Picha na Video

MAONYESHO YA KILIMO NA MAZAO YALIYOANDALIWA NA SACAU YALIYOFANYIKA WHITESAND HOTEL TAREHE 13-15/05/2013 DAR ES SALAAM


















UZINDUZI WA KIWANDA CHA KUSINDIKA ASALI KINACHOMILIKIWA NA HONEY KING KILICHOPO VISIGA-MADAFU-KIBAHA.

Ziara ya wafugaji nyuki wanaofadhiliwa na shirika la Farm Africa kutoka Babati Manyara walipotembelea katika kiwanda cha kusindika asali cha Honey King kilichopo Visiga Madafu kwa lengo la kujionea shughuli mbalimbali zinazofanywa na kiwanda hicho.Katika Picha ni Gasper Shirima Mtaalamu wa chakula (Food Safety Officer) akielezea jinsi mtambo wa kufungasha asali unavyofanya kazi.Ziara hiyo ilifanyika tarehe 07/02/2013.(Picha na mpiga picha wetu)




Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akifungua kiwanda cha kusindika asali cha Organic Honey katika kijiji cha Visiga mkoani Pwani kinachomilikiwa na kampuni ya Boleyn International, Juni 9, 2012.Kushoto ni mkuu wa mkoa wa Pwani Mwantumu Mahiza na anyepiga makofi katikati ni Mkrurugenzi Mtendaji wa kampuni hiyo, Jack Liu. (Picha na mwandishi wetu)
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akikagua mitambo baada ya kufunguza kiwanda cha kusindika asali cha Organic Honey katika kijiji cha Visiga mkoani Pwani kinachomilikiwa na Kampuni ya Boleyn International, Juni 9, 2012. (Picha na mwandishi wetu)
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akikagua vifaa mbalimbali vinavyotumika katika usindikaji wa asali katika kiwanda cha Honey King ambacho kitakuwa kinasindika orgaic honey kinachomilikiwa na Boleny International, Aliyeweka mikono mfukoni ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Bw Said Meck Sadiki, Juni 9, 2012. (Picha na mwandishi wetu)


Mheshimiwa Waziri Mkuu akikagua mzinga wa nyuki wa kisasa aina la "Langstroth" mara baada ya kufungua kiwanda cha kusindika asali kilichopo visiga-Kibaha, Mizinga hii inayosambazwa na kampuni ya Honey King.

                                 UFUGAJI NYUKI WA KISASA

Hili ni banda la kufugia nyuki linaloonesha ufugaji nyuki wa kisasa unaoendelea katika shamba la Mheshimiwa Waziri Mkuu-Mizengo Pinda lililopo Dodoma.
Kuna aina nyingi za ujenzi wa mabanda ya kufugia nyuki kwa ajili ya kivuli pamoja na kuzuia mvua.Huu ni mfano wa banda la kisasa la kienyeji la kufugia nyuki lilipo katika shamba la kufugia nyuki la Mh. Pinda lililopo kijijini kwake Kibaoni-Mpanda


SEGA LA ASALI ILIYOVA











hili ni sega la asali ya nyuki wanaouma, sega hili lina asali ambayo imeiva kabisa na sasa ipo tayari kwa kuvunwa.Asali inayotoka kwenye sega kama hili ni asali ambayo ina kiwango cha hali ya juu, sega hili limetoka kwenye mzinga aina ya top bar.

WAFUGAJI NYUKI WAMTEMBELEA MH.PINDA
Mheshimiwa Waziri Mkuu, Pinda akipokea zawadi ya asali kutoka kwa kikundi cha wafuga nyuki kutoka Zanzibar asali iliyotokana na nyuki wanaouma.Asali hii inatokana hasa na maua ya mti wa Mkarafuu.Inaaminika kuwa asali hii kwa kiasi kikubwa ni tiba inayotibu magonjwa mengi.P(icha na mpiga picha wa nyuki wetu Tanzania)


Mheshimiwa Waziri Mkuu Mizengo Pinda akinywa chai ya pamoja na vikundi vya wafuga nyuki kutoka Mafia na Pwani, wataalamu wa Ufugaji nyuki pamoja na maofisa wa TASAF nyumbani kwake Dodoma baada ya kutembelea shamba lake la mfano la ufugaji nyuki lililopo Zuzu nje kidogo ya Mkoa wa Dodoma.



Mheshimiwa Waziri Mkuu akiwa katika piha ya pamoja na baadhi ya maofisa wa TASAF, maofisa nyuki pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Pemba walioongozana na vikundi vya wafugaji nyuki kutoka Mafia na Zanzibar walipomtembelea nyumbani kwake Dodoma, Kulia kwake ni Mkurugenzi Mkuu wa TASAF.(Picha na Mpiga Picha wetu)


Mhehimiwa Pinda akiwa katika picha ya pamoja na wafuga nyuki kutoka Pemba na Mafia pamoja na wataalamu wa nyuki na maofisa kutoka Mfuko wa TASAF walipomtembelea nyumbani kwake Mjini Dodoma.(Picha na mwandishi wetu)

ZIARA YA WAKUU WA MIKOA NA WILAYA KWENYE SHAMBA LA UFUGAJI NYUKI LA MH.PINDA DODOMA.




Mheshimiwa Pinda aitoa darasa la ufugaji nyuki wa kisasa kwa Wakuu wa Mikoa na wakuu wa Wilaya walipomntembelea kwenye shamba lake Mjini Dodoma 29/05/2012
.(Pica na mwandishi wetu)
Mheshimiwa Pinda akitoa darasa la jinsi ya kutumia mashine ya kisasa ya kuchakatulia asali kwa wakuu wa Mikoa na Wakuu wa Wilaya walipomtembelea shambani kwake.29/05/2012


Nyuki wetu Tanzania
Mheshimiwa waziri Mkuu Mizengo Pinda akiwa katika haraati za kutafuta eneo linaofaa kwa shughuli za ufugaji nyuki wanaouma.Ni vyemna kuchagua eneo zuri la kufugia nyuki na kulifanyia tathmini kabla ya kuanza kufuga nyuki.(Picha na Mpiga picha wetu)
                      MAWASILIANO YA NYUKI KWA "WAGGLE DANCE"Nyuki kama walivyo viumbe wengine hutumia njia nyingi kama mawasiliano baina yao.Waggle dance ni miongoni mwa njia ambayo nyuki hutumia kwa ajili ya mawasiliano ya kwenda kutafuta chakula.Mawasiliano ya waggle dance hutumika kwa nyuki kwa kuonesha chakula kilipo ikiwa ni paoja na umbali pamoja na upande chakula kilipo.Nyuki huyu hucheza kwa kuzingatia upande jua lilipo kwani nyuki hutumia jua ili kwa ajili ya kwenda na kurudi kwenye chakula.




 Hiki ni kitenga malikia kilichotengezwa kwa mali bhafi zetu wenyewe.kimetengezwa kwa kutumia mbao laini ambazo zimechingwa kwa ustadi wa hali ya juu.
ELIMU YA UTUMIAJI WA MIZINGA YA KISASA NI MUHIMU.
Wanavikundi wa ufugaji nyuki kutoka Babati Manyara wakiwa pamoja na maofisa wa FARM AFRICA walipotembelea kiwanda cha kusindika asali kinachomilikwa na Kampuni ya Honey King Kilichopo Visiga madafu kwa ajili ya kupata maelezo mbali mbali ya jinsi kiwanda na kampuni ya Honey King kwa ujumla jinsi inavyofanya kazi zake.Mwenye shati nyeusi ni Segunda Lesilwa (mtaalamu wa nyuki kutoka kampuni ya Honey King)

3 comments:

  1. Hii imekaa vizuri. Uhamasishaji ukiendelea eneo hili litasidia wananchi wengi kiuchumi na kijamii

    ReplyDelete
  2. Nina nyuki wamevamia nyumbani kwangu miaka 10 nikiwaondoa warudi nisaidie

    ReplyDelete