Maisha ya Nyuki



Nyuki ni mdudu mwenye mabawa manne angavu na mwiba nyuma ya mwili wake anayekusanya mbelewele ya maua kama chakula chake. Aina inayojulikana hasa ni nyuki wa asali wa familia apis. Kuna spishi zaidi za 20,000 zinazojumlishwa na biolojia kati ya nyuki lakini ni wale wa jenasi apis wanaokusanya asali inayovunwa na wanadamu.

Nyuki za asali mara nyingi wanafugwa lakini wengine wanaishi porini na asali yao inakusanywa kwa kuvunja mzinga wao. Katika Afrika kwa jumla sehemu ya asali bado inatokana na nyuki asali wa porini lakini ufugaji nyuki unapanua.



Mwili wa nyuki
Mwili una pande tatu jinsi ilvyo kwa wadudu wote: kichwa mbele, kidari katikati na tumbo nyuma, halafu jozi tatu za miguu na jozi mbili za mabawa.
Mwili huwa na nywele na ina rangi kali za njano-nyeusi kama onyo dhidi ya maadui.
Nyuma ya tumbo wanabeba mwiba wanaotumia kudunga wakijisikia wameshambuliwa. Wakidunga mwiba wanaingiza pia kiasi kidogo cha sumu katika kidonda. Sumu hii inasababisha maumivu na watu wengine wanaathiriwa vikali lakini si kila mtu. Kuna nyuki wanaokufa baada ya kudunga kwa sababu mwiba unabaki kwenye kidonda lakini wengine wanaweza kutoa mwiba na kudunga tena.
Wadudu wa kijamii
Nyuki asali ni wadudu wa kijamii maana yake wanaishi katika kundi si peke yao kama aina nyingine za nyuki. Wanajenga sega ya nta ndani ya mzinga wa nyuki na humu wanatunza asali yao.
Kuna aina tatu za nyuki ndani ya kundi na mzinga wao ambao ni
  • malkia wa nyuki ni mama wa nyuki wote ndani ya kundi na kazi yake ni kutega mayai pekee
  • nyuki wafanyakazi ni wakazi wengi wa mzinga na wote ni wa kike. Ni hao wanaofanya kazi yote kama kukusanya mbelewele, kusafisha mzinga, kutengeneza nta , kujenga sega, kumlisha malkia na wadogo, kultetea mzinga
  • nyuki dume ni wachache na kazi yao ya pekee ni kuzaa na malkia; baadaye wanafukuzwa kwenye mzinga na hawapewi chakula tena
Spishi na nususpishi za Afrika
Spishi za Asia

    Nyuki ni wadudu wanaokaa pamoja. Hufanya kazi pamoja na ulinzi wa maisha ya kila mmoja wao katika jamii unaimarishwa. Kuna aina tatu ya nyuki katika jamii na kila mmoja ana kazi yake, kwa ujumla nyuki ni wadudu ambao ni rafiki wa binadamu isipokuwa huwa wanakasirika sana pale wanapofanyia vitendo tofauti na wanavyotaka.
    Katika aina tatu za nyuki katika kundi moja yupo malikia mmoja, nyuki watenda kai na nyuki dume.Na kila mmoja ana kazi yake pekee katika mzinga au kundi zima.

                                                             MALIKIA WA NYUKI
    Huyu ni malkia na ni mmoja pekee katika jamii. Yeye ndiye ‘mama nyuki’ kazi yake ni kutaga mayai yatakayotoa nyuki wapya. Anaweza kutaga mayai 1000 kila siku katika wakati Fulani wa mwaka.Malikia huyu hutaga maai kwa wingi hasa unapokaribia msimu wenye chakula kwa wingi.Malikia huanza kutaga mayai kwa wingi ili kukuza kundi na kuweza kupata watenda kazi wengi ambao wataweza kukusana chakula kwa wingi pindi msimu wenye chakula kwa wingi ukifika.

                                                                  NYUKI DUME

    Huyu ni nyuki dume. Kazi yake hasa ni kumtia malkia mchanga mimba. Kuna karibu
    dume 500 kwenye mzinga wakati kuna chakula cha kutosha. Wao hufukuzwa wakati
    wa upungufu wa chakula, kwani huonekana kama hawana kazi yoyote ya kufanya katika mzinga kipindi ambacho chakula huwa kichache.Kwa kawaida msimu ambao chakula huwa kichache malikia huimamisha kabisa utagaji wa mayai kwa ajili ya kuongeza kundi hivyo hatahitaji kupandwa tena msimu huo mpaka msimu unaokuja.Sababu hii ndio huwa inasababisha nyuki dume wafukuzwe au kuuwa kipindi hicho.

                                                       NYUKI WATENDA KAZI.
    Huyu ni nyuki mtenda kazi. Yeye ni wa kike lakini hawezi kutaga mayai yaliyorutubishwa kama malikia.Hutaga maai mara chache sana ambayo hayajarutubishwa na mara nyingi tokeo la yai atakalotaga nyuki huyu huwa anazaliwa nyuki dume. Yeye ndiye
    hufanya kazi yote kwenye mzinga. Idadi yao inaweza kufikia kama 40,000 wakati wa
    kutengeneza asali.Kwa ujumla huyu ndie mtendaji mkuu wa kazi zote za kundi ikiwa ni pamoja na kutafuta chakula, kufanya usafi wa ndani, kulisha malikia na watoto na madume, kutuliza joto pindi linapozidi na ulinzi wa kundi.
                                       UTAGAJI WA MAYAI KWA MALIKIA
    Kwa kawaida malikia huweza kutaga mayai zaidi ya 1000 kwa kila siku.Utagaji huo wa mayai huwa na utaratibu maalumu yaani yai moja atika kila chumba cha sega.

    mara baada ya kutaga yai hilo hukaa kwa siku mbili hadi tatu na kuanguliwa kwa hatua nyingine ya buu.
    mara baada ya kufikia hatua hii nyuki hufunika juu kwa nta hadi yanapoanguliwa kwa hatua ya kiluwiluwi.Nyuki wanapokuwa hatua hii hulishwa chakula maalumu na nyuki watenda kazi.
    huendelea kukua ndani kwa ndani.Nyuki wanapokuwa katika hatua ya kiluwiluwi huwa hali chakula chochote hadi pale anapoanguliwa na kuwa nyuki kamili ndip anapoanza kula.Mara baada ya kuwa nyuki kamili hutoboa juu kulikozibwa kwa nta na kutoka nje ya sega, hatimaye amekuwa nyuki kamili.
    hapo tayari amekuwa nyuki kamili na sasa yupo tayari kwa kazi za kila siku za nyuki.

    UTENGENEZAJI WA SEGA.
    Nyuki hutengeneza sega kwa kutumia nta, Nta ni majimaji yaliyo kwenye mfumo wa mafuta ambayo nyuki hutoa katika mwili wake kwa ajili ya kutengeneza sega.Huwa wanafanya kama wanajivua nguo kwa kutumia miguu yako hadi hutokea sega kamili.Kwa kawaida hufanya kazi hii kwa ushirikiano wa hali ya juu ili kuhakikisha kazi hii inaenda haraka na uanza kuhifadhi chakula.
    UTAFUTAJI WA CHAKULA
    kwa kawaida kila kunapokucha nyuki huruka huku na kule kwa ajili ya kutafuta chakula watachokipenda wao.Mara baada ya kupata chakula hubeba na kupeleka kati nyumba zao.

    Pindi akifika katika nyumba yao huanza kubadilishana chakula kile kabla hajahifadhi ili kila mmoja ajue ladha ya chakula kile.
    Iwapo wengi wataipenda ladha ile nyuki yule huanza kuonesha ishara ya kuwaelekeza wengine upande na umbali wa chakula kilipo.Nyuki wengine huweza kutoka nje na kwenda kuchukua kile chakula bila kwenda na yule aliyewaelekeza.Kumbuka hatua zote hizi za kuelekezana juu ya umbali na upande chakula kilipo hutumia hasa upande jua lilipo.
    huendelea kucheza kwa kuonesha umbali na upande ambao chakula hicho kitamu kinapatikana
    lakini pia jua ndio huwa kiongozi chao kikubwa sana wanachotumia ili kuweza kujua wapi chakula kilipo lakini pia jua hili hilo huweza kuwasaidia wasiweze kupotea pindi wanaporudi katika nyumba yao.
    Mara baada nyuki kumaliza kuchukua chakula a kuhakikisha kuwa sega lote limejaa asali nyuki huanza kuziba matundu yote ya sega kwa kutumia nta.Asali hii huwa ndio asali iliyoiva na hapo inakuwa tayari kwa kuvunwa.


    8 comments:

    1. Kiuhalisia nyuki hutumia mda gani kutengeza hasali

      ReplyDelete
    2. Asanteni Sana nimevutiwa mmno kwa hii Habari ya nyuki

      ReplyDelete
    3. Nashukuru sana kutembelea ukurasa wenu, nimependa na nataka kuanza kazi hii mara moja. Niko Kahama naomba nipe ushirikiano

      ReplyDelete
    4. Naomba nifahamishwe nijue jina la mwiba atumiwayo nyuki kudungia

      ReplyDelete
    5. Kwa mwaka nyuki anatengeneza Asali mala ngapi?

      ReplyDelete