watenda kazi peke yao.Hivyo malikia na madume ya nyuki hayawezi kupanda kuelekea kwenye super box.

c.       Box la kuhifadhia asali
Hili ni box ambalo huwekwa juu mara tu baada ya queen excluder.Box hili huwa ni maalumu kwa nyuki watenda kazi kuweza kuhifadhi asali yao kwa wingi.Asali inayokuwa katika box hili haiwezi kuchanganyika na watoto wa nyuki wala chavua kutokana na kuwapo kwa queen excluder chini yake.Asali inayotoka katika Box hili huwa nzuri na safi kutokana na kutochanganyika na masega ambayo yalitumika kwa kuangulia watoto wa nyuki.
Uvinaji wa asali katika mzinga huu, mfugaji anapaswa kutoa frame zilizopo katika super box ambazo asali yake tayari imeiva.Mara baada ya kutoa frame hizo mfugaji anapaswa kukamua asali hiyo kwa kutumia mashine ya kisasa iitwayo  Honey Centrifuge Machine.Mashine hii huweza kufyonza asali yote iliyopo katika sega na kubakiza sega likiwa halina asali.

Mara baada ya hapo mfugaji anapaswa kurudisha sega hilo kwenye mzinga likiwa na frame yake ili nyuki aweze kujaza asali tena.Hii inamsaidia sana nyuki kumpunguzia kazi ya kujenga sega jipya la Sali kila baada ya mvuno wa asali na hivyo kuongeza uzalishaji wa asali mara dufu.Tofauti tu ya aina ya mzinga huu ni kwamba huwezi kupata zao la nta.

2.      Mzinga wa viunzi
Huu ni mzinga wa teknolojia ya kati kutoka kwenye mizinga ya kienyeji na kuelekea mizinga ya kisasa.Mzinga huu uhifadhi wake wa asali hautofautiani sana na uhifadhi wa asali katika mizinga ya kienyeji, isipokuwa katika mzinga huu masega hupangwa kwa kufuata utaratibu wa viunzi vilivyowekwa.nyuki huweka sega moja katika kila kiunzi kimoja cha mzinga huu.
Mzinga huu pia haujagawanywa kwa kutenganisha sehemu za kuhifadhia asali na sehemu ya malikia kuangulia watoto.Hivyo asali itokayo katika mzinga huu huweza kuchanyanyika na watoto iwapo mfugaji hatakuwa makini katika uvunaji wa asali hiyo.

Uvunaji wa mzinga huu, mfugaji anapaswa kukata sega lote lenye asali pekee na kulihifadhi katika chombo kisafi kwa jili ya kukamua asali hiyo kwa kutumia mashine ya kusasa au kwa kutumia njia za kitamaduni.

PICHA ZA MABANDA TOFAUTI TOFAUTI YA KUFUGIA NYUKI

Picha 1:Banda la kufugia nyuki lililojengwa kwa miti na kuezekwa kwa udongo maarufu kama tembe.
Picha 2:Banda la kufugia nyuki lililojengwa kwa miti na kuezekwa kwa nyasi
Picha 3:Nyumba ya kufugia nyuki iliyojengwa kwa matofali na kuwekewa midomo maalumu ya nyuki kwa ajili ya kuingia na kutoka pindi wanapokwenda kutafuta chakula
Picha 4:Kibanda kidogo cha kisasa kwa jili ya kufugia nyuki.
Picha 5:Banda la kufugia nyuki lilijengwa kwa miti na kuezekwa kwa bati
Picha 6: Banda la kufugia nyuki lilijengwa kwa miti, kuezekwa kwa bati na kuwekewa uzio wa waya.

49 comments:

  1. Hongera kwa maelezo mahsusi. Naomba kupata kitabu cha Ufugaji wa Nyuki.
    Mchg.Joseph Muhehwa
    0756 025 146 / 0789 025 146

    ReplyDelete
  2. This comment has been removed by the author.

    ReplyDelete
  3. Tunashukuru kwa kazii nzuri muliofanya ila naomba munitumie kitabu cha ufugaji wa nyuki.
    Asante,
    HUSSEIN AHMED
    hirsitz@hotmail.com

    ReplyDelete
  4. naomba kupata kitabu cha ufugaji wa nyuki
    0654517602
    ndichihero@gmail.com
    dar es salaam

    ReplyDelete
  5. asanteni sana ndugu kwa elimu yen nzuri sana. Endeleeni kuielimisha jamii ili ijikwamue kiuchumi.

    ReplyDelete
  6. Ahsante kwa maelezo, ila naomba kujua nia wapi ntapata mavaziya kuvunia asali?

    ReplyDelete
    Replies
    1. Unaweza kupata mavazi kutoka kwetu lakini pia yapo makampuni binafsi ambayo pia unaweza kupata mavazi hayo, bei na ubora ni vitu unapaswa kuzingatia sana kabla ya kufikia hatua ya kununua vazi hilo

      Delete
  7. nashukuru sana naomba kupata ratiba yenu kwa vipindi vya ufugaji wa nyuki

    ReplyDelete
  8. Asante sana Frolian kwa kutembelea ukurasa wetu, naomba ufahamu kuwa ratiba ya ufugaji nyuki zinatofautiana sana kulinga na eneo la nyuki walipo. Kwa mfano kwa sasa tuna mradi wetu Mkoani Tabora, ambapo vipindi vya ufugaji nyuki wa mkoa huu ni viwili yaani Msimu mkubwa unaonza mwezi June - August na Msimu mdogo unaonza mwezi Decemba - Februari. Ni vyema ukatufahamisha wewe kwa sasa unaishi mkoa gani

    ReplyDelete
  9. Samahan mfano kwa mkoa wa njombe je?

    ReplyDelete
  10. Samahan mfano kwa mkoa wa njombe je?

    ReplyDelete
  11. Ma Vihe. Hbr naomba kuwasiliana na nyie mie nipo Tabora na ni mfugaji ila sina uzoefu

    ReplyDelete
  12. Samahani naomba kuwasiliana na nyie Mimi ni kijana ninayetaka kujikita katika suala LA ufugaji Wa nyuki nipo Sokoine university hapa morogoro

    ReplyDelete
  13. nawezaje pata Kitabu cha ufugaji Nyuki?

    ReplyDelete
  14. Mnapatikana wapi....kama kuna kitabu ngependa kukisoma email yangu ni fai.nargis@gmail.com

    ReplyDelete
  15. Ahsante sana kwa makala hii kwa imekuwa chachu kwangu juu ya uanzzishaji wa kufuga nyuki mahali ninapoishi.

    ReplyDelete
  16. Naomba kupata kitabu cha namna ufugaji wa nyuki 0655071992

    ReplyDelete
  17. Mimi naitaji nta Kama tan 1 je naweza kupata

    ReplyDelete
  18. Nmejifunza nashukuru sana kwa kupata elimu hii ntakapopata wasaha ntawasiliana nanyi

    ReplyDelete
  19. Elimu ni nzuri Kikubwa ni kutoa hamasa zaidi ili kufikia hatua kubwa ya ufugaji

    ReplyDelete
  20. Nilikua nahitaji vifaa vya kuvunia asali

    ReplyDelete
  21. Nahitaji kujua ivunajinsumu ya nyuki na soko.make likoje?

    ReplyDelete
  22. Somo Zuri, Lakini Je Endapo Mtu Una Eneo Lililo Karibu Na Makazi Ya Watu Laweza Kufaa?

    ReplyDelete
  23. Somo zuri sana je naweza fuga nyuki ninapoishi bila madharaà

    ReplyDelete
  24. Nashukuru kwa elimu nzuri nahitaji kujua bei ya mzinga mmoja wa kisasa na mavazi ya kuvaa unapowahudumia nyuki tafadhali.

    ReplyDelete
  25. Ningeomba kitabu kama kipo au softcopy

    ReplyDelete
  26. Asanteni kwa darasa huru, natarajia kufanya mradi huu kwa ajili ya biashara. Hivyo Napenda kujua tathmini ya gharama za awali. Eneo lengwa Ni mkoani Tabora

    ReplyDelete
  27. Shukran kwa elimu nzuri kuhusu ufugaji wa nyuki. Nataka kujua kama ufugaji huu unaweza kufanyika mikoa mingine zaidi ya Tabora. Mimi eneo langu liko mkoa wa Pwani ambako nataka kufanya mradi huu kibiashara. Pia nataka kujua gharama za mizinga ya kibiashara ili niweze kujipanga kuanza zoezi. Ahsante

    ReplyDelete
  28. Nashukuru sana kwa elimu ya ufugaji nyuki.Mimi ni mfugaji wa nyuki nimeanza na mizinga ishirini ya kisasa,ninafuga eneo la Monduli juu Arusha nimeanza mwezi wa Dec mwaka jana 2019,natamani angalau kuwa na mizinga mia,ninaomba kujua ni wapi ninaweza kuuza asali kwa faida

    ReplyDelete
  29. Naomba msaada wenu wa hali na Mali Mimi nikijana ambae nahitaji sana na natamani sana kufuga nyuki ila ninaupungufu wa elimu ya nyuki kwa Sasa nipo chuoni ila napenda kujishungulisha na ufugaj wa nyuki kwa mda huu no 0622095530.msaada wenu wakuu.

    ReplyDelete
  30. Asante sana kwa elimu safi. Mimi nataka kuuliza ni maeneo yapi na muhimu kwa ufugaji na pia kuhusu masoko yakoje?

    ReplyDelete
  31. Asante.Mimi naomba msaada wenu kufahamu kuhusu aina ya nyuki safi,gharama na masoko pia na bei za asali: Mathew 0787110812

    ReplyDelete
  32. nataka nijue ni aina gani ya mimea ambayo nikiipanda itakuwa chakula cha nyuki

    ReplyDelete
  33. Kwa mtu anayehitaji eneo la kufugia nyuki mnamsaidiaje?

    ReplyDelete
  34. Ahsante sana ni mafunzo mazuri sana kwa mwenye nia ya kufuga nyuki kwa matumizi ya kawaida na kibiashara pia.

    ReplyDelete
  35. Kwakweli nimependa elimu yenu je mtu akitaka kujifunza zaidi huwa mnadarasa?pia naweza kukipata kitabu?mimi samson toka arusha0786912960 samsnsanya127@gmail.com

    ReplyDelete
  36. Kwakweli nimependa elimu yenu je mtu akitaka kujifunza zaidi huwa mnadarasa?pia naweza kukipata kitabu?mimi samson toka arusha0786912960 samsnsanya127@gmail.com

    ReplyDelete
  37. Kwakweli nimependa elimu yenu je mtu akitaka kujifunza zaidi huwa mnadarasa?pia naweza kukipata kitabu?mimi samson toka arusha0786912960 samsnsanya127@gmail.com

    ReplyDelete
  38. kwa anayehitaji asali nina kiasisi kikubwa cha asali na nta no 0756428695

    ReplyDelete
  39. Msaada wa kitabu. Mungu awabariki sana

    ReplyDelete
  40. Mimi niko moshi mjini na ningependa kufuga naomba kama kuna mawakala wenu hapa ili niweze pata mizinga ya kisasa.
    Asante

    ReplyDelete
  41. Nimeanza ufugaji nyuki. Hadi Sasa Nina mizinga 85 ya kisasa.mzinga mmoja TU ndio umeingia nyuki tangia Oct/2021. Naomba ushauri.nafugia wilaya ya ulanga kata ya Lupilo. Halmashauri Haina mtaalamu was nyuki

    ReplyDelete
  42. Kwa wafugaji walioko dodoma wanaweza kuvuna asali zaidi ya maramoja? Kama ndio ni mara ngapi na kipindi kipi na kipi

    ReplyDelete
  43. Haiqezekani hate Maria nne kama mzinga yako iko maeneo yanayokua na majimaji kwa mwaka mzima n.a. malisho toshelevu ya Nyuki.

    ReplyDelete
  44. Nahitaji Kitabu Cha Ufugaji Nyuki na Ushauri Zaidi.
    Whatsapp Namba-0652380737

    ReplyDelete