Mavazi ya Nyuki

Kwa ujumla mavazi ya nyuki ni kitu cha muhimu sana katika kazi za ufugaji nyuki wa kisasa.Kila mtu anapokwenda katika mzinga wenye nyuki kwa ajili ya ukaguzi au uvunaji wa mazao ya nyuki ni vyema akavaa mavazi ya kuzuia nyuki kumuuma.
Kuna aina nyingi za mavazi ya kuzuia nyuki kuuma.Kuna yale yaliyotengenezwa kisasa na kuna yale yanayotengenezwa kwa kutumia malighafi zilizopo.

JINSI YA KUTENGENEZA NGUO ZA KUKINGA NYUKI KUUMA.
Njia rahisi na ya haraka ya kutengeneza nguo ya kuzuia nyuki kuuma ni ile ya kutumia mifuko ya plastiki au salfeti.

Nguo hizi huwa imara sana na ni rahisi sana kutengeneza.
Hatua za kutengeneza nguo hizo ni kama ifuatavyo.

1.Chukua mfuko wako ukunjue na ulaze chini.

2.Mara baada ya kulaza chini, chukua mkasi wako na anza kukata mfuko wako kwa uefu na kwa upana ili kupata vipande vinne ambavyo vitakuwezesha kupata vizuia nyuki vinne.
3.Tenganisha kabisa vipande hivyo ili kuopata hivyo vipande vinne.

4.Mara baada ya kukata, chukua nyavu yenye matundu madogo madogo hasa ile inayotumika kwenye kuzuia mbu.
5.Weka mkunjo mzuri kati ya kipande chako cha mfuko na nyavu yako uliyoiandaa.

6.Tumia nyuzi ngumu kwa kushonea na hakikisha unashona kwa karibu karibu ili kuzuia kabisa nyuki kupenya wakati unafanya kazi za nyuki.
7.Hapo nguo yako ya kuzuia nyuki kukuuma kichwani itakuwa imekamilika.Ni imara na salama kabisa.

8 comments:

  1. nomba kufahamishwa wapi nitapata kifaa cha kupulizia moshi

    ReplyDelete
  2. naomba kufahamu ni wapi nitapata mavazi ya nyuki yanayouzwa.

    ReplyDelete
  3. Kifaa cha kipulizio au BEE SMOKER unaweza kupata kutoka kwetu inategemea unahitaji ngapi

    ReplyDelete
  4. Mi nahitaji mavazi ya kisasa ya kulinia asali pamoja na kifaa cha kupulizia moshi

    ReplyDelete
  5. Mi nahitaji mavazi ya kisasa ya kulinia asali pamoja na kifaa cha kupulizia moshi

    ReplyDelete
  6. Naomba namba zenu nahitaji mavazi kwa ajili ya kulinia asali0

    ReplyDelete
  7. 0799178459 naomba kuwasiliana na wabobezi wa nyuki

    ReplyDelete