Kazi zetu

Nyuki Mkombozi Company ni kampuni iliyosajiliwa kisheria yenye usajili namba 248557 chini ya sheria ya usajili wa makumpuni ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Kampuni hii imedhamiria kufanya mambo makuu yafuatayo hasa katika idara ya ufugaji nyuki Tanzania

1.Kushauri na kushawishi wananchi wengi zaidi hasa wenye kipato cha chini kujikita katika uwekezaji wa ufugaji wa nyuki au katika kipengele chochote kilichopo katika uwekezaji wa idara ya nyuki kama vile
  (a) uuzaji wa vifaa vya kufugia, kuvunia na kufungashia mazao ya nyuki.
  (b) Utengenezaji wa vifaa vinavyohusiana na idara nzima ya ufugaji wa nyuki.
  (c) Uanzishaji wa kiwanda kidogo cha kusindikia mazao ya nyuki kama vile asali na nta.
pamoja na nyanja nyingine nyingi ambazo muwekezaji anaweza kupewa fusra ya kuwekeza katika idara ya nyuki Tanzania.

2.Kuunganisha wajasiriamali walipo na masoko ya mazao ya nyuki yaliyopo ndani na nje ya nchi.

3. Kutoa elimu ya ufugaji nyuki pamoja na utengenezaji wa vifaa vya kisaa vinavyohusiana na idara nzima ya ufugaji wa nyuki Tanzania na nchi jirani.

4.Kuishauri serikali juu ya maboresho ya idara ya nyuki Tanzania hasa vijijini.

5.Kushirikiana bega kwa bega na wadau nwengine wanaohisiana na njia moja au nyingine na idara ya ufugaji nyuki kama vile wadau wa masoko, misitu na wadau wengine wengi Tanzania na nchi ya jirani.

3 comments:

  1. NAOMA KUPATA BEI ZA MIZINGA YA KISASA,NA VIFAA VYOTE VYA UVUNAJI NA UKAMUAJI WA ASALI

    ReplyDelete
  2. Ni muda gani huchukua asali kukamilika au kuwa tayari kwa kulinwa baada ya mzinga kuwa na nyuki tayari ?

    ReplyDelete
  3. Naomba kupata wanunuzi wa jumla wa asali mbichi ya nyuki awkubwa

    ReplyDelete